Na hii ndio kitu waCCM na MATAGA yao hawaelewi unapowaambia tatizo la ufisadi wa Tanzania si Lowassa & Co, bali ni mfumo wa utawala. Mfumo wenyewe ni fisadi (wizi wa pesa za walipa kodi ambao umehalalishwa kwa kutungiwa sheria na watawala = kleptocracy), na kwa mantiki hii maamuzi mengi ya Magufuli ni ufisadi (mfano, CIA, ndege za atcl, nk). Malipo na mafao ya wabunge ni aina nyingine ya ufisadi uliokubuhu. Mbunge analipwa mabilioni na mabilioni kwa miaka kumi, kumi na mitano lakini jimboni mwake wananchi wanakunywa maji ya vidimbwi, watoto wanakaa sakafuni kusoma, nk. Na kila baada ya miaka mitano mtu huyo huyo anarudi kuomba kura. Sasa hakuna namna nyingine yo yote ile ya kuuondoa huu ufisadi bila kubadilisha mfumo, na njia ya kubadilisha mfumo ni Katiba Mpya, na kwa hakika katika hili tuliishapiga hamtiamo wako swaltua - Rasimu ya Warioba. Inahitaji ujasiri tu wa waTz kukubaliana turudi pale tulipopumzikia na kuendelea na safari. Ninafurahi sana kuona TAL analisisitiza jambo hili. Bahati mbaya ni wachache wanamwelewa.