Uchaguzi 2020 Magufuli alitudanganya, hebu tumpe kura Tundu Lissu naye atende

Uchaguzi 2020 Magufuli alitudanganya, hebu tumpe kura Tundu Lissu naye atende

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Ndugu yangu mwanaJamiiForums tuwe na kumbu kumbu kua 2015 wakati Rais Magufuli anaomba kura aliahidi mambo mazuri na makubwa sana lakini mpaka sasa anatimiza ungwe ya miaka mitano hajatumia yote. Hii maana yake alitudanganya sana.

Hebu tazama haya halafu tathmini kisha chukua hatua muhimu.

1. Aliahidi kuboresha maslahi kwa watumishi wa umma, mpaka sasa hakuna kitu kama hicho. Maana yake alidanganya.Eti sasahivi anaomba kura kua ataboresha, alikua wapi miaka 5 iliyopita?

2. Aliahidi kuondoa tatizo la ajira lakini hakufanya hivyo. Ni juzi tu amekiri kua ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa huku akiomba tena ridhaa ili aje aboreshe utafikiri miaka 5 iliyopita hakuwepo.

3. Aliahidi milion 50 kila kijiji kitu ambacho hakutimiza hata kidogo.

4. Aliahidi kuboresha maisha ya watanzania lakini mpaka hali za maisha ya watanzania ni ngumu kupata mlo mmoja kwa siku ni tatizo kubwa.

5. Aliahidi kuwakopesha wanafunzi wote wenye sifa Elimu ya juu,lakini mpaka sasa ni vilio kila mahali vijana wengi hawapati mikopo kwa sababu mbali mbali zikiwemo kusoma shule binafsi.

Watanzania wenzangu, kumbu kumbu hizi zitoe hukumu ya kutosha na ni dhambi kurudia makosa yale yale.
 
Urais sio Sehemu ya kujaribu

Tunataka Rais Magufuli aendelee na tutampigia kura za kishindo, Kwasababu msaliti wa Nchi toka ubeligiji ametutharau sana Watanzania

Muulizeni Lissu Kwanini amekata tikit ya kurudi ubeligiji wiki moja baada ya Uchaguzi

Anajua Watanzania wamemkataa
 
Magufuli aliingia 2015 akiwa Rais? Hopeless kabisa wewe
 
Urais sio Sehemu ya kujaribu

Tunataka Rais Magufuli aendelee na tutampigia kura za kishindo, Kwasababu msaliti wa Nchi toka ubeligiji ametutharau sana Watanzania

Muulizeni Lissu Kwanini amekata tikit ya kurudi ubeligiji wiki moja baada ya Uchaguzi

Anajua Watanzania wamemkataa
Lile goli lililotungisha mimba yako afadhari mshua angelipigia puri bafuni..maana hauna maana kabisa.
 
Urais sio Sehemu ya kujaribu

Tunataka Rais Magufuli aendelee na tutampigia kura za kishindo, Kwasababu msaliti wa Nchi toka ubeligiji ametutharau sana Watanzania

Muulizeni Lissu Kwanini amekata tikit ya kurudi ubeligiji wiki moja baada ya Uchaguzi

Anajua Watanzania wamemkataa
Nyie hata akiamua kupita mfereji hadi mfereji akiwapima oil mtamuunga mkono.
Sishangai
 
Weka mabaya na mazuri waliyokwisha fanya na wanayopanga kufanya wote wawili
 
Urais sio Sehemu ya kujaribu

Tunataka Rais Magufuli aendelee na tutampigia kura za kishindo, Kwasababu msaliti wa Nchi toka ubeligiji ametutharau sana Watanzania

Muulizeni Lissu Kwanini amekata tikit ya kurudi ubeligiji wiki moja baada ya Uchaguzi

Anajua Watanzania wamemkataa
Hata huyo magufuli alijaribu akapata ndo maana kila wakati analia urais ni kazi ya mateso, mwambie aachie kwa amani Lissu aichukue ateseke.
 
Watanzania hawawezi kupigia kura msaliti wa Nchi
Pia Tanzania hatutaki ushoga,
Hata huyo magufuli alijaribu akapata ndo maana kila wakati analia urais ni kazi ya mateso, mwambie aachie kwa amani Lissu aichukue ateseke.
 
Yote uliyoyataja Rais Magufuli ameyatekeleza kama aliavyoahidi tena na zaidi. Fungua macho yako uone nje ya mtaa wa Ufipa. Watanzania tumeamua tunampa tena kura za Kimbunga Dkt Magufuli. Hatutaki wakala wa Mabeberu na anayepapatwa na mabeberu
 
Alichotekeleza Magufuli ni Uwanja wa Ndege Chato na Uwanja wa Mpira wa Kimataifa kijijini Chato
 
Alichotekeleza Magufuli ni Uwanja wa Ndege Chato na Uwanja wa Mpira wa Kimataifa kijijini Chato
Uwanja wa mpira unaojengwa Chato utakuwa na uwezo wa watazamaji 105,000 na ni ule ulioombewa msaada toka kwa Mfalme wa Morocco pamoja na ule Msikiti uliojengwa Dar ambao unangoja Mfalme aje afungue.

Uwanja wa Mkapa ulio Dar wenye uwezo wa watazamaji 60,000 huwa haujai labda siku Simba na Yanga zinacheza, haiingii akilini kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kujenga uwanja mkubwa kuliko yote nchini kijijini Chato.

Dar ina wakazi milioni 6 wengi wao ni wafanyabiashara, wafanyakazi na wakulima pembezoni na mkazi yeyote anaweza kufika popote ndani ya madakika tu, thanks to Flyovers, Mwendokasi hata Daladala.

Ukanda wa Chato una Wasukuma milioni 6 wengi wao ni wakulima, wafugaji na wafanyakazi wachache walioenea eneo kubwa kuliko nchi nyingi duniani zenye wakazi wengi kama hao. Pamoja na kuwepo kwa Chato International Airport na madege lukuki ni wakati gani utatumika ukiwa umejaa walipa kiingilio halisi kuwezesha Uwanja kujitegemea bila ruzuku? Cha bure huwa bure!
 
Magufuli aigeuza Zanzibar kuwa kama "DARFUR" wakati Maalim anataka uwe kama SINGAPORE

Jionee mwenyewe
👇
 
Sumu hailambwi.Kuwapa kura chama cha Mbowe ni kupoteza kura yako bure.
 
Back
Top Bottom