Magonjwa yasiyoambukiza yashika kasi Tanzania

Magonjwa yasiyoambukiza yashika kasi Tanzania

EMT, lete na elimu ya Kisukari, nadhani hili ndio gonjwa tata kuliko yote hayo mnayosema, mtu mwenye High blood Pressure anapiga kazi kwa wife wake kama kawa lakini mwenye Kisukari, mh, full fedheha binafsi nadhani hili gonjwa ndio baya kuliko hata ukimwi, mwenye uelewa zaidi ya namna ya kujikinga please, hebu tupeni nyuzi.

Mkuu, umenifanya nikumbuke post yangu moja ya zamani kidogo, jaribu kuipitia kwa kubofya hapa. Mambo mengi sana yameshaandikwa humu jf, pekua tu jukwaa la madaktari.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
dawa ya shinikizo la damu ni MAZOEZI vijana tufanye mazoezi,pili tuepuke kula chips na tuzingatie kunywa maji ya kutosha pungufu kwa siku angalau lita 2,sasa hasa wadada wao ni soda tu kumbe wanajaza chemical mwilini
 
Kwetu mimi tu ndio hadi mwaka jana nilikua nakula nyama,wengine wote ni vegetarian toka
utotoni. Nimesha adopt lifestyle yao na ni nzuri sana.

Generally, sidhani kama kula nyama kuna madhara. Kwanza nyama ina virutubisho mwilini kama protini, vitamini na madini. Nadhani tatizo lipo kwenye aina ya nyama unayokula, jinsi nyama hiyo inavyotayarishwa kwa ajili ya kula, unakula kwa kiasia gani. Kuna hii makala ya Esbon Kgya labda inaweza kutoa mwangaza juu kiini cha nyama kuwa na madhara.

Makala imenifanya nielewa kwa nini wazungu wakioaka au kupika nyama ya ng'ombe hawaoki/pika mpaka ikaiva kabisa. Wakikata katikati utaona bado nyama ni mbichi kabisa lakini wanakula hivyo hiyo.

===================================================

Ulaji nyama una madhara makubwa kwa binadamu

Nyama kwa kawaida ni aina mojawapo ya chakula kitamu sana kwa binadamu, tukila inatupatia virutubisho vingi vikihusisha protini, vitamini na madini. Lakini kula nyama yoyote siyo tatizo wala shida kwa binadamu, tatizo ni jinsi gani nyama hiyo inavyotayarishwa katika kupikwa, kuchomwa na kuokwa ili mpaka binadamu apate kuila. Tunapokula nyama huwa tunakula seli za misuli, na seli hizi za misuli zinapokuwa nyingi na zimejirundika sehemu moja kwa wingi ndivyo sehemu ya nyama hiyo inavyokuwa ngumu sana.

Kitendo cha kuipika nyama ili ipate radha na tuweze kuila, kinaibadilisha nyama hiyo kwa seli zake kuwa ngumu. Mabadiliko hayo makubwa yanayotokea kwenye virutubisho vya protini, kuondosha majimaji na damu na hivyo seli za nyama kushikamana. Nyama inapochemshwa kwenye jotoridi la kati ya 600 C na 650 C, majimaji hutoka, protini hubadilika, na seli zinajikunyata na kujikunja na kuwa ngumu tofauti na nyama inapokuwa bado ni mbichi.

Kuchemsha nyama kwa joto kali kunafanya mabadiliko kwenye nyama hasa ya kemikali aina ya amino. Virutubisho vya protini ambavyo huchanganyika na kemikali ya kretani ambayo inakuwa kwenye seli za misuli ya nyama na yenyewe hutengeneza kemikali nyingi aina za amino. Kemikali hizi hutengenezwa kwa kiasi zikilinganishwa na uwiano wake kwa kila gramu moja ya nyama. Matokeo ya utafiti wa maabara na majaribio ya kisayansi kwa wanyama yameonyesha kuwa kemikali hizi za amino zitokanazo na nyama ni vianzilishi vikuu vya ugonjwa wa saratani kwa binadamu.

Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani- International Agency for Research on Cancer, limethibitisha kuwa kemikali hizo za amino ni chanzo cha kusababisha ugonjwa wa saratani kwa walaji wakuu wa nyama. Utafiti huo umezidi kusisitiza na kuonyesha kuwa walaji wa nyama wa kila mara wanajiweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya matiti na figo. Utafiti mwingine uliofanyika mwaka jana, na Chuo Kikuu cha Harvard cha nchini Marekani, ulibainisha ya kwamba walaji wakubwa wa nyama ya ng’ombe, kondoo, mbuzi, na nguruwe, wako katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa saratani ya matiti hasa wanawake.

Watafiti wanayo maelezo mengi ya kwa nini nyama imekuwa ni chanzo cha kusababisha ugonjwa wa saratani, Lakini wanasisitiza kuwa kemikali za amino zinazopatikana kwenye nyama ndicho chanzo kikuu cha kusababisha ugonjwa huo.Katika maelezo yao wanafafanua kwamba aina yoyote ya virutubisho vya protini, vikichomwa au kuchemshwa, vinazalisha kemikali aina za amino, lakini kiwango cha kemikali ya sumu katika mayai na maharage ya soya ni kidogo sana ikilinganishwa na kiwango kinachopatikana kwenye nyama inapochomwa au kuchemshwa.

