Nicolas J Clinton Gabone
JF-Expert Member
- Mar 13, 2014
- 897
- 559
MAGEUZI YA MUONEKANO WA VIWANJA VYA UHURU NA BENJAMIN MKAPA KUELEKEA CAF 2027
Imeandaliwa na, Nicolas Jovin Clinton Gabone
Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wameshiriki kikamilifu katika ukarabati wa viwanja vikuu vya Uhuru na Benjamin Mkapa, wakiweka mkazo mkubwa kwenye miundombinu ya ndani. Ukarabati huu umejikita kwenye pitch, viti, taa, vyumba vya wachezaji na mahitaji ya mashindano ya kitaifa na kimataifa. Hata hivyo, muonekano wa nje wa viwanja hivi umebakia ule ule, hali inayozua hatari ya kupoteza fursa ya kiuchumi na branding, hasa tukikabiliwa na mashindano ya CAF 2027.
Mashindano ya CAF 2027 yatakuwa tukio la kimataifa, likilenga mashabiki wa bara zima na waandishi wa habari, udhamini na watalii. Katika muktadha huu, uso wa viwanja vya Uhuru na Lupaso hauwezi kuonekana wa kawaida au wa mazoea, bali lazima uakisi hadhi ya mashindano na taifa lenyeji na lenye ligi kuu kubwa na yenye kuvutia mitaji mikubwa ya fedha.
TATIZO KUU
Muonekano wa nje
1. Uwanja wa Mkapa na Uhuru, licha ya ukarabati wa ndani, haujaakisi muundo wa kisasa unaovutia macho ya mashabiki, udhamini, utalii au vyombo vya habari.
2. Muonekano wa nje ni kipimo cha kwanza cha branding ya taifa, bila mageuzi hayo, Tanzania inakosa fursa ya kiuchumi, kibiashara na utalii.
Barabara na mazingira ya kuingia
1. Barabara zinazoingia viwanjani hazina hadhi, hazina mandhari ya michezo na haziwezi kuunda hisia za tukio kubwa, hasa TAIFA ROAD
2. CAF 2027 inahitaji uzoefu na ubunifu kamili wa mashabiki, kuanzia wanapokuwa njiani hadi kuingia uwanjani. Hali ya sasa inapunguza thamani ya tukio na taswira ya Tanzania.
Michezo kama biashara na branding
1. Viwanja vya Uhuru na Mkapa lazima vionekane kama bidhaa ya kisasa, jukwaa la matangazo, chombo cha taswira ya taifa na sehemu ya kuendeleza soko la michezo na utalii wa kimataifa.
2. Muonekano wa nje unaathiri moja kwa moja mvuto wa udhamini, matangazo, na heshima ya ligi na taifa lenyeji.
Ukubwa wa Ligi ya Tanzania
Ligi Kuu ya Tanzania ina mashabiki wengi na ushindani mkubwa. Viwanja vikuu vinapaswa kuwa kielelezo cha ubora wa ligi, siyo tu kwa ndani bali pia kwa muonekano wa nje. Hali ya sasa inapingana na ukubwa wa ligi na matarajio ya mashabiki.
MAPENDEKEZO YA HARAKA
Mageuzi ya muonekano wa nje
1. Kuboresha facade za viwanja, mabango, taa za nje na mandhari ya kuingia uwanjani.
2. Kutengeneza uso unaovutia mashabiki na wadhamini kabla hata ya mpira kuchezwa.
3. Kuboresha barabara kuu zinazoingia viwanjani, ukizingatia alama za michezo, mitaa ya kuishi tukio na urahisi wa usafiri.
4. Kuongeza ifadhi ya magari, taa na signage zinazowezesha uzoefu mzuri wa mashabiki na wageni wa kimataifa.
5. Viwanja viwe na alama ya kipekee ya taifa, ikionyesha Tanzania kama mwenyeji makini wa mashindano ya kimataifa.
6. Kuunda sehemu za matangazo, vipindi vya waandishi wa habari, na nafasi za biashara ndogo ndogo zinazojumuisha bidhaa za kienyeji na utalii.
Nimalize kwa kusema, CAF 2027 ni fursa ya kihistoria kwa Tanzania kuonesha uwezo wake kama mwenyeji wa mashindano ya kimataifa. Hata hivyo, ukarabati wa ndani pekee bila mageuzi ya muonekano wa nje na barabara za kuingia viwanjani unazidisha hatari ya kupoteza fursa ya kibiashara na branding.
Serikali na TFF zinashauriwa kuchukua hatua haraka za kuboresha muonekano wa viwanja vya Uhuru na Mkapa na mazingira yanayoyazunguka, ili mashindano ya CAF 2027 yawe ushahidi wa hadhi, ubora na mtazamo wa kimataifa wa Tanzania.
Na, Nicolas Jovin Clinton Gabone
Dar es Salaam,
3rd January 2026.