Magonjwa ya akili: Tukutane humu kama una mtu wa karibu mwenye ugonjwa wa akili

Magonjwa ya akili: Tukutane humu kama una mtu wa karibu mwenye ugonjwa wa akili

Habari Wadau,

Wazo tu lilinijia majuzi kuanzisha hii thread. Unajua Waafrika hatuongelei hii issue sana kuhusu Afya ya Akili yaani Mental health issues. Na ikitokea kwenye familia basi tunashikana mashati kuwa ndugu yetu kalogwa, laana, katolewa kafara na suluhisho mara nyingi huwa ni kwenda kwa mganga au kuzunguka makanisa yoooote aombewe.

Chakusikitisha ni kwamba magonjwa ya akili yapo mengi from depression, bi-polar, schizophrenia etc na suluhisho izo mbili nilizotaja hazisaidii! Suluhisho ni kumuona daktari, apate ufumbuzi na kuanza kunywa dawa pamoja na kuahudhuria therapy, inategemea na diagnosis ya daktari.

Nina mzazi ambaye ni mgonjwa kiakili na hakuna maombezi yoyote yaliyosaidia na yuko na maradhi haya miaka mingi sana. Ilituchukua miaka 10 kuelewa kuwa ni ugonjwa na tunashukuru Mungu kuwa akizingatia dawa anakuwa salama anafanya shughuli zake kama kawaida ila asipozingatia dawa inakuwa hatari sana tunakuwa na hofu juu yake na sisi tunaomzunguka.

Tulivoanza therapy, nikagundua kuwa kuna wagonjwa wengi kama yeye, in a selfish way, nilifarijika kusikia kuwa si mzazi wangu tu mwenye tatizo kama lake, maana magonjwa haya tumezoea kuyasikia kwenye tv kama vile ni ya wazungu tu.

Mara nyingi, huwa najisikia vibaya sana anapoumwa, natamani angekuwa tu kama wazazi wengine, aliacha biashara zake kwasababu hakuweza kuitumikia 100%, hatakiwi kuwa na stress aina yoyote, anaweza kusema maneno makali sana asikumbuke, akikumbuka alichofanya analia kwa uchungu sana. Huwa anaomba msamaha kwa vitu alivyofanya au sema hata miaka 10 iliyopita, huwa najisikia vibaya sana japokuwa sisi tumezoea.

Nina uhakika kuna wengine mlioko kwenye situation kama hii, naomba tu share experiences zetu, breathe, exhale, najua ni ngumu sana. Naomba mchukue fursa hii kuongelea juu ya magonjwa ya kiakili, ni tatizo gumu sana kulitamka katika jamii yetu na mara nyingi tunayaficha.

Labda hapa ni sehemu nzuri kuongelea bila kuwa judged sababu ni maradhi yanatokea tu kutegemea na maisha ya mtu aliyokulia, lelewa, pamoja na mlundikano wa mawazo na kadhalika.

You are not alone!
Niliandika hii post nikiwa na machungu sana, nikijua pengine kuna wengi wanapitia ninachopitia. Nafurahi kuwa wengi mmefunguka. Mungu azidi kuwainua na kuwaponya.
 
Kuna hizi hospital za vichaa wagonjwa wanapigwa sana na ni Moja ya mbinu zinazotumika kuwatuliza, wachanga wa hili wanaporudi kwenye sense wanalaumu sana kunahaja ya kuja na solution ya tiba za asili juu ya hili, tena hii liwe ni jambo la kitaifa. Na kuhusu neno la afya ya akili ni propaganda akili haina afya maana akili haipo kichwani ni mawimbi. Maana ulivyo tuna ubongo yaani antenna au dish Sasa akili ikowapiil hapo ndio maana mtu akipata tatizo kama ajali na eneo la ubongo likaathirika basi mawimbi ambayo tunaita akili hupatikana kwa shida.
Ni vyema kama unamtu mwenye changamoto hii ni lazima mumuhimize awe anapata usingizi wakutosha hata kwakutmia dawa na hapa pia ziko dawa za asili zakumps urahisi wakulala.
 
Nazungumzaga hapa kila muda juu ya usingizi na muda mwingi wa kulala. Unajua wagonjwa wemgi wa mood disorders wanasumbuliwa na kukosa usingizi na ashki iliyopita kiwango.. kulala zaidi kuna matokeo chanya juu ya maendeleo yao asee
 
U
Unatumia model ya mwak gani kufanya assessment ya mgonjwa wako?
Mimi sio daktari ila hujui kuwa kuna mood disorders ambazo ni magonjwa ya akili, na magonjwa yote ya akili sio mood disorders, kama umeshindwa kujua hili katika this Internet era basi tena...
 
Back
Top Bottom