Magufuli alikuwa Sahihi Kukomesha Cartels wa TFF

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Kulipita andiko kama hili bila kuli-share huku,nitakuwa sijaitendea haki akili yangu!

Nakupa hongera
Yericko Nyerere!
Ila nakukumbusha kwamba,sasa uanze kuelewa usahihi wa Magufuli kwa ule Udikteta wake,juu ya Cartel's wa wizi kupitia sekta ya soka nchi hii.aliona mbali zaidi.
Ambapo na wewe leo ndio unapaona!
Eid kareem!
[emoji116]
SIMBA IMEZULUMIWA KWENYE MGAO "YERICKO NYERERE"
"Ameandika Mwanaharakati Yericko Nyerere [emoji3578]".

"Hii haikubaliki kabisa, mgawanyo huu wa mapato ni wizi wa mchana kweupe. Klabu mwenyeji wa mchezo haiwezekani ipate karibu chini ya 30% ya mapato. Hebu fikiria, Mchezo wa Simba vs Yanga wa jumapili 16/4/2023, kwa mujibu wa TFF uliingiza TSH. Million 410,645 000 halafu Klabu mwenyeji wa mchezo Simba kuambulia milion 188,898,504 tu.

Ukisoma kinachoitwa ni Mchanganuo wa Pesa ulivyo utaona ni wizi mtupu, Mfano; VAT ambayo kisheria ni 18% ambapo kwa TFF wamesema ni mil 62,640,762, inautata maana kisheria 18% hukatwa baada ya kutoa gharama uendeshaji, Tuwahoji TFF hii pesa waliyokata ni baada ya kutoa gharama za uendeshaji?. Sasa tuje, BMT imechukua million 10, 440,127. Hatujaambiwa kwa sheria ipi au kwa kanuni ipi ili tui challenge hiyo kanuni. Kisha tunaambiwa Uwanja wa Mkapa wao wamechukua million- 47,246,795. Bila kusema ni kwa kanuni ipi na wanatafsiri ipi kati BMT na Uwanja

Kisha tunaambiwa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limechukua million -12,599,145, Bila kuambiwa wamechukua kwa kanuni ipi inayowaelekeza kuchukua kiasia hicho. Halafu chombo cha TFF yaani mkono wa kulia wa TFF unaoitwa Bodi ya Ligi ukachota milioni 25,198,290. Sasa hapa unatofautishaje kati ya TFF na bodi ya Ligi ambacho ni chombo cha TFF?

Hawakuishia hapo, Kuna chama cha soka Mkoa kinachoitwa FA mkoa kikajichotea milioni 18,898,718 bila kuelezwa kwa sheria au kanuni ipi na kimehusikaje na mechi za Ligi Kuu Tanzania. Wakaja na Gharama za tiket, hawajaeleza wana maana gani kusema gharama ya tiketi, bila shaka ni kampuni zilizoprint na kuuza tiketi ambapo wamezilipa milioni 22,585,475.

Kituko kingine cha wizi wamekuja kuchota pesa milioni 22,048,504 kwakusema ni za "Gharama za mchezo", Unaweza kushangaa na roho yako! Sijui wana maana gani, Yaani gharama walizochukua TFF, Bodi ya Ligi, Uwanja wa Mkapa, BMT na FA Mkoa sio gharama za mchezo bali kuna kikundi kingine kinachojilipa kinachoitwa gharama ya mchezo?. Vyombo vyote vilivyochota pesa hapo juu ni vya serikali, ilitosha baada ya makato ya TRA, kinachofuata kiwe klabu mwenyeji kuchukua 70% ya kilichobaki baada ya kodi kisha TFF na wahuni wengine wote waliochota pesa hapo juu basi wagawane 30% iliyobaki.

Shirikisho la Mpira nchini TFF litoe maelezo utata wa makato haya, Vilabu vinatumia gharama kubwa sana katika kuandaa timu zao lakini pesa ikiingia zaidi ya 70% zinaliwa na magenge ya uhalifu yaliyojificha katika mpira nchini. Pengine tuombe ukaguzi maalumu wa CAG katika mechi hizi za watani wa jadi na ikiwezekana ufanyike ukaguzi wa jumla kuanzia BM hadi huku chini."
 
