Magufuli ang'ara kwenye Sekta ya Kilimo. Hongera sana CCM

Swali fikirishi je wote tuje handeni kulima mihogo?
Handeni kwa Gondwe waliambiwa Limeni mihogo kuna viwanda vya wachina vinahitaji sana hio mihogo,hahah mihogo ikalimwa kila sehemu afu wachina wakawaachia manyoya wana Handeni kikawa ni kilio kitupu.
 
Acha kupoteza muda, tafuta wenzako, pateni maelezo toka idara ya Kilimo hapo ulipo, pateni mkopo mpige kazi
#achakaziiendelee
changamoto ya benki ya kilimo haitoi mikopo moja kwa moja kwa wakulima, bali mikopo inapitia saccos na amcos, na ikishafika huko haifiki kwa wakulima inavyotakiwa mkuu, hapo ndio tatizo lilipo
 
Mbona kijana mwenzenu analima bamia mbutu na maisha yake yanaenda poa tuu?
 
Mtoa mada bora ungekaa kimywa. Wakulima Wa Kahawa wanalia, korosho wanalia, pamba wanalia, mahindi usiseme. wewe siyo mkulima
 
changamoto ya benki ya kilimo haitoi mikopo moja kwa moja kwa wakulima, bali mikopo inapitia saccos na amcos, na ikishafika huko haifiki kwa wakulima inavyotakiwa mkuu, hapo ndio tatizo lilipo
Hapo sasa unasema kitu. Vikundi ni muhimu Ila Kama pesa haifiki Kama inavyotakiwa inaweza kuwa ni matatizo ya kiongozi hapo kwenu. Hatahivyo hakikisheni mnafikisha matatizo yenubkwa diwani, mbunge, afisa kilimo, DED, DC, RC na Kama vipi mnapanda zaidi kwa waziri.
Bashe ni mwana, anafikika. Kama vipi mchekini
 
Bado jembe la mkono linaendelea miaka 60 ya uhuru sasa wakulima hawana masoko ya mazao yao. Kilimo ni cha kienyeji sana, kupata hivyo mikopo ni shida na unaishia kupata laki 2 wakati unahitaji 50M. Hakuna lolote tunahitaji mabadiliko ya mfumo wa kilimo na sio kuwapatia wakulima vimikopo visivyosaidia kitu.
 
Hususani ikiwa ni sehemu pekee iliyojaa wapiga kura wa Lisu!

Lisu akipata walau kura 20% nipigwe ban ya maisha hapa jf
mtu apore korosho za watu afu asifiwe kilimo kipi ? labda bhangi
 
Hakika ninawaambia, kusubiri mtasubiri sana. Oktoba 28 watanzania wanamthibitisha jembe kwa wino wa dhahabu aongoze mbio za masafa marefu na kuhakikisha kazi inaendelea
Kwa umasikini huu sahau tz ya Jana sio wa Leo hii ni dotcom generation haiishi kwa propaganda za tbc
 
Aende pia akawaulize wakulima wa PAMBA kule kanda ya ziwa, watamwambia kilichowakuta.
 
Mtu anae tumia masaa mawili kuonyesha alichofanya jua nothing he did
 
Mleta mada usipotoshe umma Mimi nipo Handeni watu wamepigizwa hiyo hela walengwa wameambulia 7% ya pesa yote na 93% imeliwa kupitia vikundi feki vya vigogo wakiwemo wanasiasa na viongozi wa serikali.
Handeni ina kata 27 na kata 9 ndiyo zilikuwa na vikundi lakini vingi ni feki, nipo pamoja nawe kwamba wamepewa 1.5 mil Kwa heka lakini heka nyingi ni hewa.

Mfano mbunge aliyeteuliwa kupererusha bendera ya ccm Jimbo la Handeni vijijini amekula 160 mil. kupitia vikundi feki ambavyo havina hata uchochoro wa shamba, zipo familia za vigogo wengine ambao wamekula hardly 50 mil.

Walengwa wamefanikiwa kuchukuwa 252 mil. out of 3.6 billion vipo vikundi feki kutoka DSM navyo vimekuja kukomba hela kupitia vigogo wa hapa ofisini hadi waliopo ofisi ya mkuu wa mkoa Tanga.

Na wamekula hizi hela 7bu zimetolewa Kwa misingi ya kampeni hivyo ni za kisiasa Kwa kuwa hadi sasa hakuna soko linaloeleweka la kuuzia huo muhogo utakaovunwa.
Mimi nipo hapa Kideleko sec school.

Wakubwa wamefanikiwa kufanya ufedhuli huu kwakuwa huku Handeni bado watu wanaishi Karne ya 15 elimu duni ccm kila mahala watu walio wengi hawana walijualo ndo maana hata wewe umekuja na mbwembwe humu ndani ukifahamu fika hakuna mwananchi wa huko anaejua huu ushenzi.

Mleta mada kwani wewe upo Handeni au upo huko benki wanakokopesha wakulima? Yawezekana huna ujualo kuhusu huu mkopo Kwa vikundi vya wakulima wa mihoga hapa handeni hivyo mwambie Magu kuw only 7% out of the disbursed lump-sum went to the intended groups but the rest 93% has gone in Zigua we call malunywa.
 
Asante kwa taarifa mkuu.

Wewe mwenyewe unakiri kuwa serikali imeleta fedha ila zimeliwa. Tambua kuwa wanahandeni wenye taarifa Kama hizo ulizonazo ndio mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kutetea maslahi yenu.

Taarifa uluzinazo ni muhimu, umechukua hatua gani au mnasubiri mpaka Rais Magufuli aje?

Gondwe alikuwa makini Sana sijui hilo limetokeaje. Mmewaona Takukuru?

Walinzi wa kwanza wa maslahi ya Handeni, ni wanahandeni wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…