Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari wakuu!
Mwaka jana katika harakati za kufuatilia mirathi ya mke wangu ambaye alifiwa na baba yake ikanilazimu nizitafute ofisi za PSSSF mkoa wa Temeke au Ilala maana mimi ni mkazi wa Dar es salaam.
Nikaingia website ya PSSSF nipate location za ofisi zao. Nikachukua details muhimu na namba za simu, nafika mahali ambapo wameandika kuwa ndipo ofisi za mkoa wa Temeke naambiwa kuwa walihama kitambo.
Napiga simu niwaulize walipo anapokea mwananchi anasema namba haimilikiwi na ofisi bali yeye. Nilipomuhoji anasema kuwa wengi tu humpigia kwa bahati mbaya wakikusudia kuwapigia PSSSF.
Leo tena naingia tovuti ya wizara ya fedha Salary Portal kuna mzee hapa kazini kasahau password na e-mail aliyofungulia haitumii sasa. Ikalazimika nichukue namba ya msaada, napiga anapokea mwananchi ambaye anasema haifahamu salary portal ja hajawahi kuwa mtumishi wa wizara ya fedha.
Sasa kama tu kufanya changes muhimu kwenye website muhimu hawataki au wanapuuzia kuna haja kweli ya kuwaongezea mshahara hawa watumishi?
Mimi ni mtumishi wa umma pia na ni muhanga wa kutopandishwa daraja na mshahara ila kwa hakika huku makazini kuna uzembe sana hasa mtu akishapata kibarua cha permanent.