Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAGOMENI KWA ZITO USIKU
Miaka ya 1970 kulikuwa na mgahawa Magomeni Mapipa si mbali na hoteli ya Butiama ukiitwa Michuzi Mikali.
Mwenye mgahawa huu jina lake lilikuwa Shomvi na alikuwa shabiki mkubwa sana wa Yanga.
Yeye alikuwa anafungua mgahawa wake mchana kwa ajili ya chakula cha mchana.
Wateja wake walikuwa vijana washabiki wa mpira na wachezaji mpira khasa wachezaji wa Simba na Yanga.
Miaka imekwenda na leo hupita mtaa alipokuwa Shomvi.
Hakuna hata dalili kama kulikuw ana mgahawa maarufu hapo.
Leo Magomeni anaewika ni Zito na yeye anafungua mgahawa wake jua likizama.
Magomeni Kwa Zito ni sehemu maarufu.
Kwanza maarufu kwa mwnye jina lake na pili maarufu kwa chips zake na vyakula vingine vinavyopatikana hapo.
Unataka ''Chips Zege,'' Chips Kuku,' ''Chips Mshikaki Kuku au Nyama Ngisi, Samaki,'' nk.
Unataka ''Kisinia...''
Mkate wa Ajemi, chapati, salad...
Wewe ni mlaji wa pilipili za aina aina?
Siku ya Ijumaa mchana kuna ''Speciality of the Day'' - Biriani Kuku na Biriani Nyama, Biriani Samaki.
Hii ni maalum kwa siku ya Ijumaa watu wakitoka msikitini wanapita Kwa Zito kwa ''Take Away'' au kula hapo hapo.
Kwa kawaida utaikuta foleni.
Lakini hutochelewa haraka ''hot pot'' yako itajazwa na wewe utaondoka.
Kwa Zito.
Umaarufu wake ni kuwa yeye mwenyewe ni mtoto wa Magomeni.
Mkazi wa Kariakoo, Kinondoni, Ilala na kwengineko anapiga simu anatoa oda na haraka chakula kinatayarishwa muda haupiti na bodaboda anachukua kupeleka.
Kwa Zito nilipajua kama maarufu siku moja najaribu kumuelekeza dereva wa taxi nyumbani kwangu.
Kwa kiasi cha dakika mbili, tatu hajapajua kwangu na mimi namaliza ''landmark'' na mitaa yote kumfahamisha.
''Mzee uko karibu na Zito?''
''Khasaa.''
''Sasa mzee si ungesema twende kwa Zito?
Siku hizi sipati shida nikitaka kumuelekeza mtu kwangu namwambia, ''Kwa Zito.''
Umaarufu huu wa Kwa Zito ni hayo machopochopo yake.
Kwa Zito kuna Idara Maalum ya Juisi.
Inataka ufike mwenyewe Kwa Zito ushuhudie kwa macho yako.
Haya si ya kuhadithiwa.
Nahitimisha.
Zito mwenyewe ni ''dandy'' yaani mtu anaependa kuvaa.
Iko siku Zito utamkuta ''counter'' katika dariz nyeupe na kofia ya mkono.
Siku nyingine kaweka Panama Hat na shati la kupendeza.
Siku nyingine katia ''msasa'' yaani jeans.
Ili muradi kwangu mimi ni kivutio tosha.
Mimi wala si mteja wa maana nakwenda kwa nadra kuchukua ''Take Away.''
Zito hataki kuniona nimesimamishwa pale hata kwa nusu dakika.
''Haya fanyeni haraka mzee aondoke, mfungieni haraka.''
Lakini Kwa Zito kuwa katika mazingira yale usiku ni burdani tosha.
Utakutana na watu wengi hujawaona muda mrefu wamekuja kula na jamaa zao.