Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 8,367
- 12,362
Wewe si umepewa buku Saba kupiga porojo. Sasa sisi tunaoshika jembe kulima ndo tunasema hatumpigii kura .Wewe wasema
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe si umepewa buku Saba kupiga porojo. Sasa sisi tunaoshika jembe kulima ndo tunasema hatumpigii kura .Wewe wasema
Hapa tayari umepanic hadi umehama mada.Hususani ikiwa ni sehemu pekee iliyojaa wapiga kura wa Lisu!
Lisu akipata walau kura 20% nipigwe ban ya maisha hapa jf
Wewe umepewa ngapi kuongea umbea?Wewe si umepewa buku Saba kupiga porojo. Sasa sisi tunaoshika jembe kulima ndo tunasema hatumpigii kura .
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kupoteza muda, tafuta wenzako, pateni maelezo toka idara ya Kilimo hapo ulipo, pateni mkopo mpige kaziWewe si umepewa buku Saba kupiga porojo. Sasa sisi tunaoshika jembe kulima ndo tunasema hatumpigii kura .
Sent using Jamii Forums mobile app
Me Ni mkulima Sina wa mgombea wa kupigia debe kama wewe. Au umeona sehemu namsifia mgombea fulaniWewe umepewa ngapi kuongea umbea?
Endelea kusifia tu. Watakuteua kuwa DasAcha kupoteza muda, tafuta wenzako, pateni maelezo toka idara ya Kilimo hapo ulipo, pateni mkopo mpige kazi
#achakaziiendelee
Si Lumumba mna ID tano tano? Lazima utaipiga chini hii ID dada.Hususani ikiwa ni sehemu pekee iliyojaa wapiga kura wa Lisu!
Lisu akipata walau kura 20% nipigwe ban ya maisha hapa jf
Wakipinga kila kitu inakuuma nini. Si na wewe uunge mkono kila kitu ili ngoma iwe draw ebo!Hapo ndipo tatizo lenu lilipo, kupinga kila kitu na kushindwa kuelewa uhalisia wa mambo.
Changamoto zipo, hilo sijakataa. Pili nimeandika kuwa Roma haikujengwa ndani ya siku moja. Hatua zilizofikiwa zinaonesha mafanikio. Nometoa mfano wa sehemu husika, bado mnapinga. Nyie watu vipi? Mnafikiri tunaweka kuwa Kama Ubelgiji ndani ya miaka mitano tuu?
Mwaka jana wakati nipo nyumbani huko Tanzania,nilienda hiyo benki kuomba 700 milioni. Nilichoambiwa na kufanywa,nilipeleka PCCB,majibu sijapata.Undeni vikundi nendeni benki ya Kilimo. Acheni maneno mbofumbofu
Swali fikirishi je wote tuje handeni kulima mihogo?Wanajamvi. Amani kwenu
Leo ni siku nyingine ya kutafakari utendaji mzuri wa Rais Magufuli na serikali yake katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 - 2020. Leo tuangalie Sekta ya Kilimo.
Katika jitihada za kuendeleza kilimo, kuliundwa dirisha la kilimo katika Benki ya Uwekezaji (TIB). Akiwa katika miaka yake ya mwisho, mzee Kikwete aliunda benki ya Kilimo. Katika kipindi hiki cha miaka mitano, Rais Magufuli ameendelea kuiimarisha benki ya Kilimo.
Sekta ya Kilimo ni sekta iliyoajiri watanzania wengi zaidi. Ni sekta kubwa. Ninaomba Leo niongelee benki ya Kilimo. Kwa kutambua kuwa wakulima wengi hawakidhi vigezo vya kukopesheka katika mabenki ya biashara, kwa makusudi serikali imeweka utaratibu maalimu wa kuwakopesha wakulima, utaratibu ulio tofauti kabisa na mabenki ya biashara.
Wakulima wadogowadogo wenye mashamba yenye ukubwa wa heka 1 - 50 wanaunda kikundi cha watu 5 - 30. Serikali inawakopesha fedha kw ajili ya kuendeleza kilimo. Fedha inatoka kwa awamu na timu ya Kilimo ya wilaya chini ya afisa kilimo anafanya ufuatiliaji.
Nitatoa mfano wa wakulima wa mihogo wilayani Handeni mkoani Tanga. Hapa vikundi vingi vimepata mikopo na kazi inaendelea. Wakulima wanapata shilingi 1,500,000 kwa heka moja. Fedha hii inatoka kwa awamu kuanzia kuandaa shamba, pembejeo, upandaji, upaliliaji, uvunaji na usafirishaji. Rejesho linafanywa baada ya mavuno kuuzwa. Hii sio hadithi, ni mambo halisi yanayotokea. Mpaka Sasa shilingi bilioni 3.6 zimeshakopeshwa kwa wakulima wilayani Handeni. Hali iko hivi maeneo mengine ya Tanzania.
Nawashauri watanzania wenzangu kufika ofisi za kilimo zilizopo karibu nanyi mpate maelezo ya kina nanyi mfaidike.
Nimelazimika kuandika haya kwasababu mnaulaumu tuu, mnasema hakuna kilichofanyika kwenye kilimo. Tatizo hamfuatilii mambo mnaulaumu tuu huku mkiwa hamna taarifa sahihi.
Mambo yameanza kunoga, mambo yameanza kukaa sawa Ila ni lazima tuwe na subira, Roma haikujengwa ndani ya siku moja. Tinaposema JPM 5 tena, ni mambo kama haya yanayotupa nguvu.
Hongera JPM
Hongera serikali
Hongera CCM
JPM mitano tena #achakaziiendelee
Kumbe aliyekuita msukule hajakosea. Nenda kwenye maandishi ya taasisi mbalimbali za GoT uone yalivyo matamu,ila nenda kwenye uhalisia uone uakisi wa hayo maandishi kivitendo.
Basi karibu umuunge mkono Dr. Magufuli, tusonge mbele kwa pamojaMe Ni mkulima Sina wa mgombea wa kupigia debe kama wewe. Au umeona sehemu namsifia mgombea fulani
Sent using Jamii Forums mobile app
Handeni ni sehemu ya Tanzania. Mfano huo umetumika kuonesha kuwa kazi ya kukuza na kuimarisha sekta ya Kilimo inafanyika.Swali fikirishi je wote tuje handeni kulima mihogo?
Kelele tunazo mimi kele yangu ni sera za majukwaaniHandeni ni sehemu ya Tanzania. Mfano huo umetumika kuonesha kuwa kazi ya kukuza na kuimarisha sekta ya Kilimo inafanyika.
Kama haitoshi, hatuwezi wote kuwa wakulima wa mihogo.
Nataka mtu aje aseme yeye na wenzake walichukua hatua gani? Wako wapi na ni nani aliyewakwamisha? Kinyume na hapo acheni kelele, chukueni hatua
[emoji23][emoji23][emoji23]Basi karibu umuunge mkono Dr. Magufuli, tusonge mbele kwa pamoja
Huko unakoishi hakuna vigezo na masharti? Milioni 700 ni mkopo kwa mkulima mkubwa. Sasa wewe umetoka kubeba boksi unataka upewe tuu kirahisi M700?Mwaka jana wakati nipo nyumbani huko Tanzania,nilienda hiyo benki kuomba 700 milioni. Nilichoambiwa na kufanywa,nilipeleka PCCB,majibu sijapata.
Benki pesa hawapewi kama inavyotakiwa. Wewe endelea na propaganda zako.
Ulijaribu wapi ukakwama?Kelele tunazo mimi kele yangu ni sera za majukwaani
PCCB tena mkuu?Mwaka jana wakati nipo nyumbani huko Tanzania,nilienda hiyo benki kuomba 700 milioni. Nilichoambiwa na kufanywa,nilipeleka PCCB,majibu sijapata.
Benki pesa hawapewi kama inavyotakiwa. Wewe endelea na propaganda zako.
Nikizitaja km una pacemaker utazimiaUlijaribu wapi ukakwama?