Choganya
Member
- Jun 19, 2024
- 5
- 3
Wakati ambao dunia inabadirika kwa kasi katika siasa, uchumi, afya, elimu na technolojia, jamii yetu inahangaika kupambana ili kuhakikisha kila mtu anaishi maisha bora na maendeleo yanapatikana kwa kila mmoja. Lakini, juhudi hizi zinarudi nyuma kutokana na changamoto kubwa ambazo jamii inapitia. Ikiwemo magonjwa ya akili. Takwimu za shirika la afya ulimwenguni (WHO) za mwaka 2019, zinaonyesha kuwa taklibani watu milioni 970, duniani kote waliishi na magonjwa ya akili. Hiki ni kiashiria cha kwamba matatizo haya ya afya ya akili yapo kwa kiasi kikubwa sana katika jamii.
Kuna aina nyingi za magonjwa ya akili kwa binadamu kama: sonona, msongo wa mawazo, skizofrenia na ugonjwa wa wasiwasi, haya ni baadhi tu. Haya ndiyo magonjwa hatari Zaidi duniani ambayo hayajapewa jicho la ziada na jamii nyingi. Lakini haya magonjwa ya akili ndio magonjwa pekee yanayoweza kusababisha magojwa mengine mengi ya mwili. Kwasababu mtu yeyote asiye na akili timamu hufikiri mawazo machafu na kuona wengine wote ni maadui kwake. Hivyo, hapa ndipo shida nyingi za kisiasa, kiuchumi na kijamii huanzia.
MADHARA YA MAGONJWA YA AKILI KATIKA UTAWALA
Ni dhahili kwamba mtu yeyote mwenye magonjwa haya ya akili hawezi kutimiza majukumu yake kama inavyotakiwa, kwasababu anakosa motisha ya kazi, akili inachoka haraka, anakuwa na hasira kali, anapoteza uwezo wa kushirikiana na wengine na kujiingiza kwenye uraibu wa madawa ya kulevya, ngono na kubeti. Hali hii inapelekea utovu wa nidhamu kazini, uzembe, maamuzi yasiyo sahihi, upotoshaji na ukiukwaji wa haki za binadamu. Kwa mfano, wanawake kunyanyaswa kingono wakati wakitafuta kazi katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi. Kuminywa kwa uhuru na haki za binadamu.
Magonjwa ya akili kwa viongozi wa taasisi za umma na binafsi yanaweza kuonekana kupitia dalili zifuatazo: kunyanyasa wananchi, kufungia baadhi ya vyombo vya habari kwasababu kiongozi mwenye ugonjwa wa akili huwa anahisi hayupo salama kila wakati na kwamba kila anaye sema ukweli kuhusu kiongozi yule ni adui, kuzuia maandamano ya kisiasa kwasababu hawapendi kukosolewa, kudanganya wananchi ili kiongozi apate kura, kuiba mali za umma na kufanya maamuzi yasiyosahihi. Mara zote kiongozi bora hupimwa kupitia maamuzi yake katika kutatua changamoto za jamii yake, kama kiongozi hana huu uwezo maana yake ni bora kiongozi.
Ndoto kubwa ya kila mtu katika jamii ni kuona maendeleo anayoyahitaji yanatokea. Lakini hii ndoto haiwezi kutimia kama walioaminiwa kusimamia shughuli za maendeleo katika jamii wana hangaika na ni wagonjwa wa akili. Ikumbukwe kuwa akili ni injini ya mwili wa binadamu, inashughulikia kila kazi ambayo binadamu anaifanya. Hivyo, bila akili timamu hakuna maendeleo, kwasababu maendeleo yanaletwa tu na wenye akili timamu. Sasa basi, ili tupate maendeleo tunayoyahitaji katika jamii ni lazima tuwekeze katika kuimarisha na kuboresha afya ya akili zetu na viongozi wa umma.
ZIFUATAZO NI NJIA MHIMU ZINAZOWEZA KUTUMIKA ILI KUIMARISHA NA KUBORESHA AFYA YA AKILI KWA VIONGOZI NA JAMII KWA UJUMLA.

- Kuanzisha uchunguzi wa kisaikolojia kwa kila anayeteuliwa au kuchaguliwa kushika nafasi katika utumishi wa umma. Uchunguzi huu ufanyike kuwa lazima kama unavyofanyika uchunguzi wa kisheria kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi na wote wanaoteuliwa. Itasaidia kupata viongozi ambao wana afya timamu ya akili.
- Kuhakikisha kila ofisi ya umma inakuwa na mwanasaikolojia atakaye hakikisha usalama wa afya ya akili za watumishi katika ofisi husika. Kwamfano, ofisi ya rais kuwa na wataalam wa saikolojia ya binadamu, ofisi ya mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mtendaji wa kata na mtaa na ofisi za wabunge. Hii itatusaidia katika kuchukua maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Kwa mfano, mwanasaikolojia anaweza kukuambia wakati gani na ukiwa katika hali gani unapaswa kuchukua maamuzi au haupaswi. Sambamba na hayo, mwanasaikolojia atatoa huduma kama mnasihi kwa viongozi pia anaweza kushuri uanzishwaji wa progamu kama michezo, rikizo na mapumziko ya muda mfupi tukiwa kazini ili kuongeza weledi kazini.
- Kuanzisha huduma za kisaikolojia mashuleni, nyumbani, maeneo ya kazi, nyumba za ibada na katika kila kituo cha afya. Ili kusaidia wananchi kuwa na afya timamu ya akili. Uhalisia ni kwamba kila mtu anayokea kwenye familia ambapo alilelewa na wazazi.
MANUFAA YA SAIKOLOJIA KATIKA UTAWALA
Wanasaikolojia wanaweza kushauli wa kitaalamu kuhusu namna bora ya kuchagua na kuteua viongozi wa umma. Kwa mfano, viongozi wakipendekezwa wanafanyiwa uchunguzi (screening) wa kisaikolojia kabla hawajatangazwa na kupelekwa maeneo maeneo ya kazi, Kwa lengo la kubaini changamoto za akili walizonazo. Baada ya hapo ndipo uteuzi unaweza kuendelea.
Saikolojia itasaidia kupatikana kwa viongozi bora na wazalendo ambao watatimoza majukumu yao bila visasi, uonevu, unyanyasaji na wizi wa mali za umma. Ikumbukwe kuwa mtu yeyote mwenye changamoto ya kisaikolojia hupoteza uwezo wa kutumia akili yake vizuri, kukosa hisia chanya na matendo yake pia hubadirika nakuwa ya hovyo. Hivyo kiongozi asiyesalama kisaikolojia hawezi kulinda utamaduni wetu dhidi ya ushoga na usagaji.

HITIMISHO
Mwisho, napenda kutoa rai kwa yeyote anayehusika kwamba kuimarisha matumizi ya Saikolojia katika utawala itaboresha ufanisi wa juhudi za kuleta maendeleo katika jamii. Saikolojia ni kiungo mhimu Zaidi katika utawala na maendeleo ya jamii, kama taifa tuweke nguvu za kutosha katika kada hii kama ambavyo tunaweka nguvu katika kada zingine kama sharia, afya ya mwili na elimu, ndipo tutaona maendeleo makubwa yakisimamiwa na viongozi wazalendo.
Upvote
4