selemala
JF-Expert Member
- Feb 14, 2007
- 370
- 253
Watu wengi wanafanya kosa la kifikra kwa kufikiria Ulaya ni Majengo/Miundo mbinu/ Vitu tu, na kusahau kitu muhimu zaidi “Watu wa ulaya.”Nimemsikia mgombea wa urais CCM anasema anataka tanzania iwe kama ulaya.
1. Mwambieni hakuna ulaya ambayo imezuia vyama vya upinzani kufanya mikutano ya hadahara na wananchi wake kuandamana.
2. Hakuna Ulaya ambayo imezuia kurusha matangazo ya bunge liv10. Hakuna Ulaya ambayo ina sheria zinazo wanyima ...,,
Ukitaka kuelewa hili fikiria ni nini kitatokea baada ya miaka kumi iwapo tutabadilishana nchi na Taifa moja lililoendelea la Ulaya. Yani sisi twende huko halafu wao waje huku.
Nashahuri kua badala ya “kama Ulaya” kua lengo au kipimo na cha maendeleo yetu (kipimo hafifu sana hichi na nicha muda mfupi), kwanza tuache uvivu wa kufikiri, halafu tukae chini kitaifa na kupanga/kutafuta suluhisho za muda mrefu za matatizo yanayotukabili sasa na yanayoweza kuja mbeleni, halafu tuje na mikakati ya utekelezaji isiyo na chama, dini wala kabila.
Tumepewa na Muumba ubongo wenye nguvu sana. Viongozi;
- acheni kupofushwa na umimi, uchama, ukabila na Udini na anzeni kuona kupitia utaifa na ubinadamu.
- andaeni na tumieni rasimali watu ipasavyo. Msichukie tofauti za mawazo badala yake muweke mazingira ya watu kuchangia mawazo yao katika hali umoja wa kitaifa.