Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

Bila ya kusukumwa na ushabiki wa vyama, kwa mtazamo wangu hivyo si vitendo vya kushabikia. Sioni tafauti na yale yaliyodaiwa kufanywa na Masaburi. Hata kama Mbeya ni ngome ya chama fulani, wafuasi wake hawapaswi kuanzisha vurugu kwa wagombea wa vyama vyengine. Je ikiwa hao waliofanyiwa fujo leo, siku wakija kulipiza kisasi watakapokuwa katika ngome yao, huko si ndio kuhatarisha amani?

Ninamshauri kila mwenye hekima alikemee hili na walio na uwezo wa kulizuwia wafanye hivyo. Pia ninawashashauri wapenda demokrasia wote wasubiri tarehe 25 Oktoba kuonesha hasira na mapenzi yao katika kisanduku cha kura, tujuwe mbovu na mbivu. Tanzania ni yetu sote. Uchaguzi utapita, Tanzania itabaki, na ningependa kuona imebakia Tanzania yenye amani kabla na baada ya uchaguzi.

Nategemea na nasubiri matusi na kejeli za baadhi ya watu, kama yanayoendelea kumkuta Raisi Karume kutoka kwa wanaCCM wenzake kwa kuwaambia waache lugha za matusi.we
 
Hiyo ilikua maeneo ya Soweto siku nyingi wakati akifanya Ziara mkoani mbeya, kwa leo Magufuli alikua sehemu za Iringa, Njombe kwa maana ya Makambako na Mbarali
 
kila chaguzi zinapofika huwa watu hawa wanaandaliwa japo kwetu sisi ni faida kwetu ila kwenu ni sifa pia kuwa mgombea wetu amezowa lakin amin nawaambia magufuli ndo atashinda
 
  • Thanks
Reactions: snn
Hiyo siyo nguvu ya umma ila ni uhuni.

Uhuni mtu yeyote akiamua anaweza kuufaya, lakini matokeo yake ni kuvujika kwa amani.

Kama wao wameshaamua kuwa wanamtaka Lowassa nini kinawapeleka kwenye mkutano wa Magufuli?

Inaonekana kabisa kuwa kuna kundi lililojiandaa kufanya fujo na walishaandaa camera wapige hii picha ya video.

Ukawa badala ya kuchekelea vitu kama hivi inabidi mvikemee kwa sabau watanzania hawapendi vurugu, hawatamchagua mtu anayeandaa vikundi vya vurugu.

siku hizi mikutano inafanyikia barabarani au ndiyo walewale lower thinkers....................???????????????????????
 
Bila ya kusukumwa na ushabiki wa vyama, kwa mtazamo wangu hivyo si vitendo vya kushabikia. Sioni tafauti na yale yaliyodaiwa kufanywa na Masaburi. Hata kama Mbeya ni ngome ya chama fulani, wafuasi wake hawapaswi kuanzisha vurugu kwa wagombea wa vyama vyengine. Je ikiwa hao waliofanyiwa fujo leo, siku wakija kulipiza kisasi watakapokuwa katika ngome yao, huko si ndio kuhatarisha amani?

Ninamshauri kila mwenye hekima alikemee hili na walio na uwezo wa kulizuwia wafanye hivyo. Pia ninawashashauri wapenda demokrasia wote wasubiri tarehe 25 Oktoba kuonesha hasira na mapenzi yao katika kisanduku cha kura, tujuwe mbovu na mbivu. Tanzania ni yetu sote. Uchaguzi utapita, Tanzania itabaki, na ningependa kuona imebakia Tanzania yenye amani kabla na baada ya uchaguzi.

