Magufuli achana na Raila,sifa zake "chafu" Msaidizi wake wa karibu kazianika hadharani kupitia kitabu

Magufuli achana na Raila,sifa zake "chafu" Msaidizi wake wa karibu kazianika hadharani kupitia kitabu

Haha siku mkizijua tabia za John kinaga ubaga mtalia na kusaga meno..... hayo ya Raila ni tone ktk dimbwi la tabia za John.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Pengine Miguna wa Miguna ataandika sura moja kuhusu tabia za marafiki zake Odinga. Kiuhalisia yule ni mtu hatari sana. Ukiona mtu anayefanya mbinu watu wake wasipate chakula ili apate umaarufu wa kisiasa muogope kama ukoma.

Bahati nzuri kwenye kampeni katika nchi yenye demokrasia kama Kenya alitumia jina la mwandani wake kuomba kura akaangukia pua kwenye uchaguzi, kwamba mkinichagua nitaongoza kama rafiki yangu. Hii kauli ilimgharimu sana RAO.
 
Raila ameanikwa mambo yake na aliyekuwa Msaidizi wake Mkuu,mshauri wake wa mambo ya kisiasa,kisheria na katiba kipindi cha serikali ya umoja wa kitaifa nchini kenya,MIGUNA MIGUNA,kama mnakumbuka,Raila alikuwa waziri Mkuu,wakati Mwai Kibaki ni Rais baada ya zile vurugu na mauaji baada ya Uchaguzi

MIGUNA MIGUNA alitunga kitabu kiitwacho "PEELING BACK THE MASK" humo kamuanika Raila Odinga mambo yake yote ya binafsi(vidosho)mpaka ya Ofisini kwake,Ofisi ya Waziri Mkuu wa Kenya,hakika kamuacha uchi na pengine ndio sababu urais atabaki kuuota ndotoni

Bwana MIGUNA ndiye alikuwa mtu wa karibu sana na Raila Odinga,anajua mambo yake,hivyo mtanzania mwenzetu yeyote anayemsogeza Raila kwa ukaribu wa kupitiliza lazima tumuangalie kwa jicho kali

UKURASA wa 512,MIGUNA MIGUNA anaandika kwamba Ofisi ya waziri mkuu Raila ilikuwa kama pango la wanyanganyi,watu wenye briefcase za mapesa,bahasha za khaki,wauza unga,watakatisha pesa,wezi waliingia bila tabu,anasema familia ya Raila ilitajirika ghafla baada ya yeye kuwa waziri mkuu na anasema familia ya Raila ilikuwa inasaka mabilioni kama watu waliopandwa na kichwa

JPM kwa kauli zake huwa anasema hapendi wapiga dili,sasa urafiki wake na Raila kwa nini asiuvunje?

UKURASA WA 511

Anasema Raila ana udhaifu wa ajabu kwa wanawake wa kila aina bila kujali kwamba ameoa,mkewe anaitwa Idda Odinga,lakini misafara ya wanawake ilikuwa inamtembelea na wakati mwingine kumletea chakula,anatoa mfano wa wanawake kama Rachel Shebesh,Ann kairuki,na easthet Passaris,na anasema kulikuwa na mgogoro mkubwa kati ya mke wa Raila na Bi Rachel Shebesh,ambaye Raila alifanya juu chini mpaka akampa ubunge wa kuteuliwa akiwa acha wanawake wengi walioipigania ODM

Mwandishi anasema kuna kipindi walimwalika Raila Canada,baadae wakamfanyia dhifa nyumbani,Mara akatokea binti mwenye kama asili ya kinyarwanda,mgeni ambaye hakualikwa,ila baadae raila akawaambia ni kidosho wake,na walipoenda kumsabahi asubuhi hoteliniI,wakapishana na kidosho huyo akitoka chumbani kwa raila(manyoya)

Anaendelea kusema Raila ni mdhaifu kwenye Pombe,ngono na pesa,kama alikuwa hanywi pombe basi yuko na wanawake anafanya ngono,yeyote mwenye pesa halali au haramu kwa Raila alikaribishwa

Je Mambo haya yanafaa? Nakushauri umpige chini

Pia mwandishi MIGUNA MIGUNA katika UKURASA wa 175,mbali na kutaja ofisi ya waziri mkuu Raila kuwa ni shimo la rushwa,anasema Raila alijaza ndugu zake serikalini

