Magoli 10 ya kufungwa katika mechi mbili,Simba inabaki vipi kama ilivyo?

Magoli 10 ya kufungwa katika mechi mbili,Simba inabaki vipi kama ilivyo?

  • Kocha hajafukuzwa
  • Benchi la Ufundi halijaguswa
  • Wachezaji hawajachunguzwa au kuwajibishwa
  • Viongozi hawajafukuzwa wala kuhojiwa
Timu iliyofungwa na Simba katika mechi ya kwanza ilishamtimua Kocha wake. Sasa inapata matokeo. Imetoa sare na wababe wote wa Simba.

Simba kuweni serious. Hii ni Klabu Bingwa Barani Afrika. Mnatuwakilisha Tanzania. Mkiaibishwa tunaaibishwa sote. Mkifanikiwa na kupata sifa tunapata sifa sote.

Simba haiwezi kubaki kama ilivyo sasa!

Kufukuzwa sio suluhisho kwa sababu zifuatazo

1. Kila jambo linakuwa na lengo. Lengo la Club ya simba kwenye mashindano ya mwaka huu limeshatimia. Ilikuwa ni kufauru kuingia hatua ya makundi.
2. Timu iliyofukuza kocha (J.Soura) lengo lake lilikuwa ni zaidi ya kuingia hatua ya makundi. hivyo hata maandalizi yao yalikuwa ni tofauti na ya Simba.
3. Simba ni "Under dog" kwenye kundi hili. Hivyo hata wakimaliza nafasi ya tatu ni mafanikio makubwa zaidi.
 
Kocha kaenda kutumia style(kufunguka) ile ile tuliofungwa na As vita badala ya kulinda na kushambulia kwa kustukiza.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naweza kubaliana na consultant kwamba aina ya chakula kwa wachezaji wa Simba na ni tatizo,ukilinganisha na Alahly.Wenzetu wanatumia zaidi raw food (Ngano).Hiki chakula humpa mtu nguvu na uwezo wa juu Sana katika kufikiria.Hivyo maamuzi yao uwanjani yanakuwa sahihi sana na kwa haraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli sisi tunaweza kuwa ni underdog kwa al ahaly na as vital ilo tupo pamoja!!!! Mimi hoja yangu ni kwa hawa professional players tunaowalipa millionz of money, na mwisho wa siku they deliver nothing kwenye haya mashindano ndomana Mimi naungana na mtoa mada lazima kitu kifanyike. Thamani ya kikosi cha as vital ni 1.6billion na simba 1.8b meanz kumbe tunauwezo mzuri tu wakukinunua kikosi kizima cha as vital. Why as vital kikosi chao thamani yao kinaenda na thamani ya simba lakini wao wanaperform sisi tu nashindwa. Kuna matatizo mengi sana kwenye idara ya usajili wa simba ndomana wameweza kutuletea garasa kaulibaly na hapa hapa majuzi juzi wametuleta wachezaji kwa ajili ya majaribio badala ya kununua complete players.Inatupasa tuanze upya
Ten percent mkuu ...mbaya sana
 
Mpira ni uwekezaji wenzetu wamewekeza vizuri kwa miaka mingi sisi Simba ndio tunaanza uwekezaji na mkataba aliosaini kocha wa Simba ni kuhakikisha timu inafika kwenye makundi msimu huu na amefikia malengo...kwaio tunajua tunachokitafuta sisi bado wachanga katika huu mpira wa kisasa ila Tumeanza mikakati na malengo ya Simba ni ndani ya miaka mitano (5) tuwe tumetwaa kombe la Africa kwaio huu ndio Kwanza mwaka wa pili....Ushauri tukitaka kushindana kikweli kweli ni kuchukua wachezaji kweli kweli kwenda Zambia kuchukua mfungaji Bora wa ligi yao,Kwenda Ghana kuchukua Beki bora,Kwenda Kenya kuchukua Beki bora,Kwenda Uganda kuchukua winga Bora, Yani nikwenda kuchukua Top player ilo ndio wanalolifanya Mazembe...uzuri kwamba Mo dewji ukiacha uwekezaji pia ni shabiki kindaki ndaki Kama sisi matokeo haya nae yamemuumiza Sana Kama sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ligi mbovu hivi hata uwachukue hao unaowasema msaada wao utakuwa ni mdogo sana!! Kwani kwenye ligi ya ndani watakuwa hawana ushindani ki vile, hivyo wanaona kuwa wamefika, viwango lazima vitashuka tu ngoja wakutane na wanaume wenzaolazima watepete tu
 
Back
Top Bottom