Maghorofa 64 hatarini kuanguka Kariakoo

Maghorofa 64 hatarini kuanguka Kariakoo

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Maghorofa 64 yaliyopo eneo la Kariakoo, Manispaa ya Ilala yamejengwa kinyume na sheria na kwamba baadhi yanaweza kuporomoka kutokana na ujenzi wake kuwa chini ya kiwango.

Kampuni iliyopewa zabuni ya kufanya ukaguzi wa majengo Manispaa ya Ilala, inayoitwa Design Plus Architects (DPA) imebaini kati ya majengo ya ghorofa 90 yaliyokaguliwa, 67 yamejengwa kinyume na sheria.

Uamuzi wa kuipa kampuni binafsi kazi ya kukagua majengo, ulikuja baada ya jengo la ghorofa 16 kuanguka na kuua watu 36 Machi 26, mwaka huu.

Meneja Uendeshaji wa DPA, Mustafa Maulid alisema jana kwamba ukaguzi wa majengo hayo ulianza Julai mwaka huu baada ya kupata zabuni hiyo.

“Hali ni mbaya katika majengo tuliyoyakagua, kuna majengo ya ghorofa yenye nyufa nyingi, pia yapo majengo yanayogusana ambayo ni hatari kwa watumiaji,” alisema.

Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alipoulizwa hatua za kuchukua, alisema vikao vya madiwani vitaamua hatua za kuchukua baada ya kuipitia ripoti ya ukaguzi huo.

“Ukipita Kariakoo hata kama siyo mtaalamu wa ujenzi utagundua kwamba majengo mengi yamejengwa bila kufuata sheria za ujenzi, baada ya kuanguka kwa jengo katikati ya jiji, tukaamua kuipa kampuni binafsi kazi ya ukaguzi ili kuona ni majengo gani yapo kinyume na sheria,” alisema Silaa.

Akifafanua zaidi, Maulid alisema makosa waliyoyabaini ni watu kuendesha ujenzi bila kuwa na vibali.

Alisema makosa mengine ni ujenzi bila kufuata michoro iliyoidhinishwa na Manispaa ya Ilala.

“Hii ina maana kwamba watu wanajenga majengo tofauti na michoro inayotoka kwa wataalamu wa manispaa. Kwa mfano majengo yote Kariakoo yanatakiwa kuwa na maegesho ya magari lakini wao wanaweka flemu za maduka,” alisema Maulid.

Pia, alisema watu wanahamia kwenye maghorofa kabla hayajaisha kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

Kuhusu changamoto walizokutana nazo, Maulid alisema baadhi ya wamiliki wa nyumba walikuwa wakiwazuia kuingia kufanya ukaguzi, huku wengine wakikimbilia kushtaki kwa wanasiasa.

Alisema wengine wamekuwa wakiwatishia kwa lengo la kuwazuia kufanya kazi hiyo na kwamba, wataendelea na kazi hiyo hadi wamalize.

CHANZO:Mwananchi.

MY TAKE:
Tusubiri janga lingine litokee alafu tume iundwe kuchunguza.

Hii ni moja ya matumizi bora kabisa ya kodi zetu!
 
Magorofa 67 yaliyopo eneo la Kariakoo Manispsaa ya Ilala yamejengwa kinyume cha sheria na taratibu na kwamba baadhi yake yanaweza kuanguka wakati wowote.

Kampuni iliyopewa zabuni ya kufanya ukaguzi wa majengo,Design Plus Architects(DPA) imesema kati ya majengo ya gorofa 90 yaliyokaguliwa 67 yalijengwa bila kuzingatia sheria na kanuni za ujenzi.

Meya wa Manispaa ya Ilala Jery Slaa amesema baraza la madiwani litakutana kujadili taarifa hiyo.

CHANZO:Mwananchi.

MY TAKE:
Tusubiri janga lingine litokee alafu tume iundwe kuchunguza.

Hii ni moja ya matumizi bora kabisa ya kodi zetu!
Hii ni post iliyoandikwa miaka 10 iliyopita, mpaka leo hii hakuna kitu kiliwahi kufanyika, na huenda hata hilo ghorofa lililoanguka jana ni miongoni mwa maghorofa yaliyokaguliwa.

CCM ni laana katika hii nchi.
 
20241117_121043.jpg
 
Na Mm nitaanzisha mada nikisema kiongozi fulani atakufa, halafu baada ya miaka 10 akifa watu waje waniite nabii kwa kutabiri hicho kifo.

Au

Nitabiri kuwa ipo siku simba itashinda kombe la ligi kuu halafu baada ya misimu miwili ashinde halafu mje mniite nabii
 
Back
Top Bottom