Magonjwa yasiyoambukiza yashika kasi Tanzania

Magonjwa yasiyoambukiza yashika kasi Tanzania

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Asilimia 50 ya wagonjwa wanaotibiwa Muhimbili, kitengo cha Fiziotherapia, wanaumwa magonjwa yasiyoambukiza. Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari Wazoeza Viungo Tanzania, Dk. Denis Mbezi, wakati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Kongamano la Wataalamu wa Fiziotherapia katika nchi za Afrika, litakalofanyika jijini Arusha, Oktoba 14.

Dk. Mbezi alisema magonjwa hayo kwa sasa yameshika kasi na yanapoteza uhai wa watu wengi kutokana na kushindwa kutambua njia za kuzuia magonjwa hayo yasiwatokee. Aliyataja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari, kuwa na mafuta mengi mwilini, kuongezeka uzito na kuna kundi kubwa la wagonjwa wa kiharusi, uchakavu wa viungo na watoto wenye mtindio wa ubongo. Kiharusi kinasababishwa na shinikizo la juu la damu, usukari, chakula chenye mafuta mengi au uvutaji wa sigara.

Alisema watu wengi wameshindwa kupata elimu ya kuzuia magonjwa hayo yanayosababishwa na maisha yasiyozingatia misingi ya afya bora huku akitolea mfano shinikizo la damu linalosababishwa na kutofanya mazoezi. Kutokana na hali hiyo chama hicho kimeandaa kliniki ya wazi itakayotoa huduma bure kama ishara ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 14 hadi 18 Arusha.

Dk. Mbezi ambaye pia anahusika na kitengo cha Fizioterapia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alisema kazi za chama hicho ni pamoja na matibabu hasa kwenye magonjwa yasiyoambukiza, kinga na kutoa elimu jinsi ya kuepuka magonjwa hayo.

Chanzo: Magonjwa yasiyoambukiza yaongezeka
 
Nilikuwa na njaa mbayaa! Nikashindilia chips yai mishkaki 5! Kusoma hi mada kidogo nikajitapishe!!!!!!!!!!! Mafuta mengi ni balaaa! Kuanzia kesho naanza kula choma na chemsha! Daaah!

Tuwe tunakumbushana bana!
 
Kama shinikizo la damu wanaita silent killer...

maana unaweza kuwa na hilo tatizo kwa miaka na usijue...ndio unasikia kafa ghafla alikuwa haumwi wala nini...

Kumbe alikuwa mgonjwa kuliko mwenye HIV.

Hili ni tatizo kubwa sana; ila mtu ni ngumu kuelewa mpaka likukute mwenyewe au ndugu wa karibu
 
Nilikuwa na njaa mbayaa! Nikashindilia chips yai mishkaki 5! Kusoma hi mada kidogo nikajitapishe!!!!!!!!!!! Mafuta mengi ni balaaa! Kuanzia kesho naanza kula choma na chemsha! Daaah! Tuwe tunakumbushana bana!

Baada ya hapo ulishushia na nini?

4c1d6398057911e3963b22000a1f9c8c_7.jpg
 
Nilikuwa na njaa mbayaa! Nikashindilia chips yai mishkaki 5! Kusoma hi mada kidogo nikajitapishe!!!!!!!!!!! Mafuta mengi ni balaaa! Kuanzia kesho naanza kula choma na chemsha! Daaah!

Tuwe tunakumbushana bana!
Mishikaki 5? Duh kweli hakuna kulemba! imeisha yote?
 
Sisi Watanzania wengi tuishio mijini ni wavivu sana wa mazoezi na mfumo huu wa maisha unagharimu na utaendelea gharimu wengi...

Wengine zoezi pekee alifanyalo ni kugombea daladala asubuhi au jioni, akifika kituo aendacho huishia kupanda bodaboda...hapo hajafika nyumbani na kukutana na hii milo hatarishi kwa afya...
 
Asilimia 50 ya wagonjwa wanaotibiwa Muhimbili, kitengo cha Fiziotherapia, wanaumwa magonjwa yasiyoambukiza. Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari Wazoeza Viungo Tanzania, Dk. Denis Mbezi, wakati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Kongamano la Wataalamu wa Fiziotherapia katika nchi za Afrika, litakalofanyika jijini Arusha, Oktoba 14.

