Wakuu Magufuli alikuwa Rais hadi umauti ulipomkuta Samia akashika uraisi kwa ile miaka 5 iliyobaki na je kama alimalizia ile miaka 5 ya Magufuli.
Si bado miaka kumi tena ya kwake kwa manaa ile mitano alisukuma durumu na haikuwa miaka yake kama raisi wa Tanzania naomba Muongozo
Katiba inasema kwa muda alioshika urais Samia anahesabika kuwa ile ilikuwa term yake ya urais ya kwanza, akiweza kuchaguliwa tena 2025 atamalizia term ya pili ya urais kutoka 2025 mpaka 2030.
Na 2030 kama yupo bado huo ndio utakuwa mwaka wake wa mwisho kuwa rais.
Hili jambo ni kwa nujibu wa katiba, soma katiba ya Tanzania ibara ya urais, mtu anavyopata urais na ukomo wa urais.
Hili ni suala ambalo lipo kwenye katiba.
Soma katiba ibara ya 40 (4)
"4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa
mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua
miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au
zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu."
Samia kashika urais kwa mujibu wa ibara ya 37(5) (rais kufariki) kwa zaidi ya miaka mitatu. Hivyo ataruhusiwa kugonbea urais mara moja tu.
37(5) hii hapa.
"(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais
kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais
ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi
cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka
Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na
uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote."