fatakifataki
Senior Member
- Nov 2, 2009
- 134
- 60
Nimepita katika hospitali kadhaa katika pilika zangu za utafutaji rizki. Nimeona katika mageti mengi ya hospitali za wilaya, mikoa, hasa zile za rufaa za mikoa, vituo vya afya pia, kunakuwa na maaskari ama wawili ama mmoja magetini ambaye yeye kazi yake ni kuuliza unayo barakoa? Wengi wao akijibiwa sina anakujibu kanunue barakoa kisha ndipo uingie ndani ya hospitali.
Jambo la kushangaza hata wao askari hao unakuta hawavai kabisa hizo barakoa. Nje ya geti pale unakuta barakoa limeshonwa shonwa na mwananchi hivi amelishika mkononi anakwambia anauza elfu moja. Kwa kuwa una shida hospitali unalazimika kununua ile barakoa ndipo anakuruhusu kuingia.