Anasema Raila alimteua kaka yake Oburu Oginga kuwa naibu waziri wa fedha,mpwa wake Jakayo Midiwo kuwa mnadhimu wa ODM, Dada yake Akinyi Wenwa kuwa balozi Los Angeles,dada yake Beryl Qchieng kuwa mkuu wa mfuko wa pensheni wa watumishi wa Reli,mpwa wake Carey Orege kuwa katibu mkuu wizara ya maendeleo ya mikoa,mpwa wake Paul Gondi kuwa Mkurugenzi wa Geothermal Development Company,mpwa wake Ochilo Ayacko kuwa mkurugenzi wa Kenya Nuclear Electricity Project,mpwa wake Joe Aged alimpa nafasi kubwa katika kampuni ya Kenya Power Lighting,mpwa wa mkewe Agnes Odhiambo kuwa mdhibiti wa bajeti,pia aliteua nduguye Alex Kazongo kuwa mkuu wa shirika la pensheni,na mwingine Edward Ouko kuwa mkaguzi wa mahesabu

Nduguye James Ogundo alimpa ujumbe wa Bodi ya mfuko wa maendeleo ya jumbo nafasi iliyokuwa na malipo manono

Pesa za kampeni za Raila Odinga zilikuwa zinashikwa na dada yake Akinyi Walkoa au binti yake Rosemary Akeyo au George Opondo

Hivyo Raila ni mkabila wa kutupwa,nakushauri mheshimiwa Rais uachane naye,atakushawishi na wewe uwe mkabila na uwe mtu wa kuendekeza undugu wa kupitiliza

Pia Msaidizi mwingine wa Raila aitwaye Carol Omondi inadaiwa alitajirika ghafla na kuwa bilionea mkubwa,na ni huyu alitumwa kwenda ikulu ya Uganda kwa museveni wakajadili suala la bomba la mafuta,MIGUNA anasema Msaidizi huyo aliporudi kutoka uganda alikuja na sura ya "mpiga dili" halisi anayeashiria kuwa dili limekubali,

Je kwa nini museveni alibadili msimamo wa kulijenga bomba kupitia Mombasa na akaamua kupitia Tanga? Kuna siri gani? Raila alikwepa nini kenya? Ana mkono kiasi gani na ushawishi kiasi gani kwenye bomba hili?mkataba wa bomba na ujenzi kwa nini ni siri? Je kwa nini ujenzi wa bomba la mafuta ulizinduliwa wakati wakenya wakielekea kwenye uchaguzi? Hasa kupiga kura?ilikuwa kwa amelekezo ya Raila uzinduzi ufanyike ili Uhuru Kenyatta apungukiwe kura kwa kuwa alishindwa kulibakiza bomba kenya? Kumbuka raila ni rafiki wa JPM na pia akiwa waziri mkuu alituma watu wake mara kadhaa ikulu ya uganda,je JPM na museveni walikuwa na ajenda iliyojificha kipindi cha uzinduzi?

Mbona kagame na museveni walichekelea sana JPM alipokuwa rais na ghafla wakavunja urafiki na kenya(coalition of the willing?)

Mwandishi huyo MIGUNA MIGUNA anasema mkono wa raila kwenye dili umefika mpaka kwenye migodi ya shaba Zambia na machimbo ya Dhahabu DRC,
Raila ni nani na anataka nini au ana maslahi gani anataka kuyalinda Tanzania? Hajui kuwa mkuu wetu hapendi dili?

Hivi urafiki wa JPM na Raila chanzo ni nini? Kama ni kupinga ufisadi,mbona Msaidizi wa raila anadai raila ni fisadi wa kutupwa?

Pia mwandishi anasema chuo kikuu cha Minnesota kilimwalika Raila nchini marekani,kikaonyesha nia ya kusaidia chuo kikuu cha maseno nchini kenya,raila akaulizwa na wahusika awape contact person,raila akamtaja mkewe Idda Odinga! Dili,hela isitoke nje ya familia

Kitabu kina story nyingi nzito kuhusu raila,Mimi nimezitoa kwa ufupi,lakini mwisho raila alimtimua kazi msaidizi wake kwa kuwa walishindwa kuelewana katika mambo ya kupinga rushwa,ukabila na ufisadi

Nenda Google ukidownload upate habari kamili

Je nini sababu ya JPM kumfanya huyu jamaa rafiki? Kwenye kampeni tulimchangia? Tsh ngapi?
Urafiki wa JPM na Raila hauna uhusiano na urais wa nchi ni urafiki wa mtu na mtu kama mimi na wewe hivyo basi kila mtu ana haki ya kuwa na rafiki ampendae
 
Ila kwa kweli raila ana sura ya kilevi,tena ule ulevi wa kuyumba na kupepesuka
 
Hayo mawaa ya Raila usifananishe kabisa na Pogba..

Huyu ni balaa hasa kwenye kupenda wanawake..

