Amemtaja Jinga Kubwa?..Hiyo ni mbinu tu kama hizi zifuatazo!! Hakika mwaka huu ni wa ΒMabadilikoΒ maana CCM wametumia na bado watatumia mbinu nyiingi bila Kufanikiwa kuyazuia Mabadiliko!!Mfano;
1. Wamenunua vyombo vya habari kama Magazeti,Vituo vya Redio na Runinga na Blogs lakini wapi!!
2. Wamenunua Viongozi Waandamizi wa vyama vya Upinzani kudhoofisha Mabadiliko lakini wapi!!
3. Wamenunua Wasanii wa Maigizo,Wanamichezo na Wanamuziki wa Kizazi Kipya kuwavuta vijana lakini wapi!!
4. Wametoa vitisho kwa watu wanaopenda mabadiliko vijana na wakina mama lakini wapi!!
5. Wamepenyeza watu kudhoofisha upinzani katika vyama na kwa Wanaharakati lakini hollaa!!
6. Wamejaribu kuzusha tuhuma mbalimbali kwa Viongozi wa ΒMabadilikoΒ lakini wapiii!!
7. Wametumia vyombo vya dola kuzima ΒMabadilikoΒ kwa kuwakamata na kuwasweka ndani na kuwafungulia kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu wana Mabadiliko lakini wapiiiii!!
8. Wameunda Kamati ya watu 32 maalumu kwa ajili ya kuporomosha matusi na kuzusha tuhuma za ufisadi kwa Lowassa na wana ΒMabadilikoΒ Lakini wapiiii!!
9. Waliapa kutokutumia Helkopta katika Uchaguzi wa Mwaka huu kwa kusingizio wanataka kupita kila kata kwa wapiga kura lakini wapiiii!!
10. Wameandaa tafiti feki za Twawezwa na Ipsos kuwalaghai wana ΒMabadilikoΒ lakini wapi!!
11. Wametumia Mamilioni kuwalaghai watumishi wa Umma kama Polisi waliowatelekeza siku nyingi kwa kuwapa posho nono na ahadi lukuki lakini wapiiii!!
12. Wamejaribu kuwalaghai walimu ambao waliwasahau miaka nenda rudi na sasa wameahidi kuwalipa baadhi ya madai yao lakini wapiii!!
13. Wamejaribu kutoa kuwaondoa baadhi ya Watumishi wa idara Muhimu zinazohusika na uchaguzi ili kujenga hofu na kuandaa mipango miovu lakini wapi!!
14. Wamejaribu kuwatumia Vingozi wastaafu kuomba Huruma kwa Wananchi waliowaacha katika Umaskini mkubwa,maradhi na ujinga huku wakiwakejeli lakini wapiiii!!
15. Wamejaribu kuwazuia Wapinzani kutumia Viwanja vyao na Sehemu mbalimbali kwa ajili ya Kampeni lakini wapiiii!!
16. Wamejaribu kutumia ulaghai wa kuwavalisha wafuasi wao mavazi ya Upinzani ili wawakatate Viongozi wa Upinzani eti kuonesha kumeguka kwa Upinzani lakini wapi!!
17. Wamejaribu kupanga njama za kuwadhuru Viongozi wa Upinzani kwa namna mbalimbali lakini wapiii?
18. Wamejaribu kutumia Matamasha,Makongamano,Mikutano,Semina,Maandamano,Mikusanyiko,Matamko,na Warsha mbalimbali kubadili hisia za Wananchi dhidi ya Mabadiliko lakini wapiiiiiiiiiiiiiii!!!
19. Wamejaribu kupanga Mapinduzi hewa ya Kuwapindua Viongozi wa Upinzani kuonesha kumeguka kwa Umoja wa UKAWA lakini wapiii!!
20. Wamejaribu kupiga push ups,kuongea lugha za makabila mbalimbali,kucheza rhumba,kuandaa fiesta na Kufunga milango watu wasiondoke Viwanjani baada ya Fiesa lakini waaapi!!
21. Wamejaribu kusomba watu kwa malori,pikipiki,bajaji,Mabasi kutoka Mkutano mmoja hadi mwingie kujaza mikutano kuwahadaa wana ΒMabadilikoΒLakini waaapi!!!
22. Kuzuia post za Ki ΒMabadilikoΒ katika Mitandao ya Kijamiii kama JF,FB,Twitter, na Kuwa Block wanao post Mabadiliko ..Lakini wapiiii!!
23. Wamejaribu kuwashinikiza waajiri kuwafukuza Wafanyakazi wao wanaopenda Mabadiliko ili kuwatisha wengineo Lakini waapiii!!
24. Wamejaribu kurusha ndege za Kivita ili kuwatisha wananchi dhidi ya Mabadiliko pamoja na kuonesha Picha za Machafuko katika nchi mbalimbali na kufananisha Mabadiliko na Kuwait NA Iraq lakini waaapiiii!!!!
25. Wanajaribu kutengeneza ΒGoli la MkonoΒ kwa takwimu za wapiga kura na kuzuia Wapinzani kuhakiki taarifa sahihi za Vifaa na Daftari kwa wakati lakini wapiiiiii!!
26. Wamejaribu kuzindua Miradi iliyokwisha zinduliwa zamani pamoja na Miradi hewa ama ambayo hata haijaanza kuwarubuni wananchi lakini wapi!!!!
27. Na bado ndani ya siku zilizobakia watakuja na mbinu mbalimbali tena huenda zikawa ni mbaya zaidi na zenye dalili ya uvunjifu wa AMANI na UTULIVU wa Nchi ili mradi wazuie ΒMabadilikoΒ ninaamini kwa Msaada wa MUNGU watashindwa na kulegea!!!!
Mimi nitampigia kura yangu ya thamani ΒEDWARD NGOYAI LOWASSAΒ pamoja na ΒDiwani na ΒMbungeΒ wa UKAWA!!..Kwa maisha bora ya kwako nay a Kizazi chako Ondoa CCM,kwani imeishiwa pumzi!!!! ΒALUTA Continua, Victoria AscertaΒ.... ΒThe Struggle Continues, Victory is CertainΒ; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!