Dk. Mbezi alisema magonjwa hayo kwa sasa yameshika kasi na yanapoteza uhai wa watu wengi kutokana na kushindwa kutambua njia za kuzuia magonjwa hayo yasiwatokee. Aliyataja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari, kuwa na mafuta mengi mwilini, kuongezeka uzito na kuna kundi kubwa la wagonjwa wa kiharusi, uchakavu wa viungo na watoto wenye mtindio wa ubongo. Kiharusi kinasababishwa na na shinikizo la juu la damu, usukari, chakula chenye mafuta mengi au uvutaji wa sigara.

Alisema watu wengi wameshindwa kupata elimu ya kuzuia magonjwa hayo yanayosababishwa na maisha yasiyozingatia misingi ya afya bora huku akitolea mfano shinikizo la damu linalosababishwa na kutofanya mazoezi. Kutokana na hali hiyo chama hicho kimeandaa kliniki ya wazi itakayotoa huduma bure kama ishara ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 14 hadi 18 Arusha.

Dk. Mbezi ambaye pia anahusika na kitengo cha Fizioterapia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alisema kazi za chama hicho ni pamoja na matibabu hasa kwenye magonjwa yasiyoambukiza, kinga na kutoa elimu jinsi ya kuepuka magonjwa hayo.

Chanzo: Magonjwa yasiyoambukiza yaongezeka
Du!tumekwisha so akuna dalili za ugonjwa??
 
Kama shinikizo la damu wanaita silent killer...

maana unaweza kuwa na hilo tatizo kwa miaka na usijue...ndio unasikia kafa ghafla alikuwa haumwi wala nini...

Kumbe alikuwa mgonjwa kuliko mwenye HIV.

Hili ni tatizo kubwa sana; ila mtu ni ngumu kuelewa mpaka likukute mwenyewe au ndugu wa karibu

Hali zinazosababisha shinikizo la damu

  • Hali ya unene wa kupindukia
  • Ulaji mwingi wa chumvi au sodium
  • Hali ya uvivu
  • Uvutaji wa sigara
  • Mazingira ya mifadhaiko ya hali ya juu
  • Ulaji wa vyakula visivyo vya afya
  • Historia ya kifamilia ya kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu
Jinsi Ya Kuzuia Ugonjwa Wa Shinikizo La Damu

  • Acha uvutaji wa sigara
  • Pungua uzito kama ni mnene
  • Ongeza mazoezi ya viungo ili kuimarisha hali ya afya ya moyo
  • Punguza sodium iwe chini ya gramu 2.4 za sodium au chini ya gram 6 za chumvi kwa siku (chumvi kijiko
kidogo kimoja na robo)

  • Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta na kolestero
  • Punguza unywaji wa pombe ( tumia kinywaji kimoja au viwili kwa siku)
  • Ulaji wa kiwango kinachotakiwa cha kalsiumu, potasiamu, magnesiamu,
  • Dhibiti hali ya mifadhaiko na majonzi
Dalili za Shinikizo la Damu

  • Kuumwa kwa kichwa
  • Uchovu
  • Matatizo ya macho
  • Hali ya kichefuchefu na kutapika
  • Hali ya woga
  • Hali ya kuchaganyikiwa
  • Kupauka kwa ngozi au kuongezeka wekundu wa ngozi
Muhimu: Mara nyingi watu wenye ugonjwa wa shinikizo la damu hawana dalili yoyote.

Tiba ya Shinikizo la Damu

  • Ulaji wa vyakula vyenye afya, punguza vyakula vyenye chumvi, mafuta na kolestero
  • Uthibiti wa mifadhaiko, kupunguza mifadhaiko au kutafuta njia ya kudhibiti mifadhaiko
  • Ufanyaji wa Mazoezi; dakika thelathini kila siku za shughuli za mazoezi ya viungo zinashauriwa
  • Kupungua kwa uzito, kama inwezekana
  • Daktari wako anaweza kukuandikia dawa kwa ajili ya shinikizo la damu

http://www.rochestergeneral.org/~/media/Images/Imported/gedownload/hypertension swahili.pdf
 
watu wanaona unene dili full kujishindilia mafuta... ukiwa mwembamba unaambiwa 'siku hizi hauli au'.. kitambi na matumbo ndio dalili zao za kupima afya bora... wanavipataje sasa bila kujibweteka na kujishindilia! ngoja nianze tena mazoezi na mie nisije muona huyo dokta mbezi bure.
 
