Mageuzi mifumo ya Serikali

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Rais Samia Suluhu amesema ndani ya miezi sita kuanzia sasa mifumo ya kiteknolojia inayoundwa na serikali itampa uwezo wa kufuatilia taarifa zote za taasisi za umma zikiwemo za bandari.

Ili kukuza biashara ni lazima mifumo yote ya serikali isomane na taarifa zioane kwani mifumo iliyopo sasa haisomani na kusababisha baadhi ya changamoto.

Maboresho ya mifumo hiyo ni muendelezo wa adhima ya Rais Samia wa kuiinua sekta binafsi nchini kwa kuwatengenezea mazingira bora ya biashara ili kuinua uchumi wa taifa kwani wao ndio wanafanya biashara na si serikali.
 
Amekomaa kweli na hilo la mifumo kusomana, hiyo ni excuse tu ya wasaidizi wake. Yes, ni muhimu mifumo kusomana lakini hilo sio kiini cha matatizo.

Taarifa zote unazozihitaji zipo hata huko kwenye hiyo mifumo isiyosomana, nini kinasababisha zisifanyiwe kazi?

Kuwa na data ni jambo moja, kuchata hizo data na kuzigeuza kuwa taarifa (information) ni jambo lingine. Kutengeneza maana ya taarifa unazozipata na kuweza kufanya maamuzi ni jambo tofauti pia.

It's a mundane, boring task, inahitaji mtu mchapa kazi, mwenye akili nyingi na moyo wa kufuatilia bila kuchoka, kama alivyokuwa JPM.

If you can't use the data you have now, hiyo mifumo kusomana won't make any difference. Your people will just come up with another excuse as to why things aren't working out.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…