Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Crescentius Magori, ametangaza kuwa kikao kilichofanyika Bunju hakikuwa kikao rasmi cha Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama, hivyo maamuzi yote yaliyotolewa katika kikao hicho ni batili na yanakwenda kinyume na Katiba ya klabu.
Soma: Try Again arejeshwa Simba, aunda Baraza jipya la Wadhamini lililopitishwa na Wanachama Bunju
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Katiba ya Simba ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2026 inaelekeza kuwa Mkutano Mkuu Maalum uitishwe na Mwenyekiti wa Klabu kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi. Bodi imesema itakutana Agosti 3, 2026 kujadili ajenda za mkutano huo, huku tarehe rasmi ya Mkutano Mkuu ikitangazwa baadaye.
Soma: Try Again arejeshwa Simba, aunda Baraza jipya la Wadhamini lililopitishwa na Wanachama Bunju