Kiwango cha joto kinachotumika katika kutayarisha nyama ili ipate kuliwa, ndicho hasa chanzo kikuu cha utengenezwaji wa kemikali za amino kwenye nyama hiyo. Hivyo kuoka, kukaanga na kuchoma nyama, ni tatizo linalozalisha kemikali kwa vile huhusisha matumizi ya joto kali. Kemikali za amino huenea kwenye milimita chache za mzunguko wote wa kipande cha nyama kufuatana na hali ya nyama hiyo ilivyochomwa, kukaangwa au kuokwa.

Nyama ya kuchoma ndiyo yenye madhara makubwa zaidi, kutokana na vile nyama hiyo inapochomwa kufukizwa na moshi (polycyclic aromatic hydrocarbons), moshi wenye kemikali zenye vichocheo vya kusababisha ugonjwa wa saratani. Hizi kemikali zinatokana na moshi wa mkaa na wa mafuta yanayochuruzika kutoka kwenye nyama inayochomwa.

Muda unaotumiwa katika kutayarisha nyama nao unachangia katika kuzalisha kemikali za kusababisha saratani kutoka kwenye nyama. Majaribio yaliyofanywa na maabara kuu ya Lawrence Livermore National Labaratory ya nchini Marekani, yalionyesha kuwa nyama iliyokaangwa kwa muda wa dakika 10 kwenye mafuta ya jotoridi 2300C, ilikuwa na kiasi kingi cha kemikali mara mbili zaidi ya nyama ya aina ile iliyokaangwa kwa jotoridi lilile lakini kwa muda mfupi wa dakika 4.

Hivyo nyama ya kuku na samaki inayookwa kwa muda mfupi na kuiva, ina madhara kidogo sana kwa afya ya binadamu, kuliko ile ya kondoo nguruwe na ng’ombe inayotumia muda zaidi kuokwa wakati wa kutayarishwa. Na nyama inayookwa kwenye jiko la kuoka ina madhara zaidi ya ile inayochomwa na ya kukaangwa. Hii imethibitishwa na watafiti kwa kukuta kiasi cha kemikali za madhara kwenye rojo inayochuruzika kutoka kwenye nyama iliyookwa.

Wanasayansi pia wanashauri matumizi ya viungo vya kulainisha nyama kabla ya kutayarishwa kwa kupikwa, kuchomwa na kuokwa. Baadhi ya viungo vinavyopendekezwa vina uwezo mkubwa wa kupunguza kemikali kwenye nyama inapotayarishwa. Kiungo aina ya vitunguu swaumu, vimethibitishwa na wanasayansi kupunguza sana madhara ya kemikali za sumu kwenye nyama inapotayarishwa. Pia matumuzi ya mafuta ya zeituni kwenye vyakula na kwenye kutayarisha nyama kunapunguza sana hatari ya kupatwa na saratani ya utumbo mkubwa inayotokana na kula nyama ya kukaanga.

Nchini Marekani, tishio la kemikali zitokanazo na ulaji wa nyama kuwa ni chanzo cha ugonjwa wa saratani, lilifahamika miaka 13 iliyopita. Utafiti uliofanyika ulionyesha kuwa wanawake waliokuwa wanapendelea kula hambaga, nyama choma ya ng’ombe na nguruwe, vilivyotayarishwa kwa dakika nyingi, walikabiliwa na hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa saratani ya matiti kwa mara nne zaidi ya wanawake wale ambao hawakutumia vyakula hivyo au walivitumia kwa uchache.

Utafiti mwingine wa mwaka 2003, ulionyesha ya kwamba madhara ya ugonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa, yaliongezeka maradufu kwa walaji wa nyama choma ya ng’ombe, iliyochomwa kwa dakika nyingi nchini Marekani. Baada ya tatizo hilo kuelezwa na kuifahamisha jamii, National Cancer Institute kwa sasa imetoa ripoti na kueleza kuwa nyama choma ni chanzo cha ugonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa kwa asilimia 20. Wametahadharisha kuwa ugonjwa huo ni kwa walaji wakuu wa nyama choma inayochomwa kwa muda mrefu, kwa wale ambao kwa nadra wanakula kababu, hambaga na nyama choma, hawa hawana nafasi ya kupatwa na madhara.

Pale ambapo viungo vya kulainisha nyama kama haviwezi kupatikana kwa urahisi, na vikatumika kupunguza kemikali za amino, ushauri ni kutumia njia zinazoshauriwa na National Cancer Institute kama wanavyoelekeza. Inaelekezwa kupika nyama kwa jotoridi kidogo kwa muda mfupi. Kukatakata nyama ya kupika katika vipande vidogo vidogo ambavyo vinaiva haraka kwa kutumia moto mdogo ambao siyo mkali sana. Kuchagua nyama ya kuchoma ambayo haina mafuta, nyama ambayo ikichomwa haitatoa mafuta ya kudondokea kwenye mkaa na kuungua na hivyo kuifukiza nyama inayochomwa kwa moshi wenye kemikali zenye madhara ya kusababisha saratani.