Amezaa mpaka na mdogo wa mkewe..

Huko Mwanza kila mtaa inadaiwa ana mtoto..

Anapenda ngono kupita maelezo huyu.
Noma sana
 
Umetumwa ww sio bure

ningekushauri siasa za Kenya waachie wakenya wenyewe

usihusishe na tz urafiki wa mtu na mtu ni mambo binafsi
 
Punguzeni kelele Chadeko. Tunajua kuwa mlishinda uchaguzi wa Kenya.
 
Aisee angeshinda Raila, sijui ingekuwaje.
Ikulu za east africa zingekuwa hapatoshi kwa totoz
Zingekuwa zinapigwa threesome za kufa mtu.
Kuna mmoja kapewa uongozi pale uvccm, anatafunwa km njugu, anatembea kila kona ya dunia sasa
Sent From Ikulu-Magogoni street
 
Raila si kiongozi mzuri kwani mwaka 1982 alihusika na mapinduzi yaliyofanyika Kenya kwa muda na zaidi ya wakenya 2000 waliuawa. Raila yupo tayari kuona kenya ikisarambatika na watu kufa ili apate madaraka.
Ktk issue ile ya mapinduzi ya mwaka 1982 waliootuumiwa ktk mapinduzi yale ni Kaka yale Odinga aitwae OBURU OGINGA na Babake Mzee Oginga Odinga.

Huyu Raira ktk issue ile hakuwa na nguvu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miguna Miguna is live at JKL..
---------
Anasema Raila alimteua kaka yake Oburu Oginga kuwa naibu waziri wa fedha,mpwa wake Jakayo Midiwo kuwa mnadhimu wa ODM, Dada yake Akinyi Wenwa kuwa balozi Los Angeles,dada yake Beryl Qchieng kuwa mkuu wa mfuko wa pensheni wa watumishi wa Reli,mpwa wake Carey Orege kuwa katibu mkuu wizara ya maendeleo ya mikoa,mpwa wake Paul Gondi kuwa Mkurugenzi wa Geothermal Development Company,mpwa wake Ochilo Ayacko kuwa mkurugenzi wa Kenya Nuclear Electricity Project,mpwa wake Joe Aged alimpa nafasi kubwa katika kampuni ya Kenya Power Lighting,mpwa wa mkewe Agnes Odhiambo kuwa mdhibiti wa bajeti,pia aliteua nduguye Alex Kazongo kuwa mkuu wa shirika la pensheni,na mwingine Edward Ouko kuwa mkaguzi wa mahesabu

Kwa uwezo huu wa kuteua watu muhimu kwenye serikali ya kenya bila baraka za Rais mwenyewe; Raila kama waziri mkuu alikuwa rais basi!! Jipeni Muda kutafuta ukweli. Teuzi nyingi kipindi kile zilikuwa zinafanywa kwa kushauriana kati ya Rais na waziri mkuu.
----
The United States State Department Background Note: Kenya, updated 2 September 2011, observed that:―

The unicameral National Assembly consists of 210 members elected to a term of 5 years from single-member constituencies, plus 12 members nominated by political parties on a proportional representation basis. The president appoints the vice president; under the power-sharing agreement, the president with the agreement of the prime minister makes the initial appointment of cabinet members from among those elected to the assembly. Subsequent cabinet appointments are made by the president in consultation with the prime minister, in accord with the power-sharing agreement's proportional division of cabinet positions. The attorney general and the speaker are exofficio members of the National Assembly.‖ [4a] (Government)

Chanzo: https://www.justice.gov/sites/default/files/eoir/legacy/2013/06/12/kenya_1211.pdf
…....
 
Aisee angeshinda Raila, sijui ingekuwaje.
Ikulu za east africa zingekuwa hapatoshi kwa totoz
Zingekuwa zinapigwa threesome za kufa mtu.
Kuna mmoja kapewa uongozi pale uvccm, anatafunwa km njugu, anatembea kila kona ya dunia sasa
Sent From Ikulu-Magogoni street
General Mangi. Tuanze na wewe. Je katika hayo yote uliyasema jui ya Raila,ww hauingii popote ndani sifa hizo? Je,haupendi ndugu zako pale upatapo nafasi hata hapo eneo lako la kazi? Je ukipewa nafasi hata hapo ulipo kikazi haupingi dili zaidi ya mshahara tu? Je, uonapo hao vidosho huwa hauwatamani? Je,we ktk ndoa au uhusiano wa kimapenzi hauna mchepuko???...

Maadam umeyaleta haya hapa jamvini rudi tena kuyajibu haya niliyokuuliza!!!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom