Enlightenment
JF-Expert Member
- Apr 19, 2018
- 1,321
- 3,299
Habari wanajukwaa, karibuni tuelimishane juu ya mtindo wa maisha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Utangulizi
Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO), mitindo ya maisha isiyo bora ndio chanzo kikubwa cha kuongezeka kwa magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza duniani ambayo yamekua yakisababisha mamilioni ya vifo vya mapema kila mwaka.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na: Moyo, Shinikizo kubwa la damu, Kiharusi, Kisukari, Saratani, Pumu na Magonjwa sugu ya njia ya hewa.
Maendeleo ya kiuchumi ambayo ni pamoja na kuongezeka kwa kipato, matumuzi ya nyenzo nyingi za kisasa ikiwa ni pamoja na magari, vifaa vya kisasa vya kutendea kazi, komputa na television vimechangia sana kuwafanya watu kuwa na ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ya mwili.
Mtindo huu wa maisha umechangia kwa watu kulimbikiza nishati-lishe mwilini na hivyo kujiweka katika uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
Mtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia:
ULAJI UNAOFAA
Hutokana na kula chakula chenye mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi matano(5) ya vyakula na kupunguza kiasi cha mafuta, chumvi na sukari kinachotumika. Chaula hicho kinatakiwa kiwe cha kutosha kukidhi mahitaji ya mwili.
Ulaji unaofaa unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsi, umri, mzunguko wa maisha (mf. Utoto,ujana, uzee), hali ya kifiziolojia (mf. ujauzito, kunyonyesha), kazi au shughuli na hali ya afya.
Ulaji uanofaa huchangia katika kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza maradhi, yakiwemo magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
Kula mlo kamili mara tatu(3) kwa siku
Hii inakuwezesha kupata virutubishi muhimu vinavyohitajika mwilini. Mlo kamili hutokana na kuchanganya angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula na viliwe kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji ya mwili.
Ni muhimu kuanza na kifungua kinywa asubuhi ili upate nguvu ya kuanza siku na kufanya shughuli kwa ufanisi. Inashauriwa kula vyakula vya aina mbalimbali hata vile vilivyo katika kundi moja la chakula.
Kula matunda na mbogamboga kwa wingi
Vyakula hivi husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini, hivyo kujikinga na maradhi mbalimbali. Vyakula hivi pia huupatia mwili makapi-mlo ambayo humfanya mtu ajisikie kushiba na kumfanya ale chakula kwa kiasi kidogo hivyo kupunguza uwezekano wa kuwa na uzito uliozidi au unene.
Kula vyakula vyenye makapi-mlo kwa wingi
Makapi-mlo husaidia mfumo wa chakula kufanya kazi kwa ufanisi. Pia husaidia mtu kupata haja kubwa kwa urahisi na huchangia katika kupunguza uwezekano wa kuongezeka uzito, kupata baadhi ya saratani, magonjwa ya moyo na kisukari.
Ongeza kiasi cha makapi-mlo kwa kula matunda na mbogamboga kwa wingi, nafaka zisizo kobolewa kama unga wa dona na ngano na vyakula vya jamii ya kunde.
Epuka vyakula vyenye mafuta mengi
Mafuta hutoa nishati lishe kwa wingi hivyo husababisha ongezeko la uzito kwa haraka. Ulaji wa mafuta mengi hususani yenye asili ya wanyama huchangia katika kuongeza kiasi cha mafuta katika damu hususani lehemu na hivyo kuongeza uwezekano wa kupata maradhi sugu kama magonjwa ya moyo, kisukari na shinikizo kubwa la damu.
Epuka kutumia sukari nyingi
Sukari huongeza nishati-lishe bila virutubishi vingine mwilini. Punguza kiasi cha sukari kwa kuepuka vinywaji vyenye sukari nyingi na kunywa juisi halisi ya matunda, togwa au vinywaji vya viungo. Epuka vyakula vyenye sukari nyingi kama vile jamu, biskuti, keki, chokoleti, kashata na pipi.
Epuka vyakula vyenye chumvi nyingi
Ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi huongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu na baadhi ya saratani. Matumizi ya chumvi huweza kupunguzwa kwa kutumia chumvi kidogo wakati wa kupika, kuepuka vyakula vyenye chumvi nyingi au vilivyosindikwa kwa chumvi. EPuka tabia ya kuongeza chumvi kwenye chakula wakati wa kula (mezani).
Kunywa maji safi, salama na ya kutosha
Inashauriwa kunywa maji angalau glasi nane(lita moja na nusu) kwa siku. Maji ni muhimu sana mwilini kwani:
Tafiti zimeonyesha, kuna uhusiano kati ya ulishaji wa mtoto na uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza utotoni, katika ujana na hata anapokua mtu mzima. Unyonyeshaji wa maziwa ya mama huwakinga watoto dhidi ya kuwa na uzito uliozidi na unene uliokithiri hapo baadaye. Watoto walionyonyeshwa maziwa ya mama kwa muda mfupi(chini ya miezi 6) na wale waliopewa maziwa mbadala (ya kopo au wanyama) wako katika hatari zaidi ya kupata baadhi ya magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo kubwa la damu na saratani utotoni, katika ujana na wanapokua watu wazima.
Ulishaji mtoto vyakula vya nyongeza vyenye nishati-lishe kwa wingi unahusishwa na mtoto kuwa na hatari ya kupata saratani na shinikizo kubwa la damu ukubwani
Unene wakati wa utoto humweka mtoto katika hatari ya kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama kisukari na ugonjwa wa moyo.
Tutaendelea tena....

- ulaji unaofaa
- kufanya mazoezi ya mwili,
- kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku,
- kuepuka matumizi ya pombe na
- kuepuka msongo wa mawazo.

- hurekebisha joto la mwili,
- husaidia uyeyushaji wa chakula,
- husafirisha virutubishi kwenda kwenye seli na kuondoa mabaki au uchafu mwilini kwa njia ya jasho, mkojo nk.
- Husaidia pia kulainisha maungio ya mwili.