1. Hizi timu mbili Simba na Yanga ni janga la taifa
2. Jana tumeshuhudia vijana wa alliance wakicheza sika safi, kufunga goli likakataliwa, kupata penalt mbili zikakataliwa.
3. Ninawashangaa mashabiki wa mikoani wanashiriki kuzihujumu timu za mikoa yao kisa simba na Yanga zishinde
4. Jambo kama hili huwezi kulikuta kwenye nchi za ulaya eti watu wanashanglia timu pinzani na nyumbani na kuizomea timu ya nyumbani?
5. Hivi nawauliza ninyi wasukuma wa Mwanza na shinyanga kama sio jitihada za stand, mbao na alliance hata hao simba na yanga mnaowachangia michango wakati watoto wenu wapo hoi wangekuja?
6. Kweli ninyi matajiri wa kanda ya ziwa mnasapoti timu ya wazaramo wakati ya za kwenu zimedhoofu?
7. Hivi nguvu mnazotumia kufungua matawi, kushona mabendera makubwa eti tawi na rock city na kuchangisha hela mnawapa hao wajanja wajanja wa dar hizo nguvu mngezipeleka mbao alliance, stand na mwadui kanda ya ziwa sii ingekuwa tishio?
8. Ninyi ndio mnawapokea maadui, mnawapeleka mpaka kwa wataalamu ( nijwa tuliiona inarushwa kutoka jukwa la njano) ili wawashinde vijana wenu?
9. Kumbe suala la kuisha kwa uzalendo hadi timu yetu ya taifa inapocheza na mataifa mengine baadhi ya watu wanawashangilia wageni limeanzia huku.