Kupika nyama kwanza kwenye jiko la Microwave kwa muda wa dakika mbili, kitendo ambacho kinapunguza kwa wingi kemikali za amino kwa asilimia 90. Muda wa kuichemsha nyama hiyo usizidi dakika mbili, na hivyo kusababisha kuikausha nyama. Kupasha nyama joto kabla haijapikwa, nyama ifungwe vizuri na kuwekwa kwenye maji moto ambamo itakaa kwa muda wa dakika 30 hadi 60. Nyama ikiondolewa kwenye maji moto, mara moja ipikwe maana ni kawaida ya vimelea na bakteria kuzaliana haraka kwenye nyama yenye joto.

Kugeuzageuza nyama mara kwa mara wakati wa kuchoma, kunasaidia kupunguza upande mmoja wa kipande cha nyama kuchomwa na moto na kuungua, wakati upande mwingine wa pili nyama bado ni mbichi. Nyama huiva haraka kwa uwiano sawa na hivyo kutoruhusu kuzalishwa kwa kemikali za sumu.

Chanzo: Ulaji nyama una madhara makubwa kwa binadamu
 
Mazoezi,inahitaji moyo kutoacha na maisha yetu haya ya kuiga kila kitu plus "ubize"

Ubize wapi. Wengi utatukuta baa kuanzia ijumaa jioni hadi jumapili usiku tukipiga kilaji na nyama choma kwa kwenda mbele.

Nafikiri wengi wetu tumezoa kuishi kama tunavyoishi kwa sababu hakuna motivation hasa ya kitaifa katika kufanya mazoezi.

Hatuambiwi madhara ya kutofanya mazoezi ya mara kwa mara. Kwa watu wa mijini hasa maofini hili ni tatizo kwa sababu cardiovascular activities ni chache sana.

Kwa hiyo, ukikuta mtu ambaye anafanya mazoezi kweli anajituma.
 
Na mimi nakuunga mkono...mazoezi si lele mama...na wengi wanafanya na kuacha...

Solution ya kudumu na ya kuaminika ni kula chakula bora....baaasi.

Na wanasema diet inapunguza na kuthibiti unene effectively kuliko mazoezi...ndio maana hawa maveterani wa mpira wa miguu wana vitambi ...pamoja na kuendelea kuwa wana mazoezi...nyama choma, chips plus mazoezi, sawa na kazi bure.

Kila unachokula jiulize kina faida na hasara gani mwilini...usidanganyike na utamu wa ulimini.

Nadhani diet na mazoezi vyote ni muhimu kwa binadamu whether ni mnene au mwembamba. Naelewa wapo baadhi ya watu ambao kwa sababu siyo wanene wanadhani hawana haja ya kufanya mazoezi. Wanadhani mazoezi ni kwa ajili ya watu wanaotakiwa kupunguza unene. Lakini mtu huyo mwembamba ukipanda nae ngazi ghorofa mbili tuu, jinsi atakavyohema.

Hata wale ambao wana metabolism ambayo ni active na hivyo kuweza kuwa wembamba hata wakila mazagazaga bado wanahitaji kufanya mazoezi mara kwa mara. Vingenevyo, wataishia kuwa na kitu kinachoitwa "fat fit". Maana yake ni kuwa na kiwangi cha juu cha heart-clogging cholesterol.

"Many people, especially slim people believe that they only benefit that can be achieved from exercising is weight-loss. This is not the case. ....slim people need to exercise as much as others in order to stay healthy and keep LDL cholesterol in check. ....for some people a low fat diet can help keep their cholesterol level low, whilst for some their blood cholesterol stays high no matter how thin they are. We can all take steps towards a healthier heart by eating a balanced diet and taking at least 30 minutes of moderate physical activity five times a week.": ​BBC NEWS | Health | Thin people 'must exercise too'
 
Watu wanafakamia vyakula vya hovyo hovyo, kuvuta sigara, kunywa kupindukia wakati mwingine kwa kutaka sifa kwamba yeye anaweza kufakamia bia nyingi, au glass nyingi za whisky/nyagi au kutaka kuonekana naye wa MUJINI kumbe anaharakisha safari yake ya umauti!!! Watu wa karibu wakimwambia analeta za kuleta, "Wote tutakufa". Kula vyakula ambavyo havidhuru afya yako ni muhimu sana lakini bahati mbaya wengine wametia pamba masikioni.

Tatizo la kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambikiza is an emerging problem in Tanzania, lakini bado hatuaelekeza kacho yetu kwenye preventive measures. Tahadhari zimeshatolewa na vombo mbalimbali kama TANNA. Vyanzo vipya vya magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na unywaji pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara, na kuaacha kula vyakula vya asili na kula vya fast food.

Nafikiri pia kuna tatizo kuhusiana na uandaaji wa vyakula vingi tunavyokula. kwa mujibu wa mkutano wa TANNA uliofanyika mwaka jana, wauguzi wamegundua kuwa "wabunge wengi wanakabiliwa na matatizo haya, hivyo jamii inapaswa kuelimishwa ili kujiepusha na magonjwa haya”: Ulaji usiofaa huchangia magonjwa yasiyoambukiza
 
Last week nilikuwa namuambia kijana mmoja, bora ukimwi kuliko kisukari. Management ya kisukari ni ngumu sana, ukimwi especially kwa sababu masharti ya chakula sio makali walau its manageable.

