Afcon 2027
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 309
- 579
😀😀😀😀Hayo magorofa wayaweke alama watu wapite nayo mbali
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😀😀😀😀Hayo magorofa wayaweke alama watu wapite nayo mbali
Ova
Hakika Mkuu. Kwa DareS Salaam ni hatari sana kuishi kwenye maghorofa na hasa ya Kariakoo.Dar sio sehemu salama ya kuwa Juu ya gorofa.
Huku Mikoani hakuna ujenzi wa kisenge kama huko
Hebu nisomee ulichoandika.Amiina.. kama viongozi ndio kina chalamila na mwanaFA wao kitwa nikumahukuru mama yao
KushuhukuruHebu nisomee ulichoandika.
Maghorofa 64 yaliyopo eneo la Kariakoo, Manispaa ya Ilala yamejengwa kinyume na sheria na kwamba baadhi yanaweza kuporomoka kutokana na ujenzi wake kuwa chini ya kiwango.
Kampuni iliyopewa zabuni ya kufanya ukaguzi wa majengo Manispaa ya Ilala, inayoitwa Design Plus Architects (DPA) imebaini kati ya majengo ya ghorofa 90 yaliyokaguliwa, 67 yamejengwa kinyume na sheria.
Uamuzi wa kuipa kampuni binafsi kazi ya kukagua majengo, ulikuja baada ya jengo la ghorofa 16 kuanguka na kuua watu 36 Machi 26, mwaka huu.
Meneja Uendeshaji wa DPA, Mustafa Maulid alisema jana kwamba ukaguzi wa majengo hayo ulianza Julai mwaka huu baada ya kupata zabuni hiyo.
“Hali ni mbaya katika majengo tuliyoyakagua, kuna majengo ya ghorofa yenye nyufa nyingi, pia yapo majengo yanayogusana ambayo ni hatari kwa watumiaji,” alisema.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alipoulizwa hatua za kuchukua, alisema vikao vya madiwani vitaamua hatua za kuchukua baada ya kuipitia ripoti ya ukaguzi huo.
“Ukipita Kariakoo hata kama siyo mtaalamu wa ujenzi utagundua kwamba majengo mengi yamejengwa bila kufuata sheria za ujenzi, baada ya kuanguka kwa jengo katikati ya jiji, tukaamua kuipa kampuni binafsi kazi ya ukaguzi ili kuona ni majengo gani yapo kinyume na sheria,” alisema Silaa.
Akifafanua zaidi, Maulid alisema makosa waliyoyabaini ni watu kuendesha ujenzi bila kuwa na vibali.
Alisema makosa mengine ni ujenzi bila kufuata michoro iliyoidhinishwa na Manispaa ya Ilala.
“Hii ina maana kwamba watu wanajenga majengo tofauti na michoro inayotoka kwa wataalamu wa manispaa. Kwa mfano majengo yote Kariakoo yanatakiwa kuwa na maegesho ya magari lakini wao wanaweka flemu za maduka,” alisema Maulid.
Pia, alisema watu wanahamia kwenye maghorofa kabla hayajaisha kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kuhusu changamoto walizokutana nazo, Maulid alisema baadhi ya wamiliki wa nyumba walikuwa wakiwazuia kuingia kufanya ukaguzi, huku wengine wakikimbilia kushtaki kwa wanasiasa.
Alisema wengine wamekuwa wakiwatishia kwa lengo la kuwazuia kufanya kazi hiyo na kwamba, wataendelea na kazi hiyo hadi wamalize.
CHANZO:Mwananchi.
MY TAKE:
Tusubiri janga lingine litokee alafu tume iundwe kuchunguza.
Hii ni moja ya matumizi bora kabisa ya kodi zetu!
Muda huu hapa kariaakoo mh rais kagusia ripoti hii..Maghorofa 64 yaliyopo eneo la Kariakoo, Manispaa ya Ilala yamejengwa kinyume na sheria na kwamba baadhi yanaweza kuporomoka kutokana na ujenzi wake kuwa chini ya kiwango.
Kampuni iliyopewa zabuni ya kufanya ukaguzi wa majengo Manispaa ya Ilala, inayoitwa Design Plus Architects (DPA) imebaini kati ya majengo ya ghorofa 90 yaliyokaguliwa, 67 yamejengwa kinyume na sheria.
Uamuzi wa kuipa kampuni binafsi kazi ya kukagua majengo, ulikuja baada ya jengo la ghorofa 16 kuanguka na kuua watu 36 Machi 26, mwaka huu.
Meneja Uendeshaji wa DPA, Mustafa Maulid alisema jana kwamba ukaguzi wa majengo hayo ulianza Julai mwaka huu baada ya kupata zabuni hiyo.
“Hali ni mbaya katika majengo tuliyoyakagua, kuna majengo ya ghorofa yenye nyufa nyingi, pia yapo majengo yanayogusana ambayo ni hatari kwa watumiaji,” alisema.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alipoulizwa hatua za kuchukua, alisema vikao vya madiwani vitaamua hatua za kuchukua baada ya kuipitia ripoti ya ukaguzi huo.
“Ukipita Kariakoo hata kama siyo mtaalamu wa ujenzi utagundua kwamba majengo mengi yamejengwa bila kufuata sheria za ujenzi, baada ya kuanguka kwa jengo katikati ya jiji, tukaamua kuipa kampuni binafsi kazi ya ukaguzi ili kuona ni majengo gani yapo kinyume na sheria,” alisema Silaa.
Akifafanua zaidi, Maulid alisema makosa waliyoyabaini ni watu kuendesha ujenzi bila kuwa na vibali.
Alisema makosa mengine ni ujenzi bila kufuata michoro iliyoidhinishwa na Manispaa ya Ilala.
“Hii ina maana kwamba watu wanajenga majengo tofauti na michoro inayotoka kwa wataalamu wa manispaa. Kwa mfano majengo yote Kariakoo yanatakiwa kuwa na maegesho ya magari lakini wao wanaweka flemu za maduka,” alisema Maulid.
Pia, alisema watu wanahamia kwenye maghorofa kabla hayajaisha kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kuhusu changamoto walizokutana nazo, Maulid alisema baadhi ya wamiliki wa nyumba walikuwa wakiwazuia kuingia kufanya ukaguzi, huku wengine wakikimbilia kushtaki kwa wanasiasa.
Alisema wengine wamekuwa wakiwatishia kwa lengo la kuwazuia kufanya kazi hiyo na kwamba, wataendelea na kazi hiyo hadi wamalize.
CHANZO:Mwananchi.
MY TAKE:
Tusubiri janga lingine litokee alafu tume iundwe kuchunguza.
Hii ni moja ya matumizi bora kabisa ya kodi zetu!
Si alikuwepo wakati imeshatoka? Au mpaka "WAFE" ndo tunaibuka?Muda huu hapa kariaakoo mh rais kagusia ripoti hii..
Ahsante mama ifanyiwe kazi sasa.
Na iwe na vochaTuseme ukiingia ghorofa lolote kariakoo, utakapotoka ndio ujue upo salama. Hakikisha simu yako imejaa charge.
Wengi hamkumuelewa alipoigusia hiyo ripoti.Muda huu hapa kariaakoo mh rais kagusia ripoti hii..
Ahsante mama ifanyiwe kazi sasa.