Magoli 10 ya kufungwa katika mechi mbili,Simba inabaki vipi kama ilivyo?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
  • Kocha hajafukuzwa
  • Benchi la Ufundi halijaguswa
  • Wachezaji hawajachunguzwa au kuwajibishwa
  • Viongozi hawajafukuzwa wala kuhojiwa
Timu iliyofungwa na Simba katika mechi ya kwanza ilishamtimua Kocha wake. Sasa inapata matokeo. Imetoa sare na wababe wote wa Simba.

Simba kuweni serious. Hii ni Klabu Bingwa Barani Afrika. Mnatuwakilisha Tanzania. Mkiaibishwa tunaaibishwa sote. Mkifanikiwa na kupata sifa tunapata sifa sote.

Simba haiwezi kubaki kama ilivyo sasa!
 
Sidhani kama suluhisho ni kufukuza kocha au kupangua benchi la ufundi (unless sababu za vipigo hivyo ni hao watu na ni za makusudi)

Kila team huwa inafungwa, cha muhimu ni kujitathmini ni wapi hapakuwa sawa ili kujirekebisha next time out.

Ukisema kufukuza fukuza zingatia mikataba n.k inaweza kuiweka club katika hali ambayo sio nzuri (financially)
 
10 bila.
5 congo na timu ilisheheni wachezaji MAPROFESSIONALS wa nje, jana timu karibu wachezaji saba ni foreigners, mnapigwa tena 5. Wanaosajili pia wachunguzwe, haiwezekani timu ina foreigners 8 kwenye first eleven inapigwa 10 bila.
 
Mpira na Siasa ni vitu ambavyo ukivishabikia, hautaishiwa fedheha. Hasa hizi nci zetu na mpira wa Tanzania. Hata timu ikishinda, ni kama kubahatisha tu.
 
Kufukuza ni muhimu Mkuu Jana wachezaji 9 kati ya 11 walionza ni proffesion players tumewatoa nje kwa ajili ya mashindano kama haya ya caf afu mechi mbili 2 magoli km yote kuna haja ya kuwapiga chini hawa wachezaji aisee!!!! Na pia mooo kazungukwa na mapiga pesa tu sidhan km tutaboa kwa simba hii
 
Mkuu mpira umeanza lini kuujua? Samahani kwa swali hilo ila sina nia ya kukudharau ila nashangaa kuona kuwa Simba kufungwa goli 10 ndani ya dakika 180 ni jambo la ajabu hasa ukizingati aina za team tulizocheza nazo.

Hii haina tofauti na na Ulaya kule ukute team labda ya Romania huko CFR Cluj imequalify kucheza CL alafu iko group moja na top dogs wa Ulaya labda Barca na team nyingine tuchukue hata Schalke 04. Hapo unategemea Cluj watafurukuta vipi?

Tuweni realistic jamani, tuliposhinda ile mechi ya mwanzo watu mlikua na over expectations. Mlikua delusional.
 
Huyu kocha abaki kwa gaharama yoyote ile ili maandiko yatimie, abakie hivyo hivyo mpaka Al Ahly na As Vita waje Dar kumalizia kazi yao nzur waliyoianza huko, halafu kuna 5 nyingine zinanukia kule Algeria kikubwa tegeni sikio.
Halafu Mo hajawahi kusaidia timu yoyote anapokuwa mmiliki au mtu mwenye maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpira ni uwekezaji wenzetu wamewekeza vizuri kwa miaka mingi sisi Simba ndio tunaanza uwekezaji na mkataba aliosaini kocha wa Simba ni kuhakikisha timu inafika kwenye makundi msimu huu na amefikia malengo...kwaio tunajua tunachokitafuta sisi bado wachanga katika huu mpira wa kisasa ila Tumeanza mikakati na malengo ya Simba ni ndani ya miaka mitano (5) tuwe tumetwaa kombe la Africa kwaio huu ndio Kwanza mwaka wa pili....Ushauri tukitaka kushindana kikweli kweli ni kuchukua wachezaji kweli kweli kwenda Zambia kuchukua mfungaji Bora wa ligi yao,Kwenda Ghana kuchukua Beki bora,Kwenda Kenya kuchukua Beki bora,Kwenda Uganda kuchukua winga Bora, Yani nikwenda kuchukua Top player ilo ndio wanalolifanya Mazembe...uzuri kwamba Mo dewji ukiacha uwekezaji pia ni shabiki kindaki ndaki Kama sisi matokeo haya nae yamemuumiza Sana Kama sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila matokeo unakimbilia kufukuza coach. Tatizo ni zaidi ya coach. How about training facilities, calibre ya players, arrangement ya misosi etc?

Al Ahly jana wamecheza mpira wa kasi sana. Wachezaji wa Simba hawakuweza kucope kabisa na ile speed. Sasa kama wachezaji kila mtu anakula kwake kiporo cha wali maharagwe then apande bajaji kwenda mazoezini, unategemea nini?😜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…