Non infectious diseases ni global issue kwa kweli. Risk factor kwa ajili ya zote ni pamoja na obesity, smoking and sedentary life.
EMT, lete na elimu ya Kisukari, nadhani hili ndio gonjwa tata kuliko yote hayo mnayosema, mtu mwenye High blood Pressure anapiga kazi kwa wife wake kama kawa lakini mwenye Kisukari, mh, full fedheha binafsi nadhani hili gonjwa ndio baya kuliko hata ukimwi, mwenye uelewa zaidi ya namna ya kujikinga please, hebu tupeni nyuzi.
 
Last week nilikuwa namuambia kijana mmoja, bora ukimwi kuliko kisukari. Management ya kisukari ni ngumu sana, ukimwi especially kwa sababu masharti ya chakula sio makali walau its manageable.
Non infectious diseases ni global issue kwa kweli. Risk factor kwa ajili ya zote ni pamoja na obesity, smoking and sedentary life.
Katika nchi zilizoendelea ambazo zimefanikiwa kupunguza kama si kuondoa infectious diseases tatizo linalo wakabili na ambalo linaongezeka kwa kasi ni non-infectious disease.

Chanzo kikubwa ni sedentary life na malnutrition (bad feeding).
Kwetu sisi hili halijawa tatizo kubwa kuliko infectious disease.
Watu wanaokufa kwa maradhi ya kuambukiza ni wengi kuliko yasiyoambukiza.

Management ya maradhi iwe infectious au non-infectious yanategemea sana life standard, poverty na education.
Kwangu mimi elimu ni muhimu kuliko kitu kingine. Watu wakiwa na ufahamu sehemu ya kubwa ya tatizo imeondoka.

Management ya maradhi katika individual au public level ni elimu.
Ukiongelea sukari inabidi ueleze sukari ya aina gani ili uweze kuwa na ulinganifu na kitu kingine.
Juvenile onset (type 1) au mature onset(type 2). Kwa ufupi type 2 inaweza kudhibitiwa bila dawa kama kuna ufahamu wa kutosha kuhusu ugonjwa, dalili na masharti yanayoambatana ambayo si magumu kihivyo.

Huko vijijini watu wanaokufa kwa anemia (upungufu wa damu) unaoweza kutoka hata na minyoo ya safura ni wengi. Tatizo la non-infec si kubwa kwasababu vitu kama obesity ni kidogo, watu bado wanakula vyakula vya kawaida na shughuli zao za kila siku zinawasidia sana kuepuka vitu kama obesity.

Nadhani tunaliangalia tatizo hili kimjini zaidi kuliko kitaifa. Tukiweka matatizo ya afya kwa ujumla wake hili halijawa kubwa kwa kiasi hicho.

Ukubwa wake unaonekana kwasababu idadi ya watu inaongezeka, kwa mfano kama mwaka 2010 kulikuwa na wagonjwa 10,000 waliofika muhimbili wa kisukari na sasa ni 15,000 tatizo limekua kwa asilimia 50.

Tukilinganisha na wagonjwa 100,000 wa kuhara ambao sasa wanafikia 120,000 tunawezaje kuogopa kisukari zaidi?


 
Baada ya hapo ulishushia na nini?

4c1d6398057911e3963b22000a1f9c8c_7.jpg

Lazima atakuwa alishushia na Pepsi bariiidi....
 
Ubize wapi. Wengi utatukuta baa kuanzia ijumaa jioni hadi jumapili usiku tukipiga kilaji na nyama choma kwa kwenda mbele.

Nafikiri wengi wetu tumezoa kuishi kama tunavyoishi kwa sababu hakuna motivation hasa ya kitaifa katika kufanya mazoezi.

Hatuambiwi madhara ya kutofanya mazoezi ya mara kwa mara. Kwa watu wa mijini hasa maofini hili ni tatizo kwa sababu cardiovascular activities ni chache sana.

Kwa hiyo, ukikuta mtu ambaye anafanya mazoezi kweli anajituma.

Ndugu yangu ukisubiri kuambiwa itakula kwako kua ka mwehu tu mwisho unazoea mazoezi ndio mpango mzima!
 
Nimejitahidi sana yani kaah..nina mwezi wa nne sijala chips na mwezi wa tatu sijanywa soda juice tu..kisukari na presha ni noma

It is not a matter ya kutokula vyakula fulani bali zaidi ni kula diet iliyokamilika.

Baada ya kujizua tuu kutokula ships na kutokunywa soda kwa muda wa miezi minne umekuwa unakula nini?

Hiyo juice unayokunywa umetengenezwa kivipi?
 
Hakuna kitu kigeni, tunashtuka kwasababu hatukujua kuwa tunaishi na matatizo.

1. Maradhi yasiyoambukiza kama kiharusi na ugonjwa wa moyo yamekuwepo na yapo vijijini.
Tofauti na zamani tukiita kapigwa kibao na jini mdomo ukaenda upande siku hizi tunajua ni kiharusi au stroke.
Tofauti na vijijini na zamani katupiwa mnyama ghafla kafariki siku hizi tunajua ni sukari au presha.

Baadhi ya watu wa vijijini wanaweza kusema mtoto anaharisha kwa sababu ya meno ya nailoni, kwa sababu bibi au babu yake hajatambikiwa au kachukuliwa msukule. Bwana afya kwa ugonjwa huo huo anaweza kusema mtoto kaambukizwa ugonjwa huo kutokana na mazingira machafu yasiyo na vyoo pamoja na maji masafi ya matumizi ya nyumbani. Kwa upande wake, Mwalimu anaweza kusema kuwa yote haya huletwa kwa kutokuwa na elimu.

