Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Leo, naendelea na zile mada zangu fikirishi za KMT, Kwa Maslahi ya Taifa。Somo la leo ni la kitu kinachoitwa “Kibali”。
Kufuatia Watanzania waliowengi hawapendi kusoma vitu virefu,mada hii naileta kwa vipande vipande hadi ikamilike, naanza na Outline
  1. Kibali ni nini?
  2. Kibali ni cha kazi gani?
  3. Sifa za Kibali: Kikitumika Kinakamilika, Kisipotumika, Kinafutwa!
  4. Kibali Kinatolewa na nani?
  5. Kibali Kinatolewa kwa nani?
  6. Anyepewa Kibali Anajua Kuwa ana Kibali?.
  7. Utamjuaje Mtu Mwenye Kibali?
  8. Nyerere, Mwinyi na Mkapa, Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.
  9. JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Hakikukamilika, Kilifutwa.
  10. Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
  11. Tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu ili kisifutwe? au tumuachie mwenyewe?
  12. Hitimisho na A Way Foward 2025
1. Somo la Kwanza: Kibali ni nini?
2. Somo la Pili: Kibali ni cha kazi gani?
3. Somo la Tatu: Kibali Kinatolewa na Nani?
4. Somo la Nne: Kibali Kinatolewa kwa Nani?
5. Somo la Tano: Anyepewa Kibali Anajua Kuwa Ana Kibali?. Utamjuaje Mtu mwenye Kibali?.
Somo la Sita: Nyerere, Mwinyi na Mkapa, JK Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.
7. Somo la Saba: JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Kilikatishwa kwa Kufutwa Akapewa Samia
8. Somo la Nane: Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajitambua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
Somo la Tisa: Tumsaidie ili atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu au Tumuachie Mwenyewe na Kibali Chake?
10 Somo la Kumi: Hitimisho na A Way Forward 2025
Kuhusu Kibali cha Kutawala Tanzania, Rais Samia ana kibali!.
Kwa vile kibali Rais Samia alichoingia nacho hii 2021-2025 ni kibali cha JPM alichonyanganywa akapewa Samia ili kuimalizia ngwe ya Magufuli, sijui kama mtoa vibali anaujua ule utaratibu wa mserereko wa CCM, ndio maana licha ya JPM kuingia kumalizia kipindi chake cha pili kwa mserereko, Mtoa vibali alikifuta kibali cha JPM. Japo lengo la msesereko ni jambo zuri na lengo zuri la kuondoa duplicity kwenye mchakato wa usaili wa ushindani wa wagombea urais ambao walisailiwa ili kumpata the best, Rais Samia yeye hakusailiwa urais kwa ushindani, kwa vile ameupata urais kwa kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu, ni kibali kimemuepushia na ushindani, hivyo 2025 ndiye mgombea wa CCM wa mserereko wa kubembea.

Kwenye mahojiano na Kikeke, aliposema 2025, twende na mwanamke, tumemuunga mkono ila tukamuulizia kuhusu kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Sasa sijui kama kwa vile ni mimi ndie niliulizia kuhusu kibali cha Rais Samia 2025-2030, then ni mimi ndiye niliye ambiwa kitu kuhusu HII issue ya 2025, wakati muafaka ukiwadia, na yeye mhusika mwenyewe ataambiwa na mtoa vibali.

Mungu Ibariki Tanzania.

Asanteni sana!.

Paskali
 
Akiwaendekeza machawa kibali kitafutwa

Uchawa ni zao la unyumbu wa kisiasa. Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana, kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kijipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi bila utii, (unafiki), tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo, a.k.a kujizima data.
 
Magufuli alikuwa na kibali.

Shida ya watu wenye vibali ni kulewa na mafanikio yao (Magufuli sio wa kwanza mifano ni mingi kwenye historia).

Wakishafanikiwa sana udhani wana mamlaka ya mungu, kuwaamulia watu wengine maamuzi ya maisha.

Hapo ndio mungu anapojibu, huna mamlaka yangu.
 
Ingekuwa vizuri kama ungejibu maswali yako ili kuwapa wachangiaji ufafanuzi, maana na maudhui ya ulichomaanisha. Je rais ni kabali cha nini? Ni kibali cha ufisadi, uongozi bora, ufamilia, bora uongozi, uadilifu, mamlaka nk? Je ni kibali kilichomo kwenye katiba au cha kujitengenezea? Je kibali hiki kinatumika wapi na kwa muda gani? Je nani anatoa hiki kibali na kwa sifa zipi? Je kama rais ni kibali na kibali ni rais au ni nini? Je sifa za kibali ni zipi na kwa vigezo vipi? Naona nisiteke uzi wako mwanangu, ila kuna mengi yanapwaya kama siyo. kukosekana kabisa.
 
Jiwe hakuwa na kibali,kama angekuwa na kibali ni kwanini aliiba uchaguzi.
 
Naona P.. umeanza kujitambua,
Pambana kivingine
Lakini sahau vyeo huko ccm
 
Aachwe tu
 
Karibu sana Paschal tulishaanza kukutafuta huko twitter
 
Kibali kimeshafutwa huwezi apa kwa Mungu kuilinda katiba alafu baada ya muda mfupi ukaanza pelekeshwa na madalali wa mafisadi ili kulinda maslahi yao tu. Badala ya nchi
 
Kwa hali ilivyo ni busara tumuachie mwenyewe.
 
What you are doing here is treason. Watch your steps.
 
Magufuli hakuwa na kibali, kwa kuwa hata uchaguzi hakushinda
 
No 7
Hana kibali, siyo cha watanzania tu hata juuu
 
Mungu siyo mungu please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…