Elections 2015 Magufuli ataja mafisadi CCM

Elections 2015 Magufuli ataja mafisadi CCM

Mbona hawataji?huyu kilaza anafikiri nchi ni kama barara he!yeye mwenyewe ni fisadi mkubwa kauza nyumba za serekali,amejenga magorofa makubwa kwa mshaharagani?joka mkubwa huyu.

nimeamini chadema wanahusuda na magufuli....kiukweli tuhuma zote wanazompaaa magufuli ukitaka kujuaaa ni za kinafiki wanadai magufuli ni mkali.alikamata meli ya wa Thailand Mara alibomoa Sheri ya mafuta.mara ni dikteta......hahaaaahahahaah yaaani reason za kitoto kupita kiasi aseeeee na unakutaaa jituu zimaaa LA chademaaa na mviiii zakeee linashabikiaaa uo upuuuzi
 
Wapi kataja sasa?
Kwanini asiseme kwa mfano TWIGA anafikaje airport na kupanda ndege?

Halafu hivi kesi ya meno ya TEMBO yaliyo kamatwa Malawi imefikia wapi?
 
Fisadi moja limekimbilia chadema.linaitwa Edward ngoyai Lowassa.akiingia tu huyu ndio wa kuanza nae.

Magufuli ajianze mwenyewe kwa pesa alizopiga Feri kununua kibuko kibovu cha 1978 kwa billion 8, kisha aendelee kujihukumu kwa uuzaji wa nyumba za Serikali kisha akajiuzia nyumba kibao na kuzigawa kwa michepuko na mdogo wake, huku mabilioni yakipotea wizarani kwake kwa kulipa kandarasi feki na penat kibao.akimaliza hapo aendelee na escrow na wengineo hapo italeta Maana.
 
Sasa kabla hajaenda ikulu na ndoto yake hiyo ya mchana anitajie hao mafisadi atakao washughulikia ni kina Nani ??? Akitaja tu kura yangu nampa kiroho safi ,asituletee hadithi za Jakaya na majina ya wauza unga toka anaingia Ikulu mpaka anaondoka hata jina la teja hajataja
Aanze na jina lake mwenyewe kwa kuwa kalitia Taifa hasara nyingi zikiwemo kuwalipa fidia Meli ya samaki na kituo cha mafuta mwanza,huku Dhambi ya kuuza nyumba za Serikali ikimganda pia, awataje wote waliochukua pesa za escrow kule stanbic bank.
 
Aanze na jina lake mwenyewe kwa kuwa kalitia Taifa hasara nyingi zikiwemo kuwalipa fidia Meli ya samaki na kituo cha mafuta mwanza,huku Dhambi ya kuuza nyumba za Serikali ikimganda pia, awataje wote waliochukua pesa za escrow kule stanbic bank.

Oh na yeye pia akiwa included kwenye hiyo list ....akifanya hivyo kura yangu anayo ,vinginevyo apige japo mbizi kuja kigamboni nitampa kura pia
 