Idadi ya watu wenye high blood pressure inatofautiana kati ya vijijini na mijini. Kwa mfano, inadaiwa Mara vijijini ni asilimia 2.6 wakati Dar ni asilimia 10.4. Hata hivyo, hizi ni data za nyuma kidogo.

Ugonjwa wa kisukari nao umeongezeka kwa asilimia 20 kwenye wilaya 50. Inadaiwa kuwa tafiti zilizofanyika mwaka 1986/87 na baadaye mwaka 1996/97 katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mara na Mwanza zilionyesha kuwa ugonjwa huo ulikuwa umeenea kwa asilimia moja vijijini na asilimia tatu jijini Dar es Salaam. Mwaka 2005 idadi hiyo ilifikia asilimia tano kwa wakazi wa Dar es Salaam: Kisukari kimeenea kwa 20%
 
EMT, lete na elimu ya Kisukari, nadhani hili ndio gonjwa tata kuliko yote hayo mnayosema, mtu mwenye High blood Pressure anapiga kazi kwa wife wake kama kawa lakini mwenye Kisukari, mh, full fedheha binafsi nadhani hili gonjwa ndio baya kuliko hata ukimwi, mwenye uelewa zaidi ya namna ya kujikinga please, hebu tupeni nyuzi.

Yaani wewe una-relate magonjwa na uwezo wa kupika kazi kwa wife tuu siyo eh? Tuko upo?

========================================

Huu ndiyo ugonjwa wa kisukari

Ugonjwa wa kisukari au Diabetes Mellitus hutokea pale tezi Kongosho au pancrease inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu au kitaalamu hyperglycemia. Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti sukari katika damu.

Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu katika nchi nyingi duniani zikiwemo za bara la Afrika na Tanzania ikiwemo ni ugonjwa wa kisukari. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 285 wanasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari duniani ambapo karibu asilimia 90 ya wagonjwa hao wana aina ya pili ya kisukari. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, idadi ya watu wenye kisukari inaongezeka kwa kasi na wataalamu wanasema kuwa, ifikapo mwaka 2030 idadi hiyo itaongezeka maradufu.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kisukari katika nchi za Asia na Afrika, na inasemekana idadi hiyo inatokana na kukua miji na mabadiliko ya maisha ya watu katika nchi zinazoendelea, na labda kutokana na kuiga mifumo ya maisha ya Kimagharibi. Katika miaka 20 iliyopita wagonjwa wa kisukari wameongezeka kwa kiasi kikubwa nchini Marekani ambapo mwaka 2010 watu milioni 26 walikuwa na ugonjwa huo, huku wengine milioni 7 wakiwa hawajagunduliwa.

Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa kuwa na kiwango kidogo cha Insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili. Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa glucose ambayo ni chanzo cha nguvu mwilini huingia katika damu.

Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa Kongosho au kwa kimombo pancrease kutengeneza kichocheo cha Insulin. Kazi ya insulin ni kuondoa glukosi katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati. Watu wenye ugonjwa wa kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo. Huenda Kongosho zao haziwezi kutengeneza insulin ya kutosha, au seli za mwili wao haziathiriwi na insulin kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.

UGONJWA WA KISUKARI UMEGAWANYIKA KATIKA MAFUNGU MATATU

1. Fungu la kwanza ni Kisukari Aina ya Kwanza au Type 1 Diabetes Mellitus.

Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalumu zinazotengeneza homoni ya insulin zinapokosekana katika tezi kongosho au zinapoharibika kutokana na sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu. Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa tezi kongosho kunakoweza kufanywa na magonjwa ya kinga ya mwili ya mtu mwenyewe au auto-immune diseases, au kushambuliwa na vyanzo visivyojulikana.

Kwa vile, uharibifu katika tezi kongosho hupelekea kutokuwepo kabisa insulin mwilini au insulin kuzalishwa kwa kiwango kidogo sana, wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano au pampu kila siku za maisha yao ili waweze kuishi. Kwa sababu hiyo aina hii ya kisukari huitwa pia Kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM).

2. Fungu la pili ni Kisukari Aina ya Pili au Type 2 Diabetes Mellitus.

Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua utendaji kazi wa homoni ya insulin, au seli kushindwa kutumia insulin ipasavyo. Hali hii mara nyingi husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutoushughulisha kabisa mwili (physical inactivity). Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa kwa kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi na utendaji kazi wake, wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM).

3. Aina ya tatu ya Kisukari ni Kisukari cha Ujauzito au Gestational Diabetes Mellitus.

Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2 hadi 5 ya mama wajawazito wote ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua. Hata hivyo karibu asilimia 20 mpaka 50 ya mama wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea kuwa na ugonjwa huo hata baada ya ujauzito na hatimaye kuwa na aina ya pili ya kisukari maishani.

KISUKARI HUSABABISHWA NA NINI?

Sababu za kisukari hutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa huo. Kwanza tutatuzungumzia yanayosababisha mtu apatwe na aina ya kwanza ya kisukari. Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi virusi kama vile Coxsackie virus type B4. Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za baadhi ya vyakula (food borne chemical toxins), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng'ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto uushambulie mwili wenyewe na hivyo kusababisha uharibifu katika tezi kongosho.

Aina ya pili ya kisukari kwa ujumla husababishwa zaidi na jinsi mtu anavyoishi na pia matatizo ya kijeneteki. Aidha kuongezeka uzito na unene kupita kiasi (obesity) vilevile huchangia kutokea aina hii ya kisukari. Sababu nyingine ni pamoja na kuongezeka umri, maisha ya kivivu na kutofanya mazoezi na pia ugonjwa wa tezi kongosho (pancreatitis) ambao hufanya insulin inayozalishwa kuwa na ufanisi mbovu au ya kiwango cha chini.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NI ZIPI?

  • Kukojoa mara kwa mara hali inayojulikana kitaalamu kama polyuria.
  • Mgonjwa kuhisi kiu kali na kunywa maji kwa kiwango cha kupitiliza (polydipsia).
  • Mgonjwa kuhisi njaa na kula mara kwa mara (polyphagia).
  • Kuchoka haraka Kupungua uzito Vipele mwilini ambavyo kitaalamu huitwa diabetic dermadromes.
Na wagonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya kupata maambukizi katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri. Aidha kuna dalili maalumu ambazo hutokea kwa wagonjwa wa kisukari iwapo mgonjwa atapatwa na mojawapo ya madhara (complications) ya ugonjwa huo. Madhara hayo ambayo hujulikana kwa kifupi DKA hutokea kwenye aina ya kwanza ya kisukari na huwa na dalili zifuatazo:

  • Mgonjwa kutoa harufu ya acetone (inayofanana kidogo na harufu ya pombe).
  • Mgonjwa hupumua kwa haraka na kwa nguvu,
  • kujihisi kichefuchefu,
  • kutapika,
  • kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu.
  • Kupoteza fahamu mgonjwa kunakoitwa Hyperosmolar Non-ketotic coma hutokea kwenye kisukari cha aina ya pili ambapo mara nyingi husababishwa na upungufu wa maji mwilini.
Baada ya mtu kuwa na dalili za ugonjwa wa kisukari matibabu huanza baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitisha kwamba kweli ana ugonjwa huo. Baada ya vipimo tunaweza kusema mtu fulani ana kisukari iwapo:

  1. Kiwango cha sukari kwenye damu kinatakuwa sawa na 126mg/L, kipimo ambacho kwa kawaida hufanyika kwa mtu ambaye hajakula chakula chochote. Kwa jina jingine kipimo hiki huitwa Fasting Blood Glucose (FBG).
  2. Kiwango cha sukari kwenye damu kinapokuwa sawa na 200mg/L kwa mtu ambaye amelishwa gram 75 za glucose ndani ya masaa mawili. Kipimo hiki pia huitwa Oral Glucose Tolerance Test (OGTT). Au iwapo mgonjwa atafanyiwa kipimo kinachoitwa glycoslytated hemoglobin (Hb A1C) na kuwa chanya
KISUKARI HUWEZA KUSABABISHA MADHARA YAFUATAYO KWA MHUSIKA IWAPO HAKITATIBIWA INAVYOPASWA

  • Kuziba kwa mishipa mikubwa ya damu kutokana na kuzungukwa na mafuta (Atherosclerosis).
  • Mgonjwa kushindwa kuona vizuri au kushindwa kuona kabisa na kuwa kipofu (diabetic retinopathy)
  • Kushindwa kufanya kazi vizuri kwa figo,
  • Mgonjwa kuhisi ganzi na kupoteza hisia mikononi na miguuni kwa sababu ya kuharibika kwa neva (diabetic neuropathy),
  • Kupungua kwa nguvu za kiume.
  • Vidonda (diabetic ulcers) hususan vidoleni.
  • Hali hii wakati mwingine humpelekea mgonjwa kukatwa viungo vyake.
  • Mgonjwa kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya vimelea mbalimbali hasa bakteria kutokana na kuharibika na kushindwa kufanya kazi vizuri kwa chembe nyeupe za damu.

Ugonjwa wa kisukari kama hautodhibitiwa unaweza kumsababishia mgonjwa madhara makubwa na kuathiri karibu kila kiungo mwilini. Kama tulivyosema ugonjwa huo huathiri moyo na mishipa ya damu, macho, figo neva na hata fizi na meno. Ingawa mgonjwa wa kisukari anapotibiwa na kujua jinsi ya kudhibiti kiwango chake cha sukari mwilini suala hilo hupunguza na kuzuia madhara ya ugonjwa huo, lakini kwa bahati mbaya hata kisukari kinachodhibitiwa vyema baada ya muda mrefu humuathiri mgonjwa.

Takwimu zinaonyesha kuwa, wagonjwa wenye kisukari hufa zaidi ikilinganishwa na wasiokuwa na ugonjwa huo kutokana na madhara wanayoyapata, sababu kuu ikiwa ni ugonjwa wa moyo. Zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa wa kisukari hupata mshituko wa moyo huku asilimia 25 wakipata kiharusi. Njia bora zaidi ya kuzuia hayo yote ni kuhakikisha kwamba kiwango cha glucose katika damu kiko katika hali yake inayotakiwa kila wakati, suala ambalo kwa bahati mbaya huwa gumu kwa wenye ugonjwa huo.

