Magufuli ajikosha ajificha kivulini

Magufuli ajikosha ajificha kivulini

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Malenga naanza hima,ukweli kuambiana
Kweli i wazi daima,yapasa kukumbushana
Walo watemi wajanja,kweli wajaribu ficha
Hili mujarabu Dongo,kwako wangu Magufuli

Wengi walishapotea, katika hali ni tata
Tamko hukulitoa ,ya kwamba wao nguchiro
Vitisho kutamalika,watu kutiana hofy
Hili mujarabu dongo,Kwako wangu magufuli

Raia wako kulinda ,ni lako jukumu kuu
Sijifanye hauoni,ya kwamba hofu yatanda
Malenga tunajoficha,Uhuru tushapoteza
Hili mujarabu dongo,kwako wangu Magufuli

Mambosasa telekeza,hio ndio yako nia
Kutafutia sababu, Ya siro Kumtumbua
Wajua kweli i wazi,Wananchi watambu
Hili mujarabu dongo,Kwako wangu Magufuli

Hebu fikiri kwa kina,Mo ye anataka nini
Kosale kuwa tajiri,Uchumi kusimamia
Kama manji mgeuka,Mwamwona adui enu
Hili mujarabu dongo,Kwako wangu Magufuli

Kwa taadhima nasema,wewe ndiye jemadari
Wajibu wo kutulinda,na kutetea salama
kujifanya huusiki,kwa yako mambo makosa
Hili mujarabu dongo, kwako wangu Magufuli

Tambua tunatambua,zako hila twaziona
Wajifanya kuwananga,wawachezesha kamari
Wawagueza kafara,Madaraka kuyalinda
Hili Mujarabu dongo.Kwako wangu Magufuli

Kwa kina utafakari,Taifa ulitakalo
Maanani atazama,zako hila aziona
Atachukua hatua,adabu kukushikisha
Hili mujarabu dongo,kwako wangu Magufuli

Tamati nahitimisha,kweli nimeichokoza
Najua utakereka ,kwa lango dongo la kweli
Hilazo tunazijua,utwatuma vijana
Mamluki kutumia kutenda zako hisa

Mwishoni najisemea,uzalendo jambo gani
Fikiri yalo moyoni ,na hofu zao raia
Yakupasa tafakari,yale yawapendezayo
Hili mujaraby dongo,kwako wangu Magufuli​
 
Walimu wa Arts hamuwezi kupata ajira
Mnatuharibia taifa, mnaichafua nchi
 
Back
Top Bottom