Nategemea na nasubiri matusi na kejeli za baadhi ya watu, kama yanayoendelea kumkuta Raisi Karume kutoka kwa wanaCCM wenzake kwa kuwaambia waache lugha za matusi.we

Labda mie ndo sijui maana ya vurugu! Ina maana walivyoshangilia Yanga juzi, ilikuwa vurugu? Ingelikuwa pana dhamira hiyo ya vurugu, basi mheshimiwa hata kujitokeza asingeshauriwa. Yeye kafungua roof ya gari kuwasalimia watanzania, alichokipata ni wananchi kumwambia kwa kushangilia kile wakipendacho. Unless kama walitumia lugha chafu, ama kumtupia mawe ama chupa, ningesema hii sasa wanastahili adhabu kali. Wote tu watanzania.
 
Hiyo ilikua maeneo ya Soweto siku nyingi wakati akifanya Ziara mkoani mbeya, kwa leo Magufuli alikua sehemu za Iringa, Njombe kwa maana ya Makambako na Mbarali

mkuu hiyo ni uyole na sio Soweto labda kama huijui mbeya.....magufuri alitoka uwanja wa ndege wa songwe mbeya na akawa anaelekea mbarari hadi huko iringa, alipofika hapo uyole ndipo hilo kundi la vijana wakamsimamisha na hawajamzomea bali walikuwa wakiimba lowasa na kuonyesha alama za mabadiliko, hadi aliposema peoples power ndipo wakamwachia na kuendelea na msafara wake
 
Kidonda huanza na kipele. Tusipojihadhari tunaweza kujikuta tunaangukia pabaya. Kumbuka kuwa Watanzania wengi bado hatuna uvumilivu wa kisiasa.
 
Kuhusu clip ya kuzomewa, ni kwamba hawa jamaa zetu wa UKAWA wana siasa za majitaka. Waliandaa kikundi maalum na mpiga picha za mnato na video kwa ajili ya kumzomea Dr. Magufuli. Hata wananchi waliokuwepo walikishangaa kikundi hicho.
 
Hamumtaki leo wakati mlijazana kwa maelfu kumshangilia wakati alipokuja kufanya kampeni.

Mkuu kumbuka waliomshangilia wakati wa kampeni ni watu wa kuja kwa malori na si wakazi wa Mbeya.
 
Kuhusu clip ya kuzomewa, ni kwamba hawa jamaa zetu wa UKAWA wana siasa za majitaka. Waliandaa kikundi maalum na mpiga picha za mnato na video kwa ajili ya kumzomea Dr. Magufuli. Hata wananchi waliokuwepo walikishangaa kikundi hicho.
 
Kuhusu clip ya kuzomewa, ni kwamba hawa jamaa zetu wa UKAWA wana siasa za majitaka. Waliandaa kikundi maalum na mpiga picha za mnato na video kwa ajili ya kumzomea Dr. Magufuli. Hata wananchi waliokuwepo walikishangaa kikundi hicho.
Nani alimwambia asimame pale?ukawa walijuaje atasimama pale na kuandaa kikundi?!??
Yaani ccm bure kabisa akili
 
siasa zao hizo zimeishapitwa na wakati...watanzania tumeishaamua kumchagua Dr Magufuli...
 
hiyo ni kazi ya kitoto maana watu hawa wameandaliwa kuzomea hivyo kwetu wala sio tatzo tunajua muda utafika na ndipo mtakapokuja kujua kuwa magufuli ndio rais wetu
jUKWAA LIMEINGILIWA NA LBA BUKU 7-MASAKI..
akamanda tuwe tayari kupambana nao
.
!
 
Politiziano(politicians), ukisoma ulaya unakumbana na lugha za asili ya kilatini nazo ni kifaransa,Spanish, na kireno,pia kiitaliano. Sasa herufi Z inatamkwa (tz), kumbe ujue mazingira gani ametoka na unaona kabisa ndio bado kuchanganya lugha. Kwa msomi wala hana shida kwani anajua kukosea lugha sio shida kwani lugha nyingi zinakuchanganya katika kuzungumza. Kumbe unapohukumu ujue mazingira ya msomi ndio uhukumu. Se vuoi di imparare diversi lingua è così la vita di cambiamento. Take care.

kweli kujua kwingi huondoa maarifa.We ni mtupu kabisa.

"I am politicians" by Dr.magufili.
 
Back
Top Bottom