Watu wazima wenye ugonjwa wa kisukari hushambuliwa na maradhi ya moyo mara mbili hadi 4 zaidi kuliko wasiokuwa na ugonjwa huo, na hatari ya kupata mshituko wa moyo ni mara 4 zaidi kwa wagonjwa hao. Tafiti pia zinaonyesha kwamba, kuharibika mishipa ya damu au kuharibika neva kunaweza kusababisha matatizo ya miguu kwa wagonjwa wenye kisukari, suala ambalo huenda likapelekea kukatwa miguu.

Utafiti unaeleza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya miguu inayokatwa bila kuumia sababu kuu huwa ni kisukari. Nchini Marekani ugonjwa huo ni chanzo kikuu cha watu wenye umri kati ya miaka 20 hadi 74 kuwa vipofu. Inasemekana kuwa, hata kama mgonjwa wa kisukari atatibiwa na kudhibiti vyema kiwango cha sukari mwilini, lakini baada ya miaka kadhaa taratibu ugonjwa huo huathiri macho na moyo wake. Kwa wale ambao hawajali matibabu na kudhibiti kiwango cha glucose mwilini hupata madhara hayo mapema zaidi.

Baada ya kuyaona madhara ya kisukari kwa viungo kadhaa mwilini, suala hilo linatuonyesha umuhimu wa kujikinga na ugonjwa huo na pia umuhimu wa kuutibu na kuudhibiti kwa wale ambao tayari ni wagonjwa. Matibabu ya kisukari hutegemea aina ya kisukari ingawa kwa ujumla hujumuisha matumizi ya dawa na njia ya kubadilisha mfumo au staili ya maisha. Kwa aina ya pili ya kisukari au Type 2 DM, aina hii ya kisukari huweza kutibiwa ama kwa dawa, kubadili mfumo wa maisha au vyote viwili kwa pamoja.

Katika kubadili mfumo wa maisha, ni muhimu mgonjwa kutilia maanani na kuwa makini na aina ya vyakula anavyokula na kujitahidi kufanya mazoezi na kuushughulisha mwili ili kuepuka kuongezeka uzito kupita kiasi. Kuhusiana na aina ya vyakula inashauriwa sana;

  1. Kupunguza kula vyakula vyenye mafuta ya kolestroli ambayo ni mafuta mabaya, yaani kula walau chini ya miligramu 300 za kolostroli kwa siku.
  2. Kujitahidi sana kula vyakula vya kujenga mwili vya proteini angalau kwa asilimia 10-15 kwa siku. Vyakula hivi ni pamoja na nyama na mboga za majani.
  3. Kuwa makini na ulaji wa vyakula vya wanga au carbohydrate. Inapasa kuhakikisha kuwa havizidi asilimia 50-60 ya chakula unachokula kwa siku na visiwe ndicho chakula kikuu kwa siku.
  4. Kupunguza utumiaji wa chumvi katika chakula na kuacha kabisa au kupunguza kunywa pombe.
Suala la ufanyaji mazoezi ni jambo muhimu kwa vile mazoezi husaidia sana kupunguza uzito, kuondoa mafuta yanayopunguza utendaji kazi wa Insulin mwilini na hivyo kuongeza ufanisi na utendaji wa homoni hiyo muhimu mwilini. Vile vile mgonjwa mwenye aina hii ya kisukari anaweza pia kupewa dawa ambazo atatakiwa kunywa kila siku huku akiendelea kufuata ushauri kama tulivyoeleza. Dawa hizo ambazo huitwa pia dawa za kushusha kiwango cha sukari mwilini (Oral Hypoglycemic drugs) ni kama vile Metformin na Glipizide.

Ifahamike pia kuwa, wapo baadhi ya wagonjwa wa aina hii ya pili ya kisukari (Type 2 DM) ambao pamoja na kutumia dawa za kunywa za kushusha sukari na kufuata ushauri wa daktari kuhusu mfumo wao wa maisha bado njia hizo zinaweza zisishushe sukari inavyotakiwa. Katika hali kama hiyo, wagonjwa hawa huweza pia kudungwa sindano za Insulin kwa muda ili kushusha kiwango cha sukari mwilini. Katika matibabu ya Aina ya Kwanza ya kisukari au Type 1 DM pamoja na kurekebisha aina ya vyakula na kufanya mazoezi, wagonjwa huhitaji kichocheo cha Insulin ili kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.

DAWA ZA INSULIN ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAKUU MATATU

Kuna zile zinazofanya kazi kwa muda mfupi, za muda wa kati na zinazofanya kazi kwa muda mrefu. Kulingana na utendaji wa dawa hizo, mgonjwa anaweza kuelekezwa jinsi ya kujidunga mwenyewe sindano za Insulin nyumbani kwa kufuata maelekezo yafuatayo:

  • Asubuhi: Mgonjwa hujidunga 2/3 ya insulin nusu saa kabla ya kunywa chai.
  • Usiku: Mgonjwa hujidunga 1/3 ya insulin nusu saa kabla ya chakula cha usiku.
Aidha katika hii 2/3 inayotolewa asubuhi, 2/3 yake huwa insulin inayofanya kazi kwa muda wa kati na 1/3 ni ile inayofanya kazi haraka au kwa muda mfupi.