Tanzania na wizi ni sawa na mti kwenye aridhi! Ukivitenganisha, kuna kitakachoacha uhai wake
 
Mkuu nakubaliana nawe kwamba kuendesha timu ni gharama kubwa sana. Hizi timu hazina mapato mengine ya uhakika zaidi ya viingilio. Matumizi ya Clubs za mpira ni mengi na ni ya gharama kubwa sana, kama mishahara ya wachezaji na makocha, matibabu, usafiri wa magari na ndege n.k. Nadhani kwa timu wenyeji wapewe 70% yao katika gate collection kabla ya makato yeyote; na 30% ndio ilipe hizo gharama zingine.
 
TFF, YANGA, SIMBA na tasnia ya mchezo wa mpira Tanzania imetekwa na wahuni miaka mingi sana na sehemu ya watu kupiga hela, kutakatisha hela, biashara za madawa nk.

JPM alikuwa sahihi kabisa kuwakamata na kuwafunga wale wahuni ingeweza kuleta ahueni angalau kwenye soka la Bongo.

Soko la bongo haliwezi kuendelea hata siku moja na wala vijana wetu wengi kufanikiwa kucheza soka Ulaya kama hawa wahuni wataendeelea kuachwa kwenye system ya soka la Bongo.
 
Dah!Aisee huu ni wizi kamili.TFF wametunga majina mengi kwa mtu mmoja ili kufanikisha wizi.Hapo bado hawajaandika gharama za kuwakaribisha watazamaji milioni 42!Shenzi sana hadi keshokutwa.
 
Umetumia jina zuri kwamba TFF na "Magenge ya uhalifu". Hawa wanapaswa kufungwa kwa uhujumu uchumi.
Ahsante mkuu,ila andiko hilo ni mali ya Yericko Nyerere !

Mimi nimelitumia kama uthibitisho kwamba hayati Magufuli (R.I.P),alikuwa sahihi kabisa pale alipojaribu kupambana na hili genge.
Aliwatia ndani wote na akaonekana mbaya kwa baadhi ya wana jamii.

Miaka miwili baadae,tunaanza kuona ni kwa nini Magufuli alifanya vile!
 
Mnalalamika nini? Unapanda magugu na kutegemea kuvuna mahindi? Ukisapoti uozo lazima utegemee uvundo. Hizi timu zinatumika kama chambo cha kuwapumbaza watanzania waendelee kuduwaa ili wasikumbuke kuwawajibisha viongozi wabovu. Wanapeleka mpaka mabango kwenye mpira kusapoti mafisadi. Yaani mnataka nchi iwe na viongozi wavivu na mafisadi halafu timu za mpira zisalimike?
 
Sidhani kama kuna watu walilalamika kwa wizi wa hao TFF kushughulikiwa.Jamaa ni wezi wezi wezi mnooooo!Hawa wezi washughulikiwe!
 
Uongo, hayo makato yako hivyo hata wakati wa jiwe, hakubadilisha chochote.
 
Mkuu. Kujua tatizo na kuweza kuliondoa ni vitu viwili tofauti. Tatizo la Magufuli alishindwa kuondoa haya matatizo na ndiyo maana yanarudi kwa kasi kuliko mwanzoni. Magufuli alikataa katakata kuchukuwa njia sahihi za kuondoa matatizo, na zaidi akawa anawachukia na hata kuwaua wale waliokuwa wanamshauri njia sahihi za kuchukuwa. Badala yake akajifariji kwa kupambana kwa njia za ki-local kabisa.
 
Kwani Rage alifungwa wakati wa Magufuli?

Ujinga huu.
Naona likitajwa jina la Magufuli unaharisha mkuu. Ni cheti feki au mfanyakaz hewa? Tuambiane, maana mjadala unahusu tff na makato yao pia Magufuli kukata Cartels wewe unaleta habar ya Rage kama Rage. Au hata haukujui maana ya cartels kwa vile cheti hakiruhusu.

Wewe voicer hebu kuja uelekeze huyu jamaa maana ya cartel kama ilivyotumika asiendelee kukurupuka
 
Mpira wetu kivyetu vyetu kimpango wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…