Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Upande wa mashariki mwa Afrika nchini Tanzania. Hayati John Pombe Magufuli aliupiga mwingi sana enzi za utawala wake kiasi kwamba uchumi ulipanda mpaka uchumi wa kati kabla ya kurudi kwenye uchumi wa chini katika utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan. Magufuli alileta Elimu bure jambo lilionekana kama ni kitu kisichowezekana mbele ya watu wengi. Kila baada ya miezi kadhaa kulikuwa na mradi mpya unaanzishwa au umekamilika, hata majina ya ndege kama dreamliner na bombadier yalianza kukaririwa na wananchi hata wa huko chitohori kusikokuwa na Airport.
Jamaa alipigana na rushwa kiasi kwamba barabara na makazini ukipewa hata mkono wa asante unaogopa husikamatwe, Takukuru walikuwa wanaripoti matukio ya rushwa kama habari nyingine tofauti na sasa hawasikii. Alikuwa na kauli yake kuwa tajiri kwake anafanywa chochote kitendo kilichopelekea vigogo wengi kutokutumia pesa kuhujumu uchumi. Wanachi wa kawaida wakatembea vifua mbele, na Magufuli akapewa jina jipya la bulldozer kutokana na kazi aliyofanya kwa muda mfupi, kazi ya bulldozer mnaifahamu jinsi inavyosafisha barabara.
Kama wanavyosema vizuri havidumu, mwamba alifariki 2021 mwezi machi, na watu wasiopenda maendeleo wakamwita Dikteta. Lakini hata hivyo wapinzani wake kama Mange Kimambi na Godbless Lema wamewahi kukiri hadharani kuwa mwamba alikuwa bora sana kwenye kupambana na ufisadi na kuleta maendeleo nchini.
Basi bwana, ikapita miezi kadhaa, ikawa usiku ikawa asubuhi akaibuka mwamba mwingine upande wa magharibi ya Afrika nchini Burkina Fasio, anayeitwa Ibrahim Traore. Ni kama Magufuli mwingine aliyezama mashariki akaibuka magharibi. Tangu ameingia madarakani Kapteni Ibrahim Traoré mnamo mwaka 2022, Burkina Faso imeongeza faida yake ya kuchimba dhahabu kutoka $ 1B hadi $ 18B kufuatiw kupiga marufuku kampuni za magharibi kuchukua udhibiti wa rasilimali zake.
Chini ya uongozi wake, nchi ilitaifisha migodi muhimu, na ikarudisha faida kwa nchi.
Pesa hiyo sasa inatumika kuwekeza katika miundombinu ya umma, shule, huduma za afya, na utetezi -kuhakikisha utajiri wa burkinabé unakaa na watu wa Burkinabé.