Magonjwa ya akili: Tukutane humu kama una mtu wa karibu mwenye ugonjwa wa akili

Magonjwa ya akili: Tukutane humu kama una mtu wa karibu mwenye ugonjwa wa akili

Màana ukienda hospitalini utaambiwa ni ugonjwa was akili unasababishwa na msongo wa mawazo, ukienda makanisa ya walokole utaambiwa ni suala la kiroho
Ukienda kwa waganga wanasema umerogwa au umetupiwa jini
 
So hard jamani... Kuna Mjomba wangu akianza kuugua attempt za kutaka kujiua ni nyingi sana...!!

Tatizo akitubiwa akipata nafuu anaenda kushinda kwenye kwenye baa na bucha...Ni mwendo wa pombe sana nyama kiasi...

Nawaonea huruma sana Binamu zangu.
Hiyo ni psychosis
 
Mkuu kama hutojali waweza ni PM namba za huyo daktari aliemsaidia mzee wako au jina la hospitali tafadhali....
Psychiatry hospitali kubwa zote IPO.. unless ukutane na dokta ambaye sio Competent. Mana hata magonjwa yanachanganya dalili mengine yanafanana na magonjwa ya Sukari kushuka 'Hypoglicemia'
 
Ukisema vichaa ujue wengi wana huu ugonjwa ila wametofautiana kiwango kuna wale viwango vya kawaida, ambapo akichanganya na pombe tu mitalo ndio yanageuka makazi na wale ambao at constant temperature and pressure wao zimeluka
Bila kusahau na mkono wa waswahil wameongeza sana idadi ya hawa watu uku mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
Wagonjwa wa akili karibu wote wanaanzaga na matibabu ya spirits au magic. Imani za kulogwa Afrika bado ziko kiwango cha juu mnoo
 
Hivi ugonjwa wa akili ni msongo wa mawazo au mkono wa mtu? Na je tofauti ya hzo mbili ni nini?
Wagonjwa wa akili ni mental disrupt! Binadam tukikutana na mambo magum kwenye maisha tunasafa. Na hli hii inaweza kuacha lonterm effect Kwa mtu. Kipindi mtu kaachwa/kafumania.. mtu kamaliza chuo Hana kazi, kafukuzwa kazi. Kafiwa na mtu anaempenda au kashangazwa tu. Hiv vipindi vinamleta kwenye Hali ya kufikiria muda mref then hafikii suluhu. Yani ni kufikiria tu twenti foo pa Seven. Huko ndiko mfumo wa ubongo unaanza kuleta hitilafu. Kama vile, kuzalisha kemikali za furaha nyingi kupita kiwango au ndogo . Zikiwa nyingi mgonjwa anakua na furah kupita kias na vicheko tu bila sabb za msingi na zikiwa ndogo wanahuzunika Kila wakati...
Lakin pia Kuna ugonjwa mmoja ni bigger than we think! Bila exclusion criteria kila mmoja wetu humu ataonekana anao unaitwa BIPOLAR.
 
Mpaka sasa sijajua sababu ya kitaalamu hasa mpaka kupata hilo tatizo; ila ilichukua mwezi mmoja kupona; kwani niliugua mwaka 2017 mwezi mmoja kabla ya UE nikapelekwa muhimbili nikiwa sijitambui nimefungwa kamba; nikahudumiwa pale kwa mda wa wiki kama mbili hivi na kipindi hicho chote baada ya kufika muhimbili sikuwa najitambua kabisa kwa madawa ya muhimbili...ila nikaja kupata ufahamu baadae kabisa baada ya dada yangu kuleta karatasi iliyoombewa na nabii mmoja anaitwa yaspi ingawa imani yao siielewi kabisa ila ndo nilitafuna nikApata ufahamu kabisa mpaka leo Mimi ni mzima kabisa; dawa nimeacha niña mwaka na siku zake sasa na nipo vizuri maana niliweza fanya mtihani special nikafaulu hiyo na kuchukua gamba langu na sasa napga kazi zangu binafsi vizuri na kuna ofisi fulani ya serikali nimeajiriwa na mwaka nataka Anza kusoma master ili tu kumwaaibisha shetani asiyekuwa hataki nimalize degree; hata watu wa mtaani/ndugu/rafiki wana shangaaa jamaa kaponaje?? Wengine wanafikiri nimeenda kwa waganga ila ni muujiza mkubwa sana kwangu
Kama umepona na karatasi ya tarasimu wewe ulirogwa
 
Habari Wadau,
Wazo tu lilinijia majuzi kuanzisha hii thread. Unajua Waafrika hatuongelei hii issue sana kuhusu Afya ya Akili yaani Mental health issues. Na ikitokea kwenye familia basi tunashikana mashati kuwa ndugu yetu kalogwa, laana, katolewa kafara na suluhisho mara nyingi huwa ni kwenda kwa mganga au kuzunguka makanisa yoooote aombewe.

