Don YF
JF-Expert Member
- May 24, 2014
- 10,494
- 9,854
By Aurea Simtowe
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameagiza madaktari waliokimbia hospitali ya rufaa ya Kitete kwa madai ya maslahi madogo kufuatiliwa ili kuzilipa fedha za Serikali.
Madaktari hao wamekimbilia hospitali binafsi kwa madai kuwa huko wanalipwa fedha nyingi.
Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumamosi Januari 30, 2021 baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya rufaa Kitete lililogharimu zaidi ya Sh600 milioni.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa Mkoa wa Tabora, Dk Marko Waziri amesema madaktari wanaoondoka katika hospitali hiyo wengi walikuwa wakisema maslahi ni madogo.
Amesema waliondoka na kumueleza kuwa mtu akiwa na shahada ya kwanza akajiendeleza na kupata shahada ya uzamili, tofauti ya mshahara wake na mtu mwenye shahada ya kwanza ni kati ya Sh200,000 hadi Sh300,000.
“Kuna mmoja nasikia ameajiriwa sehemu analipwa Sh5 milioni hivyo nadhani wanatoka huku serikali kwenda hospitali binafsi kutafuta hela,” amesema Dk Waziri
Magufuli amesema kama maslahi ni madogo kwa nini madaktari hao waliomba kuajiriwa serikalini na kuziba nafasi za madaktari wengine.
“Kazi ya udaktari ni kujitolea kama sadaka hata manesi hakuna mtu anayeridhika na mshahara lakini kama alipewa kazi yake akaajiriwa kwa nini asiifanye."
“Mwaka jana niliajiri madaktari 1000, kumbe daktari huyohuyo alipofika hapa akanusa tu akaondoka pamoja na mshahara wetu kwa nini asishtakiwe kwa wizi,” amesema Magufuli
Kwa mujibu wa Dk Waziri hospitali hiyo ina madaktari bingwa watano lakini watatu wameondoka.
“Na walisomeshwa na serikali, kwa gharama ya serikali na hawajarudisha hizo fedha, watafute hao madaktari ili tuje tujue hela zetu zipo wapi.”
“Kwa sababu hakuna mtu anayeridhika na mshahara hata mimi siridhiki nao, hata manesi hawa hawaridhiki lakini wanajituma, tunataka sisi wote matatizo yetu tuyatatue kwa pamoja kwa sababu hatuwezi kuyatatua kwa siku moja halafu mtu akaingia kwa ubinafsi,” amesema Magufuli.
Amesema hiyo ni kwa sababu hatua mbalimbali zinachukuliwa ili kuimarisha huduma za afya na miongoni mwa hatua hizo ni kuajiri watumishi zaidi ya 14,000 katika kipindi cha miaka mitano, kujenga hospitali na vituo vya afya, hospitali za rufaa, mikoa na zahanati
“Tumeanza na hivi baqdaye tunaingia katika maslahi ya watumishi wa afya, tunajua wanafanya kazi kubwa sana ya kujitolea na nawapongeza sana, kinachohitajika ni uzalendo pia.”
“Ukikimbia kinamama hapa wanaumwa wengine wanataka kufanyiwa upasuaji wewe unaenda huko Kamanga (hospitali). Mfuatilie huyo daktari aliyekimbia hapa mfuatilie huyo daktari ikiwezekana tunamfungia daktari tunafungia na hospitali aliyoenda kutibia,” amesema Magufuli
Amesema hilo litawafanya watu kutambua kuwa Wizara ya Afya si ya kuchezea kwa sababu watu wanasomeshwa kwa fedha za watanzania maskini na kupewa mikopo asilimia 100 lakini baada ya kumaliza wanakimbia kwa kudai maslahi madogo.
“Si ungekimbia wakati unasoma, hela yetu umekula halafu unasema maslahi madogo, tunataka maslahi yaboreshwe na hiyo ndiyo nia ya serikali hii lakini unaanza kimoja huwezi kuboresha maslahi wakati hospitali huna, majengo na vifaa,”
Amesema lengo la Serikali ni kuweka majengo ya kutosha na vifaa ili madaktari wafanye kazi katika maeneo mazuri kabla ya kuhamia eneo lingine.
“Lakini nataka niwahakikishie suala la maslahi yenu tunaliangalia kikamilifu kulingana na bajeti itakavyokuwa inakuja, nataka hilo niwahidi lakini kukimbia ni dhambi,” amesema Magufuli.