Sisi Watanzania wengi tuishio mijini ni wavivu sana wa mazoezi na mfumo huu wa maisha unagharimu na utaendelea gharimu wengi...

Wengine zoezi pekee alifanyalo ni kugombea daladala asubuhi au jioni, akifika kituo aendacho huishia kupanda bodaboda...hapo hajafika nyumbani na kukutana na hii milo hatarishi kwa afya...

Mtikikasi ya mijini imetawala afya zetu. It needs commitment and motivation.
 
Du!tumekwisha so akuna dalili za ugonjwa??

Zinaweza kuwepo kama, kuumwa kwa kichwa, uchovu, matatizo ya macho, kuwa na hali ya kichefuchefu na kutapika, kuwa na hali ya woga, kuwa hali ya kuchaganyikiwa na kupauka kwa ngozi au kuongezeka wekundu wa ngozi, lakini mara nyingi kunaweza kusiwe na hizo dalili au zinaweza kuwepo lakini mgonjwa au watu waliye karibu nae wasijue.

watu wanaona unene dili full kujishindilia mafuta... ukiwa mwembamba unaambiwa 'siku hizi hauli au'.. kitambi na matumbo ndio dalili zao za kupima afya bora... wanavipataje sasa bila kujibweteka na kujishindilia! ngoja nianze tena mazoezi na mie nisije muona huyo dokta mbezi bure.

Lakini pia kuna ambao ni wanene genetically. There is nothing they can do about hata kama wapipunguza kula au kufanya mazoezi kila mara.

Unene mbaya ni ule unaosababishwa na kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora. Hata hivyo, nasikia baadhi yenu mnatumia kigezo cha kitambi kujua kama mwanaume yuko fit kwenye wallet.

Siku hizi kuna mpaka kusalimiana kwa vitambi.

571578114.JPG
 
Asante Mungu kwa afya yangu.

Kwetu mimi tu ndio hadi mwaka jana nilikua nakula nyama,wengine wote ni vegetarian toka
utotoni. Nimesha adopt lifestyle yao na ni nzuri sana.

Mazoezi,inahitaji moyo kutoacha na maisha yetu haya ya kuiga kila kitu plus "ubize"
 
Na mimi nakuunga mkono...mazoezi si lele mama...na wengi wanafanya na kuacha...

Solution ya kudumu na ya kuaminika ni kula chakula bora....baaasi.

Na wanasema diet inapunguza na kuthibiti unene effectively kuliko mazoezi...ndio maana hawa maveterani wa mpira wa miguu wana vitambi ...pamoja na kuendelea kuwa wana mazoezi...nyama choma, chips plus mazoezi, sawa na kazi bure.

Kila unachokula jiulize kina faida na hasara gani mwilini...usidanganyike na utamu wa ulimini.

Asante Mungu kwa afya yangu.

Kwetu mimi tu ndio hadi mwaka jana nilikua nakula nyama,wengine wote ni vegetarian toka
utotoni. Nimesha adopt lifestyle yao na ni nzuri sana.

Mazoezi,inahitaji moyo kutoacha na maisha yetu haya ya kuiga kila kitu plus "ubize"
 
Watu wanafakamia vyakula vya hovyo hovyo, kuvuta sigara, kunywa kupindukia wakati mwingine kwa kutaka sifa kwamba yeye anaweza kufakamia bia nyingi, au glass nyingi za whisky/nyagi au kutaka kuonekana naye wa MUJINI kumbe anaharakisha safari yake ya umauti!!! Watu wa karibu wakimwambia analeta za kuleta, "Wote tutakufa". Kula vyakula ambavyo havidhuru afya yako ni muhimu sana lakini bahati mbaya wengine wametia pamba masikioni.

watu wanaona unene dili full kujishindilia mafuta... ukiwa mwembamba unaambiwa 'siku hizi hauli au'.. kitambi na matumbo ndio dalili zao za kupima afya bora... wanavipataje sasa bila kujibweteka na kujishindilia! ngoja nianze tena mazoezi na mie nisije muona huyo dokta mbezi bure.
 
