PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Ndoto za waliokuwa wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Catherine Magige na Zaytun Swai, kurejea bungeni zimeingia doa baada ya kushindwa kushawishi wajumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) mkoani humo katika kura za maoni zilizofanyika mjini Arusha.
Katika uchaguzi huo uliomalizika usiku wa kuamkia Julai 31, 2025, Martha Gido ameibuka kinara kwa kura 1,004, akifuatiwa na Chiku Athman aliyepata kura 775 kati ya kura halali 1,245.
Magige amepata kura 213 na Swai 141, matokeo yanayowaweka njia panda kisiasa. Wagombea wengine walikuwa ni Asanterabi Lowassa (196), Navoi Mollel (95), Martha Amo (50) na Lilian Badi (9).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na msimamizi wa uchaguzi huo, Kenani Kihongosi amesema jumla ya wapigakura walikuwa 1,261, kura halali 1,245 na saba zikiwa zimeharibika. Amesisitiza mshikamano baada ya uchaguzi huo uliofanyika kwa utulivu na demokrasia.
Chanzo: Mwananchi Digital