N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Wanabodi, leo nimepata nafasi ya kuipitia hii Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na nilichogundua ni jambo la kutia mashaka.
Yale malodge, maguest house na hata baadhi ya nyumba ndogo za kulala wageni ambazo huwa "wanawaanika ma baby daddies" au wateja kwa staili ya rejesta za wazi, kwa hakika wanavunja sheria hii.
Ibara ya 30 ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, ambayo inapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, inasema hivi:
Sasa swali ni kwa nini tunapofika pale lodge au guest house, tunalazimishwa kuandika taarifa zetu binafsi kwenye rejesta ya wazi ambayo kila anayekuja baada yako anaweza kuziona? Ukiwauliza wanakwambia Polisi wanataka tufanye hivi na ni maelekezo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa___Sasa najiuliza ina maana hayo maelekezo yanatolewa bila uelewa kwamba kuwaelekeza maloji hivyo ni kuvunja sheria hii mpya? au elimu haijawaingia bado!
Majina, namba za simu, hata utambulisho wako ikiwa ni pamoja na unakotoka na unakokwenda na kabila lako – vyote vinabaki wazi kwa yeyote anayeingia baada yako kwenye lile daftari linalokuwa pale mapokezi.
Huu si uvunjaji wa sheria?
Kwa hoteli kubwa, mfumo wao ni tofauti. Unapewa fomu/kadi za kujaza taarifa zako, na mwenye hoteli ndiye anayehifadhi taarifa hizo kwa utaratibu wa siri.
Lakini huku kwenye malodge na maguest house, mambo ni hadharani kabisa – jambo linaloacha mianya ya uvunjifu wa faragha, udhalilishaji na hata uhalifu wa kimtandao "mfano mtu anaweza kupata namba yako ya simu hapo akaanza kukutumia ujumbe wa ile pesa tuma kwenye namba hii...".
Maswali kwa wanabodi:
MY TAKE:
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi iheshimiwe na Ifuatwe. Si sawa kwa wananchi kuanika taarifa zao wazi kwenye hata madaftari ya wazi. Pia, tukumbushane kumpa mtu namba yangu ya simu bila ridhaa yangu ni kosa kwa mujibu wa hii sheria. Pia wale michepu zingatieni kuwaanika mabebi dady wenu kwenye mitandao ni kosa mkiwa sued mtalipa mamilioni in compansation!
Nyadikwa

"Mtu hatachakata taarifa binafsi nyeti bila ridhaa ya maandishi ya mhusika wa taarifa binafsi."

- Kwa hali hii, ni sahihi kusema malodge na maguest house nyingi zinavunja sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi?
- Je, kuna haja Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wachukue hatua juu ya hili kwa kutoa maelekezo ya kidhibiti kwa lodges na taasisi zote nchini kulinda taarifa binafsi za watu?
- Je, ni wajibu wa mteja kudai utaratibu wa fomu binafsi badala ya rejesta za wazi, au ni jukumu la wamiliki kubadilisha mifumo yao kwa kuzingatia sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ambayo tayari inafanya kazi?