Nimejitahidi sana yani kaah..nina mwezi wa nne sijala chips na mwezi wa tatu sijanywa soda juice tu..kisukari na presha ni noma
 
Hakuna kitu kigeni, tunashtuka kwasababu hatukujua kuwa tunaishi na matatizo.

1. Maradhi yasiyoambukiza kama kiharusi na ugonjwa wa moyo yamekuwepo na yapo vijijini.
Tofauti na zamani tukiita kapigwa kibao na jini mdomo ukaenda upande siku hizi tunajua ni kiharusi au stroke.
Tofauti na vijijini na zamani katupiwa mnyama ghafla kafariki siku hizi tunajua ni sukari au presha.

2. Kuongezeka kada ya kati kimaisha
Kuna ongezeko kubwa la kada ya kati kimaisha (middle class kwa mtazamo na vigezo vya Tanzania).
Kada hii huishi kwa chips mayai, kuku wa kukaangaaa, bia na kitimoto. Inakula bila mpangilio na bila kuchagua.
Ndiyo inayoshangilia ujio wa KFC na McDonald.

3. Kuongezeka huduma za afya na weledi
Kada ya kati ni nyepesi kutafuta huduma za afya kwasababu kuna uwezo huo ima kupitia bima za mashirika au wao wenyewe kwa kuelewa kuwa maradhi yanasababu na si uchawi. Ni kwa msingi huo hata Physiotherapist ametoa takwimu kulingana na wateja.

Ukienda vijijini watu wana maradhi ya kisukari, Moyo , presha na kiharusi kwabahati mbaya hawajulikani kwasababu ya kukosa access kwa medical services.

Ufafanuzi
Mgandamizo wa damu(Highblood pressure) unaweza kusababishwa na vitu vingi sana.
Pressure ni dalili ya tatizo si ugonjwa. Inaweza kutokana na figo, Moyo au kitu kingine.
Mara nyingi pressure hutoa kiharusi kwasababu ya uharibifu katika mifumo (ubongo).
Lakini si kila stroke inatokana na pressure.

Sigara ni risk factor hasa kwa wagonjwa wa moyo ambayo yana mahusiano na pressure.
Watu wanasahau kuwa mafuta yanayotokana na wanyama yana lehemu nyingi kuliko ya mimea.
Jiulize kama huvuti sigara vipi minyama ya kuc
homa unayofakamia !

Nini cha kufanya
1. Kuchunguza afya kila mara kabla tatizo halijawa kubwa na kuchukua tahadhari
2. Kubadili maisha na kuacha uvivu wa kupanda magari kila dakika n.k.

Upo utafiti imetolewa wiki kuonyesha kuwa mtu anayetembea umbali wa kituo cha mbasi kama mita 300-500 anafaidika sana kuliko mtu anyeshinda gym.

3. Kula vyakula vyenye ubora hasa vya asili na si vya kifahari kama fast food. Inawezekana Tanzania.

4. Kuanza kuwafundisha watoto madhara ya kula hovyo na hasa vyakula vinavyoonekana kuwavutia ambavyo si bora na vina madhara.

Vitambi na Nyungu visionekane kama 'social status' ni mtatizo yaliyo wazi. Wahurumieni wenye navyo.
Hii kauli ya mwisho inanichonganisha na jamii, ngumu ku-balance ! Nasonywa sana, nisameheni ndio ukweli huo.

EMT, lete na elimu ya Kisukari, nadhani hili ndio gonjwa tata kuliko yote hayo mnayosema, mtu mwenye High blood Pressure anapiga kazi kwa wife wake kama kawa lakini mwenye Kisukari, mh, full fedheha binafsi nadhani hili gonjwa ndio baya kuliko hata ukimwi, mwenye uelewa zaidi ya namna ya kujikinga please, hebu tupeni nyuzi.
 
....kwa upande mwingine wengi tunakula kinachowezekana sio tulichopanga mf. wanga kwa wingi na kama ni balance diet mpaka tupate ofa!
 
Back
Top Bottom