Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Leo, naendelea na zile mada zangu fikirishi za KMT, Kwa Maslahi ya Taifa。Somo la leo ni la kitu kinachoitwa “Kibali”。
Kufuatia Watanzania waliowengi hawapendi kusoma vitu virefu,mada hii naileta kwa vipande vipande hadi ikamilike, naanza na Outline
7. Somo la Saba: JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Kilikatishwa kwa Kufutwa Akapewa Samia
Kuhusu Kibali cha Kutawala Tanzania, Rais Samia ana kibali!.
Kwa vile kibali Rais Samia alichoingia nacho hii 2021-2025 ni kibali cha JPM alichonyanganywa akapewa Samia ili kuimalizia ngwe ya Magufuli, sijui kama mtoa vibali anaujua ule utaratibu wa mserereko wa CCM, ndio maana licha ya JPM kuingia kumalizia kipindi chake cha pili kwa mserereko, Mtoa vibali alikifuta kibali cha JPM. Japo lengo la msesereko ni jambo zuri na lengo zuri la kuondoa duplicity kwenye mchakato wa usaili wa ushindani wa wagombea urais ambao walisailiwa ili kumpata the best, Rais Samia yeye hakusailiwa urais kwa ushindani, kwa vile ameupata urais kwa kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu, ni kibali kimemuepushia na ushindani, hivyo 2025 ndiye mgombea wa CCM wa mserereko wa kubembea.
Kwenye mahojiano na Kikeke, aliposema 2025, twende na mwanamke, tumemuunga mkono ila tukamuulizia kuhusu kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Sasa sijui kama kwa vile ni mimi ndie niliulizia kuhusu kibali cha Rais Samia 2025-2030, then ni mimi ndiye niliye ambiwa kitu kuhusu HII issue ya 2025, wakati muafaka ukiwadia, na yeye mhusika mwenyewe ataambiwa na mtoa vibali.
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni sana!.
Paskali
Leo, naendelea na zile mada zangu fikirishi za KMT, Kwa Maslahi ya Taifa。Somo la leo ni la kitu kinachoitwa “Kibali”。
Kufuatia Watanzania waliowengi hawapendi kusoma vitu virefu,mada hii naileta kwa vipande vipande hadi ikamilike, naanza na Outline
- Kibali ni nini?
- Kibali ni cha kazi gani?
- Sifa za Kibali: Kikitumika Kinakamilika, Kisipotumika, Kinafutwa!
- Kibali Kinatolewa na nani?
- Kibali Kinatolewa kwa nani?
- Anyepewa Kibali Anajua Kuwa ana Kibali?.
- Utamjuaje Mtu Mwenye Kibali?
- Nyerere, Mwinyi na Mkapa, Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.
- JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Hakikukamilika, Kilifutwa.
- Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
- Tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu ili kisifutwe? au tumuachie mwenyewe?
- Hitimisho na A Way Foward 2025
2. Somo la Pili: Kibali ni cha kazi gani?Kibali ni ruhusa ya kufanya japo fulani,ambalo ili ulifanye ni lazima upate kibali au ruhusa kutoka mamlaka husika。Kibali cha kikuu cha kwanza kwa binadamu baada ya kuumbwa ni kibali cha uhai,kibali cha kuishi na kibali cha kuumba binadamu wengine。Baada ya hapo ni kibali cha kufanya kila kinachofanyika。Kibali kwa mwanamke kuwa mama na mwanaume kuwa baba,ni kupevuka,kibali cha kujenga familia ni kuoa,kibali cha kujenga nyumba ni kumiliki ardhi,kibali cha kufanya biashara ni kuwa na leseni,kibali cha kusafiri nje ni kuwa na passport,kibali cha kuingia nchi fulani ni kuwa na visa, hivyo vibali viko vya aina nyingi。
Kibali ninacho kizungumza kwenye uzi huu ni kibali cha kutawala nchi,kuwa mkuu wa nchi。
3. Somo la Tatu: Kibali Kinatolewa na Nani?Kibali ni cha kutimiza lile jukumu la kibali ulichopewa,kama tulivyoona kwenye somo la kwanza, kuna vibali tofauti vya kufanya mambo tofauti tofaouti, ukipewa kibali cha ndoa,inatimiza majukumu ya ndoa,ukipewa kibali cha kufanya biashara,unafanya biashara kwa mujibu wa leseni yako。
Kuna vibali vingi,hadi vibali vya kuua,licence to kill,hata mtu anayehukumiwa kunyongwa,hukumu hiyo haitekelezwi hadi mkuu wa nchi asaini death warrant ndipo anyongwe
Hivyo hata kibali cha kutawala nchi,unatawala kwa mujibu wa kibali chako
japo kibali cha kutawala nchi kimetolewa kwa mujibu wa katiba,anayepewa kibali hicho anapewa na YEYE na anapaswa sio tuu kufuata katiba,bali pia kutimiza madhumuni ya YEYE alIyempa kibali hicho,alimdhamiria afanye nini,kibali chake ni cha nini na kwanini ni yeye na sio mtu mwingine yeyote?
Sifa za Kibali: Kikitumika Kinakamilika, Kisipotumika, Kinafutwa!
Kama nilivyoeleza, kibali kinatolewa kwa madhumuni kusudiwa, au kuna vibali vya kazi maalum, task force, ukiisha ikamilisha kazi, unakuwa rewarded accordingly, kibali kimekamilika na kazi ya kibali hicho inakuwa imekwisha.
Musa kibali chake kilikuwa ni kuwakomboa tuu wana wa Israel kutoka utumwani Misri, alipokamilisha kazi ya kuwaondoa na kuwasafirisha mpaka nchi ya ahadi, kibali chake kikakamika, yeye hakuingia nchi ya ahadi, alitwaliwa, na kibali cha kuwaingiza nchi ya ahadi, kikatolewa kwa mtu mwingine.
Kwa vile kibali, ni kibali cha kazi maalum kwa mtu maalum, ukiwa ni mtu mwenye kibali, usipokitumia kibali hicho kikamilifu, kibali hicho kinafutwa!.
Ufutaji wa vibali au ufutwaji wa vibali, hufanyika kwa namna mbili
1. Ufutwaji wa uwezo wako, kufutwa, mtu alikuwa mfanyabiashara mkubwa maarufu na tajiri, anafilisika hadi kubaki apeche alolo!. Mtu alikuwa msanii mzuri, mwanamuzi mzuri, mchezaji mzuri, ghafla uwezo wake unashuka, anajikuta anatupwa nje ya gemu.
2. Ufutwaji wa kibali wa aina ya pili ni kwa wewe kufutwa kwenye uso wa dunia, kwa kutwaliwa!, kama inavyotokea kwa wengi wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana. Musa, Kanumba, Sembuli, Mbaraka Mwishehe, Shaaban Robert, John F Kennedy, Bruce Lee, JPM na wengine wengi, wameitwa kurejea kwa Muumba wao.
4. Somo la Nne: Kibali Kinatolewa kwa Nani?Kama tulivyoona kwenye somo la kwanza la kibali ni nini, kuna aina nyingi za vibali, somo la pili kibali ni cha nini, tumeona vibali vya kufanya shughuli tofauti tofauti, sasa ni vibali hivi vinatolewa na nani. Vibali vinatolewa na mamlaka husika, kutegemeana na ni kibali cha nini, na cha aina gani, nimesema kuna two types ya vibali, vibali za shughuli za kidunia, vinatolewa na mamlaka za kidunia, na vibali vya mambo makuu, vinatolewa na mamlaka Kuu ambayo ni Mungu, YEYE Mwenyewe, unakuwa umepata kibali machoni mwake.
Vibali vya YEYE mwenyewe, mtu hauombi, anazaliwa nacho, ama unapewa na YEYE mwenyewe kwa madhumuni mahsusi.
Mfano urais wa nchi hupatikana kwa kuomba kuteuliwa, waombaji wanakuwa ni wengi, anayepata ni mmoja, huyo mmoja anayefanikiwa kupata, anakuwa ndie mwenye kibali kutoka kwa YEYE. Mungu anakuwa na madhumini fulani, kwanini amempa kibali huyo aliyempa. kati ya wagombea wote wanaogombea, mwenye kibali anaitwa "the chosen one", mfano mzuri ni uchaguzi wa 2015, watu walimshobokea sana Lowassa, mimi nikiwemo, tofauti na wengi, pia nikawaandaa watu kisaikolojia Elections 2015 - Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015, Rais wetu wa 2015 ni..., hivyo JPM ndie was the chosen one mwenye kibali cha urais 2015-2020.
5. Somo la Tano: Anyepewa Kibali Anajua Kuwa Ana Kibali?. Utamjuaje Mtu mwenye Kibali?.Kwa vile kibali kinatolewa na YEYE Mungu mwenyewe, kinatolewa kwa aliyemchagua YEYE, au aliyemteua yeye.
Mfano wa Familia.
Mara nyingi kwenye familia zetu, Baba ndio huhesabika ni kichwa cha familia, tangu Mungu alipomuumba Adam, akampa kibali cha kutawala viumbe wote wa dunia hii. ila katika mambo ya tamaa za mwili, mke ndie amepewa kibali!, Eva baada ya kufundishwa na shetani jinsi tunda linavyomegwa, akaonjeshwa kwa kumegewa, kisha Eva na shetani wakamega tunda, wakala, Eva akauona utamu wa tunda, alipewa kibali cha tamaa za mwili, akamfua Adam, akamfundisha jinsi tunda linavyomegwa, japo Adamu mwanzo alikataa, kwa vile Eva ndio amepewa kibali hicho, Eva alimlaziisha Adam kumega tunda, wakamega tunda, wakala na kuishia zao usingizini. Hivyo Mwanamke nae ana kibali cha baadhi ya mambo, na ndio maana baadhi ya makabila haswa ya wafugaji, wanai katilia ile kitu, inayoweza kumpa mwanamke tamaa ya kumegwa tunda!.
Japo baba ndio anapaswa kuwa kichwa cha familia, kuna familia nyingi, mama ndio anakuwa amepewa kibali, hivyo ndie kichwa cha familia.
Familia nyingi pia huwa zinapenda mtoto wa kwanza awe mwanaume ili apewe kibali cha mzaliwa wa kwanza, lakini kuna familia nyingi, mzaliwa wa kwanza ni mtoto wa kike, hivyo anapata kibali cha uzaliwa wa kwanza.
Kwa vile kibali kinatolewa na Mungu mwenyewe, sio lazima mzaliwa wa kwanza, apate kibali, Mungu anaweza kumteua mtoto yoyote na kumpa kibali. Mfano japo mzaliwa wa kwanza wa Nabii Ibrahim ni Ismail, aliyepewa kibali ni mzaliwa wa pili Isaka. Na kwa Yakobo, japo mzaliwa wa kwanza ni Essau, aliyepata kibali ni Yakobo. Yakobo yeye alipata watoto 12, mtoto mwenye kibali ni Yusufu, mzaliwa wa 11. Na Daudi katika familia ya Yese ndie alipewa kibali.
Hivyo kibali kinaweza kutolewa kwa yeyote, anayeamua nani apewe kibali ni YEYE .
Hata kwenye imani zetu za kiasili, watoto wanakuwa na vipawa mbalimbali, anayechaguliwa kuridhi mikoba, anaweza kuwa ni mtoto wa mwisho. Hicho ndio kibali.
Somo la Sita: Nyerere, Mwinyi na Mkapa, JK Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.Hii ndio the trickiest part ya vibali. Je mtu mwenye kibali hujijua kuwa ana kibali?.
Kwa vile kibali hutoka kwa Mungu, na humpa amtakae au ampendae, hivyo kwanza ni Mungu mwenyewe ndio hutoa taarifa za baadhi ya vibali. Adam alizungumza na Mungu na kupokea kibali chake direct, Mungu huzungumza kwa njia za ndoto, maono, sauti, au kunena kwa vinywa vya manabii au kutumia malaika wake kuhusu vibali mbalimbali ambavyo kwa kawaida mtu huzaliwa navyo ama hupewa.
Kibali cha Musa, kabla hajazaliwa Farao alitoa amri watoto wote wa kiume wanaozaliwa na Waebrania, hivyo Musa alipozaliwa ni malaika walisimamia atupwe mtoni, mara aokotwe na binti Farao, Binti Farao akakilea kichanga kama mtoto wake!.
Kibali cha kuzaliwa Isaka kililetwa nyumbani kwa Nabii Ibrahim na malaika watatu walio jigeuza wageni.
Kibali cha kuzaliwa Yesu kililetwa na Roho Mtakatifu, kumpachika Bikira Maria ujauzito bila 'tunda' lake kumegwa!. Mumewe Yosefu baada ya kuona mkewe ni mjamzito huku wakiwa bila bila, akapanga kulala mbele, ndipo Mungu akamtokea kwenye ndoto kumtuliza kuwa ni mpango wa Mungu!, ndipo akatulia.
Kuna watu wengi wana vibali tofauti tofauti, lakini hawajui kuwa wana vibali hivyo kwasababu hakuna yeyote aliyewaambia kuwa una kibali fulani au kuona dalili zozote za vibali. Mimi kupitia kusoma vitabu nimewahi kujitahidi kuwafungua baadhi ya watu macho ya kujitambua vibali vyao Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo? na kwa vile mimi ni mtangazaji, nikajitolea kuwasaidia kujitambua, wale wenye vibali vya utangazaji Je, Una Kipaji cha Utangazaji? Jinsi ya Kujiajiri Utayarishaji na Utangazaji Vipindi Vyako vya TV
Hivyo hata katika uongozi, tuna viongozi wengi sio viongozi wa wito, vipawa, karama wala uwezo, ni matutusa tuu, hawana vipawa vya uongozi, karama zozote, vipaji vya uongozi na uwezo wa uongozi, lakini wanapata uongozi wa umma kwa kutumia "the universal power".
Kuna watoto wengi wanazaliwa vibali, wazazi wao hawana uwezo wa kuwabaini mapema, hivyo mwisho wa siku vibali vyao vinavutwa!. Kuna watoto wanazaliwa na vipaji fulani, bila wazazi wao kuwabaini na kuwaendeleza, vipaji hivyo vinakufa. Kuna watoto wanazaliwa na uwezo Kiislamu wanaitwa ma Sharufu, usipowabaini, uwezo wao unapotea.
Kwa vile mtoa kibali ni Mungu, yeye Mungu huwaeleza wenye vibali vyao, kuwa wana vibali, na sometimes, huwatumia watu baki kuwaeleza kuhusu vibali fulani, hao wanaotumwa ni manabii, wakisikilizwa, vibali vinatumika, wasiposikilizwa, vibali vinafutwa!.
Namna ya mtu wa kawaida kuwatambua wenye vibali, ni jinsi tuu mambo yao, yavyowanyookea. Kwa chicho la kawaida wanaonekana ni watu wenye bahati, wana ngekewa, wanafanikiwa, kumbe hicho ni kibali.
Watu wote wenye mafanikio yanayotokana na vipaji mbalimbali ni watu wenye vibali. Wafanyabiashara, wanamuzi, na wasanii wenye vipaji vikubwa, wenye vibali wanafanikiwa, na kuna watu huku mitaani, wana vipaji vya ajabu sana, lakini hawana vibali, hivyo hawatusui!.
JK Nyerere Alikuwa na kibali toka anazaliwa!, kuna mambo ya kuzaliwa kwa Nyerere naomba tuyaache yabaki kama ni siri za familia yake tuu, lakini hivyo ndivyo mambo ya vibali yanavyokuwa. Kibali chake kilianza kuonekana alipokuwa Tabora School Usiyoyajua Kuhusu Nyerere: Shuleni Alikuwa Toto Tundu!, Almanusura Afukuzwe Tabora School!
Kibali chake kilikuwa ni kutupatia uhuru, hiki kilikamilika, kufuta ukabila na kutujengea umoja, hili lilikamilika. Mwalimu alipaswa kuongoza taifa hili kwa miaka 10 tuu, 1961-1971, kisha aingie mtawala wa kuleta maendeleo.
Kwa vile kibali chake ilikuwa ni kuleta uhuru na umoja, kibali cha mwalimu kilikwisha, alipoendelea, badala ya kupata mafanikio ndipo yakafuata majanga ya vita, kuanguka kwa uchumi, hivyo ni mwaka 1985 akakubali kuwa alifanya makosa, akawaomba msamaha Watanzania kuwa kufanya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa, Japo Watanzania tulimsamehe, na akastaafu kwa amani, ila kuna issues zake nyingine ambazo public hatuzijui, zilizopolelekea kuitwa kwa jinsi ile alivyoitwa. Mchakato wa kumtangaza Mwenye Heri unaendelea, ili mwisho wa siku aje kutangazwa ni mtakatifu, unaendelea.
Ali Hassan Mwinyi Alikuwa na Kibali.
Aliyempokea Mwalimu Nyerere ni Rais Ali Hassan Mwinyi, aliyezaliwa Mkuranga kwa wazazi wote wawili wa Bara, akaenda Zanzibar akalowea, kibali chake kilithibitika licha ya kujiuzuli kwa kashfa, akiwa waziri wa mambo ya ndani, aliukwaa urais wa Zanzibar huku akiwa sio Mzanzibari wa kuzaliwa, na baadae kuwa rais wa JMT. Hayo ndio mambo ya vibali. Yeye alimaliza vizuri kwa kukitumia vizuri kibali chake, Mungu akampa umri mrefu na heri duniani, amakufa na umri wa zaidi ya miaka 100!.
Benjamin William Mkapa Alikuwa na Kibali.
Mwinyi alifuatiwa na Benjamin William Mkapa, huyu kibali chake kilionekane toka alipozaliwa huko aliko zaliwa , Mama ni Mtanzania na jina la Mkapa ni la kikeni. Zile issues za Mchungaji Mtikila kumhusu Ben, japo wengi wanamuona Mtikila kama alikuwa kama kichaa fulani, ila kiukweli alikuwa na hoja, na hayo ndio mambo ya kibali hicho ndicho kilichomsimamia yote mpaka kuwa rais wa JMT.
Alimaliza salama kwa kukamilisha kibali chake, ila na yeye alikuwa na issues zake binafsi na Mungu wake zilizopelekea kuitwa kwa jinsi ile alivyoitwa. Nilimtengenezea kipindi
View: https://youtu.be/DUOg28gosy8?si=QLzc-SZb6xRbQTcD
Jakaya Mrisho Kikwete Alikuwa na Kibali
JK pia alikuwa na kibali, haijalishi kuhusu sarakasi zote zilizopigwa hadi JK kutinga Ikulu, ikiwemo mtu kuchomolewa, mtandao kuasisiwa, timu ya Boys II Men kuundwa, EPA kutumika, na rise of King Maker, etc, ile mtu tuu kutinga Ikulu, hilo peke ni kibali tosha. Kumhusu JK niliandika humu kuhusu mapungufu yake Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim! na sifa zake njema Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour" Alikitumia kibali chake to the fullest na mpaka sasa anadunda.
7. Somo la Saba: JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Kilikatishwa kwa Kufutwa Akapewa Samia
8. Somo la Nane: Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajitambua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?Rais JPM, pia alikuwa na kibali, ila kibali chake sina uhakika kama kilikuwa ni kibali kifupi cha miaka 5 tuu, hivyo JPM alikitumia kibali chake hadi mwisho, lakini alipoamua kujiongeza kwa kuufuata mtindo wa mserereko wa CCM, kibali hicho kikaondoshwa, au pia kibali chake kilikuwa ni kibali cha miaka 10, lakini hapa katikati akatofautiana kitu na mtoa vibali, mtoa vibali akaamua kukikatisha kibali cha JPM, na kumpa Rais Samia Kibali.
JPM ana kibali, infact alizaliwa na kibali huko alikozaliwa, makuzi na mapito yake yote ni uthibitisho wa kibali. Kabla hata yeye mwenyewe hajagombea, watu humu tulishikwa sikio tukaambiwa ni JPM Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Muda wa kuchukua fomu, walijitokeza wana CCM, 62!. Kati ya hao 62, kuna watu wazuri kuliko JPM, lakini kwasababu JPM ndio alikuwa na kibali, ni JPM aliyeshinda, tukamshauri mtu wetu Elections 2015 - Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!
Alipoanza, nilisema humu, Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! na tukashauri Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! hii maana yake usikute kibali chake kilikuwa ni kuinyoosha tuu nchi na kujenga mabarabara. na baada ya miaka yake 5, apumzike, watu wa kushauri tulishauri Magufuli, "Kama Unaona Kazi ya Urais ni Ngumu Kwako, Jiuzulu! ".
Kwa vile Samia alikuwa ni msaidizi wake, sisi watu wa kudurusu, tukamdurusu Samia, tukamuona ana uwezo, tukamshauri JPM term yake ya pili ampishe Samia Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020
Pia tulitoa angalizo muhimu Elections 2015 - Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake! Alipoamua kundelea na term yake ya pili, ndio mambo yakawa kama vile, sijui ni kibali kilifutwa au!,
Nilisema mtu ukiwa na kibali ni lazima ujitambue kwanza kwa kujua kuwa una kibali, ujue ni kibali kufanya nini, na ni cha muda gani, then kitumikie kibali chako, kwa mujibu wa kibali chako na muda wako ukiisha pisha wengine, maisha yaendelee.
Miongoni mwa vitu vinavyosabisha kufutwa kwa vibali ni ukosefu wa haki kwenye demokrasia yetu na umwagikwaji wa machozi, jasho na damu zisizo na hatia, zinazopekekea kitu kinachoitwa a bad karma hivyo tulipopata fursa ya kukutana nae, tulimkabili Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
JPM alikuja kubadilika na tukampa big up
Mwishoni akabadilika, akaanza kuwa mtu mwema na kutenda matendo ya huruma
- Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana!
- Kiukweli nimeguswa sana na uchapakazi wa Rais Magufuli!. Je, kuna uhusiano kati ya kabila la mtu, na uchapakazi wake?. Je, 2020 kuna haja ya...
- Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
- Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever had. Msikivu, ana upendo na huruma. Atabarikiwa sana. Tanzania itabarikiwa!
- "Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa!
- Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani. Je, Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika
- Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere!
- Pongezi Rais Magufuli. Ameonesha uzalendo wa hali ya juu uliotukuka!, amebadilika, amejishusha, uchumi wa Tz kupaa!
Mwisho wa siku, nikaelezwa sasa yuko zake Mbinguni Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
Naombeni tumwacheni huyu baba apumzike.
Somo la Tisa: Tumsaidie ili atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu au Tumuachie Mwenyewe na Kibali Chake?Mtu wetu wa sasa ni Rais Samia.
Hoja ya kwanza ya Rais Samia, je ni Kibali?.
Jibu ni ndio, Rais Samia ni kibali, mapito yake toka alipoanza mpaka hapa alipofikia, kote kuna viashiria vyote kuwa huyu ni kibali.
Kwa vile siku hizi, kumeibuka fani ya uchawa, na watu wanaitwa machawa, hivyo ukimsifu Rais Samia kwa lolote, unaitwa chawa!, mimi mwenzenu 60 inabisha hodi, kwa umri huu kuitwa chawa sio kunitendea, naomba nikupitishe kidogo uone Samia, nilianza nae lini na nilisema nini,
Samia nilianza nae 2010 kwenye uzi huu New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa! nikaja Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material? kisha nikaja
"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Wanabodi, Niko kwenye voluntariy lockdown, hivyo leo nimepata fursa ya kuangalia TV ya Zanzibar, ZBC, Mwandishi wa habari wa CCM Zanzibar, Daudi Ismail anamhoji Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku...www.jamiiforums.com
Hivyo mtu kuniita mimi ni chawa kwa kumzungumzia Rais Samia kwasababu sasa ni rais, ni kunionea bure!
Kwa vile Rais Samia ameupata urais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeezi Mungu, ili kutokea jambo kama lile kisha mtu kuukwaa urais bila kutegemea ni ishara tosha ya kuthibitisha kuwa hicho ni kibali tosha. Kama nilivyoeleza huko nyuma, aliyempa kibali, anaweza kuwa amemweleza kwanini amekifuta kibali cha mtangulizi wake, hivyo yeye anatakiwa kufanya nini kurekebisha makosa ya mtangulizi wake ambaye time frame ya kibali chake mwisho ni 2025.
Sisi Watanzania, wengi wetu ni ma simple mind, they don't have time to think, kazi yao kubwa is to discuss people, wanaofuatia ni ordinary minds, they discuss events, wachache ni great minds ambao wana discuss ideas, humu tunawaita ni ma GT, na miongoni mwa hao ma GT, wamo ma deep thinkers, mmoja wa deep thinkers hawa ni Balozi Humphrey Polepole, huyu ndie pekee aliwahi kukifafanua kibali cha Rais Samia aliposema Rais Samia, ni rais wa 6, ila anamalizia kwanza awamu ya 5 ya JPM, kisha ndipo aanze awamu yake 2025, ila kwa vile ameipokea ndani ya mwaka mmoja, hii inahesabika ni awamu ya 6, lakini ilani ni ile ile ya awamu ya 5.
Hivyo Rais Samia alipoanza, alianza vizuri kwa kuyarekebisha makosa ya mtangulizi wake, tulimpongeza, sana tuu kwa kumwandikia humu, mitandaoni, magazetini na kwenye vipindi vyetu vya Redio na TV, our expectations of her, we had very high expectations, alipokuja na zile 4R, akaunda kikosi kazi, akaja na haki jinai, maridhiano, akafutia watu kesi, kwenye haya, nyonge mnyongeni haki yake mpeni, Rais Samia anastahili kupewa maua yake.
Licha ya pongezi, karibu kwenye kila pongezi, pia kulikuwa na maombi fulani, mengine yametekelezwa na mengine bado. Haya ni baadhi ya maombi mahsus kwake
- Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri
- Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Pongezi Rais Samia kwa Kutuhisania Openness and Transparency Kwenye Uteuzi, Mnaonaje Ifanyike Kwenye Utenguzi na UtumbuzI Iwe ni Haki na Sio Hisani?
- Kwa “nonsense” ya Sukari, Rais Samia anastahili pongezi. Je, tuishie kwenye "nonsense" ya Sukari tu au tuangazie na "nonsense" nyingine zote?
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Rais Samia ni msikivu, apewe maua yake. Vipi Serikali yake, Bunge na mahakama ni wasikivu? Kama sio inamanisha
- Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
- Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
- Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
- Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria!
- Ombi kwa Rais Samia: Sheria Mpya ya Uchaguzi Bado ina Ubatili. Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa imeporwa! Irejeshwe kwa Mujibu wa Katiba!
- Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti
10 Somo la Kumi: Hitimisho na A Way Forward 2025Japo kibali, kinatolewa na Mungu mwenyewe, na kila anayepewa kibali, pia anapewa uwezo wa kutekeleza mahitaji ya kibali chake, lakini binadamu ni kiumbe dhaifu, hakuna mkamilifu hivyo kunaweza kutokea makosa ya hapa na pale, na hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu yeye mwenyewe, ni lazima asaidiwe, ndio maana japo Rais wetu ana kibali lakini ana wasaidizi wa kumsaidia kwenye kila eneo, na bado kunatokea makosa ya hapa na pale Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
Hivyo pamoja na uwepo wa wasaidizi wa kutosha ambao ni manguli, wazoefu, wabobezi na wabebovu, lakini bado makosa yanafanyika. Na kuna watu huku mtaani, sio wabobezi, sio wabebovu lakini wana uwezo wa kusaidia. ndipo nikauliza, unapoona Rais Samia na serikali yake, imeshindwa jambo fulani na wewe umeona unaweza kusaidia, jee tumsaidie au kwa vile yeye ndie mwenye kibali, then tumuachie mwenyewe na kibali chake? WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?
Pia hapa Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
Niliuliza humu Kumuenzi Magufuli: Tujikumbushe 'spana' za JF zilivyomsaidia Hayati Magufuli na Taifa. Je, Samia pia tumsaidie kwa 'spana' au tumkune tu tusimpare?
Pia nilishauri Tanzania tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!
Tuwakumbushe wasaidizi wake kutimiza wajibu wao kikamilifu Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?
Pia niliuliza Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
Nimeendelea kusisitiza Rais Samia asaidiwe Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!
Na sio tuu, tunamsaidia Rais Samia kama rais wetu, bali pia tunawasaidia wale anaopaswa kufanyanao kazi ili wasipishane Tujikumbushe Kauli hii ya Rais Samia Atafanya Kazi na TLS ya Aina Gani? Hizi ni Salaam kwa Mwabu,. Swali ni is He A Bow Down Type or a Stand Firm?.
Mimi kwa upande wangu, nina maeneo mawili ya kusaidia, eneo la habari, na eneo la haki Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten
Kuhusu Kibali cha Kutawala Tanzania, Rais Samia ana kibali!.
Kwa vile kibali Rais Samia alichoingia nacho hii 2021-2025 ni kibali cha JPM alichonyanganywa akapewa Samia ili kuimalizia ngwe ya Magufuli, sijui kama mtoa vibali anaujua ule utaratibu wa mserereko wa CCM, ndio maana licha ya JPM kuingia kumalizia kipindi chake cha pili kwa mserereko, Mtoa vibali alikifuta kibali cha JPM. Japo lengo la msesereko ni jambo zuri na lengo zuri la kuondoa duplicity kwenye mchakato wa usaili wa ushindani wa wagombea urais ambao walisailiwa ili kumpata the best, Rais Samia yeye hakusailiwa urais kwa ushindani, kwa vile ameupata urais kwa kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu, ni kibali kimemuepushia na ushindani, hivyo 2025 ndiye mgombea wa CCM wa mserereko wa kubembea.
Kwenye mahojiano na Kikeke, aliposema 2025, twende na mwanamke, tumemuunga mkono ila tukamuulizia kuhusu kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Sasa sijui kama kwa vile ni mimi ndie niliulizia kuhusu kibali cha Rais Samia 2025-2030, then ni mimi ndiye niliye ambiwa kitu kuhusu HII issue ya 2025, wakati muafaka ukiwadia, na yeye mhusika mwenyewe ataambiwa na mtoa vibali.
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni sana!.
Paskali