Magimbi ya Nazi

Magimbi ya Nazi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Pishi hili ni maalum kabisa kwa wale ambao ni wageni jikoni au hawajui kupika.Niliomba nipewe pishi la futari ambalo hata asiejua kupika anaweza jaribu na akapatia,nikapewa pishi hili.



Mahitaji

  • Magimbi
  • Nazi,tengeneza tui zito na jepesi
  • Chumvi

Njia

1.Menya na osha vizuri
2. Chemsha na tui jepesi (Tui la pili),yakiiva kabla hayajalainika weka chumvi na tui la kwanza (tui zito).Chemsha adi tui liive na magimbi yawe laini sana.Tui lisikauke,acha liwe rojo jingi.Tayari kwa kula.
-ukipenda unaweza weka nyama au mboga mboga zozote.
 
Mkwe hii kama umeshawahi weka hapa

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Nlikula hii kitu Jana aisee imeenda shule kinoma noma hata wabeba box hawaijui hii
 
Gimbi kwa nyama iwe lainii... na achari ya ndimu/mbirimbi....
 
Aisee yaani huwa nayapita tu haya sokoni kwasababu sijui kuyapika,nakiri umenitendea haki kwa hili somo santeeee.
Nalog off
 
Back
Top Bottom