Chakusikitisha ni kwamba magonjwa ya akili yapo mengi from depression, bi-polar, schizophrenia etc na suluhisho izo mbili nilizotaja hazisaidii!! Suluhisho ni kumuona daktari, apate ufumbuzi na kuanza kunywa dawa pamoja na kuahudhuria therapy, inategemea na diagnosis ya daktari.

Nina mzazi ambaye ni mgonjwa kiakili na hakuna maombezi yoyote yaliyosaidia na yuko na maradhi haya miaka mingi sana. Ilituchukua miaka 10 kuelewa kuwa ni ugonjwa na tunashukuru Mungu kuwa akizingatia dawa anakuwa salama anafanya shughuli zake kama kawaida ila asipozingatia dawa inakuwa hatari sana tunakuwa na hofu juu yake na sisi tunaomzunguka.

Tulivoanza therapy, nikagundua kuwa kuna wagonjwa wengi kama yeye, in a selfish way, nilifarijika kusikia kuwa si mzazi wangu tu mwenye tatizo kama lake, maana magonjwa haya tumezoea kuyasikia kwenye tv kama vile ni ya wazungu tu. Mara nyingi, huwa najisikia vibaya sana anapoumwa, natamani angekuwa tu kama wazazi wengine, aliacha biashara zake kwasababu hakuweza kuitumikia 100%, hatakiwi kuwa na stress aina yoyote, anaweza kusema maneno makali sana asikumbuke, akikumbuka alichofanya analia kwa uchungu sana. Huwa anaomba msamaha kwa vitu alivyofanya au sema hata miaka 10 iliyopita, huwa najisikia vibaya sana japokuwa sisi tumezoea.

Nina uhakika kuna wengine mlioko kwenye situation kama hii, naomba tu share experiences zetu, breathe, exhale, najua ni ngumu sana. Naomba mchukue fursa hii kuongelea juu ya magonjwa ya kiakili, ni tatizo gumu sana kulitamka katika jamii yetu na mara nyingi tunayaficha.

Labda hapa ni sehemu nzuri kuongelea bila kuwa judged sababu ni maradhi yanatokea tu kutegemea na maisha ya mtu aliyokulia,lelewa, pamoja na mlundikano wa mawazo na kadhalika.

You are not alone!

Kama Unamaanisha wendawazimu, wehu, machizi, mapunguani, wasio na akili? kwa "wagonjwa wa akili", elewa kuwa hakuna Mtanzania asiyehusika.
 
Mie ningependa kukusaidia mkuu kwenye proposal yako..lol...

suggestion;

1.Police wawe trained kugundua mtu anayeumwa na kumtoa alipo na kumpeleka hospital/safe place.

2.Hospitali za watu wa magonjwa ya akili ziongezwe Tanzania, nakumbuka zamani ilikuwa ni Mirembe na Muhimbili hospitali, ndio hospitali pekee za watu wenye matatizo ya akili, hizi hazitoshi ,kama watu wanne mmoja ana kichaa,this means watu million moja katika million nne za watu wanaoishi Dareslaam wana magonjwa ya akili,je hospitali za wagonjwa hawa ni ngapi Dareslaam tu peke yake??..hili lifanyiwe kazi na serikali...

3.Anzisha Charity(nilikua na hili wazo likanishinda kiutendaji..lol )..yenye help line,uitangaze kwa bidii..watu wakiona mtu yuko hatarini kwa sababu ya matatizo ya akili,then wanapiga hio number..na kupelekwa safe place(hili tegemea na wasanii pia,watatumia huu mwanya,LOL)

4.Iandikie serikali kuikumbusha ina wajibu kama yalivyo magonjwa mengine kama kisukari kupiga kampeni(awareness) ya matatizo ya akili, watu waje forward kupata msaada wasiende kwa waganga na wengineo…

1.
Madness is not mental ilnes. Do not confuse
 
Usiache...dawa..hali itarudi kama.zamani

Dawa za mngonjwa wa akili anatumia hadi anakufa
Siyo kweli,Tricky yake ni ndogo mnoo..the day utakapo realize utajicheka sometimes.
Magonjwa mengi ya akili ni matokeo ya malezi ambayo mtu umeyapitia since ukiwa mdogo,ama traumas mbalimbali.

Ukikutana na therapist ingawa ni wachache hapa bongo,atakueleleza namna ya kurelease those suppressed Emotions ambazo zinaku control unconsciously.

By six months utakuwa ok kabisa.
 
Psychiatry hospitali kubwa zote IPO.. unless ukutane na dokta ambaye sio Competent. Mana hata magonjwa yanachanganya dalili mengine yanafanana na magonjwa ya Sukari kushuka 'Hypoglicemia'
Mkuu,mwili ukiwa katika tension muda wote unakuwa ready kwa mapambano..hivyo sukari inakuwa released kwa wingi kwa ajili ya mapambano.. maana ubongo unaamuru kuwa kuna hatari. Matokeo yake sukari yote inaisha,ndo maana unakuta huyo mtu ana energy kwa kiwango kidogo mnoo..na ukimpima sukari unakuta ipo chini sana.
 