KUMBUKA

Inasisitizwa sana kutojidunga sindano za ugonjwa huo bila kupata maelekezo sahihi ya daktari. Kwa maelekezo zaidi na sahihi ya matibabu kwa kutumia Insulin ni vizuri kuhudhuria kiliniki za kisukari. Pia njia za kutibu ugonjwa wa sukari hutolewa hospitalini, na hayo ni matibabu maalumu yakoma aina ya hyperosmolar non-ketotic (HONKC). Mkazo huwekwa katika kusahihisha upungufu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa kati ya lita 8 hadi 10 za maji aina ya Normal saline. Iwapo kuna ugumu katika kusahihisha kiwango cha sukari mwilini kwa kutumia dawa za kunywa, Insulin inaweza kutolewa.

Matibabu mengine maalumu ni ya kutibu Diabetic Ketoacidosis(DKA).

Kama ilivyo kwa hyperosmolar non-ketotic coma, matibabu ya DKA nayo hutolewa hospitali chini ya uangalizi maalumu wa madaktari. Hii ni hali ya hatari, ambapo isipotibiwa kwa umakini, inaweza kumuua mgonjwa. Jambo la muhimu katika matibabu haya ni kusahihisha upungufu wa maji mwilini, kusahihisha kiwango cha potassium katika damu na kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu kwa kutumia Insulin.

Wasomaji wa Blog hii na makala hii

Tunapaswa kujua kuwa unene na kuongezeka uzito wa mwili kwa kiwango cha kupindukia ni miongoni mwa sababu kuu zinazopelekea mtu kupata magonjwa mbalimbali kama vile ugonjwa wa moyo, kiharusi, kisukari, shinikizo la damu na mengineyo. Pia baadhi ya tabia kama vile kuvuta sigara, kunywa pombe, kutumia madawa ya kulevya na ngono za ovyo vile vile husababisha mtu kupatwa na baadhi ya maradhi. Kwa kuwa suala la unene wa kupita kiasi limekuwa janga la kiafya katika nchi nyingi hasa zinazoendelea na ni suala nyeti ambalo humsababishia mtu magonjwa mbalimbali kikiwemo kisukari.

Namalizia kwa utafiti unaosema kwamba, wale wanaokoroma wakati wakilala, wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari kuliko wale wanaolala kimya. Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliofanywa kwenye chuo kikuu cha Yale nchini Marekani, wale wanaokoroma sana wanapolala, wanakabiliwa na hatari ya kupata kisukari kwa asilimia 50. Wataalamu wanasema pia kuwa, kushindwa kupumua usingizini huenda kukahusiana na kisukari aina ya pili, bila kujali sababu nyinginezo kama vile umri, jinsia, uzito na hata asili anayotoka mtu.

Kukoroma sugu, au kitaalamu sleep apnea ni hali inayosababishwa na kushindwa kufanya kazi njia ya hewa, suala ambalo humfanya mtu aamke mara kadhaa usingizini wakati anapolala. Hali hiyo inahusiana na baadhi ya mabadiliko ya umetaboli au hali ya ujenzi wa seli na uvunjaji vunjaji wa kamikali zinatokana na chakula mwilini, kwa kimombo 'metabolism'.

Imeandikwa na;
Sayi manyanda
manyandahealthy@gmail.com
www.manyandahealthy.blogspot.com
HUU NDIO UGONJWA WA KISUKARI AU DIABETES MELLITUS. « ManyandaHealthy
 
....kwa upande mwingine wengi tunakula kinachowezekana sio tulichopanga mf. wanga kwa wingi na kama ni balance diet mpaka tupate ofa!

Ofa ya nini? Bia? Nyama choma?
 
dawa ya shinikizo la damu ni MAZOEZI vijana tufanye mazoezi,pili tuepuke kula chips na tuzingatie kunywa maji ya kutosha pungufu kwa siku angalau lita 2,sasa hasa wadada wao ni soda tu kumbe wanajaza chemical mwilini

Siyo vijana tuu, bali kila binadamu mdogo kwa mkubwa anatakiwa afanye mazoezi na ale balanced diet kwa afya yake.
 
Last week nilikuwa namuambia kijana mmoja, bora ukimwi kuliko kisukari. Management ya kisukari ni ngumu sana, ukimwi especially kwa sababu masharti ya chakula sio makali walau its manageable.

Non infectious diseases ni global issue kwa kweli. Risk factor kwa ajili ya zote ni pamoja na obesity, smoking and sedentary life.

Kwa mujibu wa WHO kuna wagonjwa wapya saratani 20,000 kila mwaka. Bahati mbaya hatuna statistics za kitaifa za ugonjwa huu, lakini data kutoka Ocean Road, katika ya mwaka 1972 na 2000 kumekuwa na uongezekaji wa wagonjwa wanaokwenda kutibiwa kwa asilimia 50. Asilimia 60 ya wagonjwa ni wanawake wanaoenda pale wakiwa na cancer ya cervix. Hizi bado ni data za zamani kidogo.
 
Ndugu yangu ukisubiri kuambiwa itakula kwako kua ka mwehu tu mwisho unazoea mazoezi ndio mpango mzima!

Watu wanatakiwa kuelimishwa juu ya magonjwa yasiyoambukiza na jinsi ya kujikinga nayo.
 
Tutabakoi kweli? Na haya magari badala ya kutembea na kugombania daladala, ni kukaa tu.
Kupanda daladala ni mazoezi tosha.
 
Back
Top Bottom