Magical Kenya!

Magical Kenya!

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
t_1505398296383_name_Screen_Shot_2017_09_14_at_10_08_52_AM.png
Wanasayansi kutoka kote duniani wametua kwenye 'Conservancy' ya Hirola, gatuzi la Garissa, Kenya, baada ya Twiga mweupe aliyeonekana kwa mara ya kwanza mwaka wa 2017 kuzaa twiga mweupe, kwa mara ya pili. Twiga weupe wamekuwa watatu sasa kwa 'span' ya miaka isiyozidi miwili. Ya mungu ni mengi, twiga hao wanasemekana kwamba sio zeruzeru na inakisiwa kwamba wana 'genetic disorder' ambayo wameirithi kwa miaka mingi. Fursa za kujitangaza na kutangaza vivutio vyetu vya kiutalii zinaendelea kuongezeka kila uchao. Karibuni Kenya wadau mje mjionee haya maajabu kwa macho yenu mawili.
 
Safi sana. Muifatilie na hii kama wakenya na KWS walivom'track' hadi akaingia Serengeti, hivi ni vitu ambavyo sio vya kupuuzwa. Kule S.A walimuona punda milia kama huyo alafu wakamnasa, binadamu buana!
 
Safi sana. Muifatilie na hii kama wakenya na KWS walivom'track' hadi akaingia Serengeti, hivi ni vitu ambavyo sio vya kupuuzwa. Kule S.A walimuona punda milia kama huyo alafu wakamnasa, binadamu buana!

Huko kwao atatoweka kama alivyotoweka faru John.....
 
Kuna mtu amebonyeza 'panic button'. [emoji1] Baada ya kuona media za kimataifa zikiwaita twiga hawa 'the only purely white girraffes in the world'. Yaani walifatilia twiga huyo muda wote huo, wakingoja kuona kama atazaa twiga mweupe. KWS nao hawakulala darasani, waliwapa update baada ya update baada ya update. 😎
 
Back
Top Bottom