Hata waumini wa makanisa ya walokole wengi wao ni wagonjwa wa akili.

Wanatakiwa wapate haloperidol
 
Nina shangazi yangu anayo hii hali. Changamoto au chanzo baada ya diagnosis kufanyika ni kwamba miaka ya nyuma alikuwa kwenye kitengo serikalini akawa anapiga sana Pesa mwaka 2000 hapo tu.

Alikuwa kwa siku akirejea na kibunda kidogo basi ni laki saba au tano. Ila mara nyingi anarudi la milioni 3, milioni 2 , milioni 5, alikuwa anapata pesa chafu sana.

Wenzake aliokuwa nao kitengo kimoja miaka hiyo wamejenga na wanamaisha na biashara zao saa hii ukikutana nao utasema ni wastaafu wa uwaziri mkuu au benki ya dunia. Wapo njema sana na wanamaisha.

Shida kwake ni alikuwa na matumizi makubwa yasiyo na future kwake. Kiasi kwamba pesa ikawa inaisha kwa kasi. Kaka yake ambaye ndie mshua alimkazia sana kumwambia ajenge mjengo aachane na upuuzi wa maisha ya kupanga ndipo kwa kujilazimisha akanunua eneo na kujenga kama kumridhisha kaka yake ila hakuwa na dhamira hiyo hata kidogo.

MUNGU wa ajabu sana. Alipomaliza ujenzi muda si mrefu kama miaka miwili mshua akavuta. Na yeye baadae kidogo kama miaka mitatu mambo yakaanza kwenda kombo kazini ikiwamo kusimamishwa kazi.

Bahati nzuri alikuwa na akiba akaiweka kwenye finishing ya nyumba akahamia haraka maana alikuwa bado kapanga na nyumba yake alikuwa anakaa ndugu alimuacha aishi kupalinda na nyingine akafungua duka za bidhaa mbili ili kujilinda.

Mwisho wasiku duka zikafilisika akawa benchi sana pesa ikakata kabisa.

Hiyo hali imeanza kumpata kuanzia miaka ya 2016. So anapitia hali ngumu sana. Alipata total mental break down na baada ya kumpeleka hospital akapata matibabu ya dawa za kumpa usingizi ule wa masaa mengi na akafanyiwa counseling ndipo akaanza kufunguka hizo details.

Kwasasa anatumia hizo dawa za antidepressants ili pale kichwa kinapoanza kwenda speed basi dawa zinazima ubongo na kuuchosha ili asiwaze mambo mengi awaze kulala kichwa kiwe kizito.

Huwa naenda sana kwake kwa wiki at least mara 5 kupiga naye story sana na kumpa mipango ya mjini ile story tu basi at least unamuona anajisikia normal. Na huwa ananipigia simu kuwa amenipikia bata , au kuku au chakula chochote ninachopenda then lazima nitaenda kula hata kama ni saa sita usiku nitapita nile then niondoke.

Kwa ambacho nimegundua ni akili yake haijakubaliana na ukweli kuwa yale maisha mazuri yameshapotea na ile fursa haipo tena kwake, na hakutumia muda ule vizuri kujiboresha na kujiwekeza alikuwa anakula life tu na marafiki au partner matapeli.

Sasa akili bado inamlazimisha kurudi alipokuwa ili arekebishe yale makosa na hapo ndipo msongo wa mawazo unamtokea na kumpelekesha kumpa hali kama ya ukichaa.

I hope baada ya miaka kadhaa atakubaliana na hali na kukaa sawa. MUNGU kama atanisaidia nikiwa vema nataka niongee nae nimtengee kiasi cha pesa aende mbuga za wanyama, halafu atembee mikoa hata mitano mikubwa akae na kutazama mazingira ya tofauti ale vyakula vya huko na kununua bidhaa yaani utalii wa ndani kisha arejee nimtafutie kitu cha kumkeep busy kidogo ili awe na focus kwenye maisha badala ya kuwa na hizi fikra za msongo wa mawazo muda wote.

Namkubali sana shangazi yangu maana ana huruma sana. Na kipindi hicho mimi nilikuwa mdogo sana ila nina uhakika ingekuwa miaka hii na yeye ndio angekuwa njema vile basi kijana ningekula sana maisha na ningekuwa napata sana sapoti yake ila ndio hivyo tena nimekua na kukuta ameshafilisika. So inabidi tu kumsapoti kwa hali yake na mimi hali yangu.
Pole sana shangazi yako ana Mme na watoto?
Watu wengi wanaopitia hyo hali Huwa wanaohitaji mtu wa kuwasikiliza na kupiga story Kwa wingi hawatakiwi kuwa na mawazo
 
Duuh kwani shangazi yako hana familia mkuu yani mume na watoto
 
Uwezekano wa ugonjwa wa akili kukurudia baada ya kuacha dawa ni mkubwa sana...nimewahi kupona kabisa ugonjwa wa akili ila baada ya miamka mitano umenieudia ila niko poa naendelea na dawa
 
Back
Top Bottom