Amemtaja Jinga Kubwa?..Hiyo ni mbinu tu kama hizi zifuatazo!! Hakika mwaka huu ni wa “Mabadiliko” maana CCM wametumia na bado watatumia mbinu nyiingi bila Kufanikiwa kuyazuia Mabadiliko!!Mfano;
1. Wamenunua vyombo vya habari kama Magazeti,Vituo vya Redio na Runinga na Blogs lakini wapi!!
2. Wamenunua Viongozi Waandamizi wa vyama vya Upinzani kudhoofisha Mabadiliko lakini wapi!!
3. Wamenunua Wasanii wa Maigizo,Wanamichezo na Wanamuziki wa Kizazi Kipya kuwavuta vijana lakini wapi!!
4. Wametoa vitisho kwa watu wanaopenda mabadiliko vijana na wakina mama lakini wapi!!
5. Wamepenyeza watu kudhoofisha upinzani katika vyama na kwa Wanaharakati lakini hollaa!!
6. Wamejaribu kuzusha tuhuma mbalimbali kwa Viongozi wa “Mabadiliko” lakini wapiii!!
7. Wametumia vyombo vya dola kuzima “Mabadiliko” kwa kuwakamata na kuwasweka ndani na kuwafungulia kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu wana Mabadiliko lakini wapiiiii!!
8. Wameunda Kamati ya watu 32 maalumu kwa ajili ya kuporomosha matusi na kuzusha tuhuma za ufisadi kwa Lowassa na wana “Mabadiliko” Lakini wapiiii!!
9. Waliapa kutokutumia Helkopta katika Uchaguzi wa Mwaka huu kwa kusingizio wanataka kupita kila kata kwa wapiga kura lakini wapiiii!!
10. Wameandaa tafiti feki za Twawezwa na Ipsos kuwalaghai wana “Mabadiliko” lakini wapi!!
11. Wametumia Mamilioni kuwalaghai watumishi wa Umma kama Polisi waliowatelekeza siku nyingi kwa kuwapa posho nono na ahadi lukuki lakini wapiiii!!
12. Wamejaribu kuwalaghai walimu ambao waliwasahau miaka nenda rudi na sasa wameahidi kuwalipa baadhi ya madai yao lakini wapiii!!
13. Wamejaribu kutoa kuwaondoa baadhi ya Watumishi wa idara Muhimu zinazohusika na uchaguzi ili kujenga hofu na kuandaa mipango miovu lakini wapi!!
14. Wamejaribu kuwatumia Vingozi wastaafu kuomba Huruma kwa Wananchi waliowaacha katika Umaskini mkubwa,maradhi na ujinga huku wakiwakejeli lakini wapiiii!!
15. Wamejaribu kuwazuia Wapinzani kutumia Viwanja vyao na Sehemu mbalimbali kwa ajili ya Kampeni lakini wapiiii!!
16. Wamejaribu kutumia ulaghai wa kuwavalisha wafuasi wao mavazi ya Upinzani ili wawakatate Viongozi wa Upinzani eti kuonesha kumeguka kwa Upinzani lakini wapi!!
17. Wamejaribu kupanga njama za kuwadhuru Viongozi wa Upinzani kwa namna mbalimbali lakini wapiii?
18. Wamejaribu kutumia Matamasha,Makongamano,Mikutano,Semina,Maandamano,Mikusanyiko,Matamko,na Warsha mbalimbali kubadili hisia za Wananchi dhidi ya Mabadiliko lakini wapiiiiiiiiiiiiiii!!!
19. Wamejaribu kupanga Mapinduzi hewa ya Kuwapindua Viongozi wa Upinzani kuonesha kumeguka kwa Umoja wa UKAWA lakini wapiii!!
20. Wamejaribu kupiga push ups,kuongea lugha za makabila mbalimbali,kucheza rhumba,kuandaa fiesta na Kufunga milango watu wasiondoke Viwanjani baada ya Fiesa lakini waaapi!!
21. Wamejaribu kusomba watu kwa malori,pikipiki,bajaji,Mabasi kutoka Mkutano mmoja hadi mwingie kujaza mikutano kuwahadaa wana “Mabadiliko”Lakini waaapi!!!
22. Kuzuia post za Ki “Mabadiliko” katika Mitandao ya Kijamiii kama JF,FB,Twitter, na Kuwa Block wanao post Mabadiliko ..Lakini wapiiii!!
23. Wamejaribu kuwashinikiza waajiri kuwafukuza Wafanyakazi wao wanaopenda Mabadiliko ili kuwatisha wengineo Lakini waapiii!!
24. Wamejaribu kurusha ndege za Kivita ili kuwatisha wananchi dhidi ya Mabadiliko pamoja na kuonesha Picha za Machafuko katika nchi mbalimbali na kufananisha Mabadiliko na Kuwait NA Iraq lakini waaapiiii!!!!
25. Wanajaribu kutengeneza “Goli la Mkono” kwa takwimu za wapiga kura na kuzuia Wapinzani kuhakiki taarifa sahihi za Vifaa na Daftari kwa wakati lakini wapiiiiii!!
26. Wamejaribu kuzindua Miradi iliyokwisha zinduliwa zamani pamoja na Miradi hewa ama ambayo hata haijaanza kuwarubuni wananchi lakini wapi!!!!
27. Na bado ndani ya siku zilizobakia watakuja na mbinu mbalimbali tena huenda zikawa ni mbaya zaidi na zenye dalili ya uvunjifu wa AMANI na UTULIVU wa Nchi ili mradi wazuie “Mabadiliko” ninaamini kwa Msaada wa MUNGU watashindwa na kulegea!!!!
Mimi nitampigia kura yangu ya thamani “EDWARD NGOYAI LOWASSA” pamoja na “Diwani na “Mbunge” wa UKAWA!!..Kwa maisha bora ya kwako nay a Kizazi chako Ondoa CCM,kwani imeishiwa pumzi!!!! “ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!

Polisi Musoma inawanyanyasa sana Wafuasi wa Ukawa wale vijana wote waliodeki barabara na kuosha gari ya Lowasa kwa mashati na tshart zao wamebambikiwa Kesi na polisi ili kuwakomoa. Mawakili wa chadema nendeni mkawatete na kuwashitaki wote wenye kuoneza uonevu wa raia
 
Tena akunje vizuri amperekee mamayake akafungie maandazikule EBO!
Nashukuru mkuu kwani walioandika ni NIPASHE ya leo kwa hiyo watamperekea mkuu ingawaje najua na wewe mmoja wa mafisadi hao waliotajwa.
 
mwaka huu hatudanganyiki ng'''''oooo

Shit haka kajamaa kalikouza nyumba za umma mpaka kwa mahawala zake! Halafu kanijifanya kanaweza kushughulikia mafisadi!
Kanifikiri kuongea kama chiriku ndo kutekeleza! Anadhani wenzake hawakuwa na akili,anafikiri ufisadi ni kitu rahisi hajui hata wafadhiri wa nchi yake ni mafisadi pia! Anadhani wachina wamepewa mikataba ya gesi hivi hivi? wamarekani wanaoendesha mitambo ya unene kwa capacity charge siyo ufisadi! Ataishia kwenda kutembeza bakuli tu kama mwenzake!

Tunataka mabadiliko ya system nzima siyo dereva huku gari ni lile lile!
 
Hao mafisi hadi waliopo kwake wana nguvu kubwa kuliko yeye.Akibahatika atanywea tu maana hata polopesa alisema hana ubia na mtu lakini walimnyoosha na wanamnyoosha tu!😀😀
 
nimeamini chadema wanahusuda na magufuli....kiukweli tuhuma zote wanazompaaa magufuli ukitaka kujuaaa ni za kinafiki wanadai magufuli ni mkali.alikamata meli ya wa Thailand Mara alibomoa Sheri ya mafuta.mara ni dikteta......hahaaaahahahaah yaaani reason za kitoto kupita kiasi aseeeee na unakutaaa jituu zimaaa LA chademaaa na mviiii zakeee linashabikiaaa uo upuuuzi
Acha hizo hizi si sababu za kitoto! Meli imelipwa zaidi ya bilion 3 na huko mwanza mwenye kituo cha mafuta alilipwa fidia billion 2 ! Hizi ni sababu za kitoto? Pesa hizi zingeweza kujenga zahati na kununua madawa pia kununua madawati na kuwalipa walimu haki zao, Magufuli si mwadilifu ni mtu wa kukurupuka sana na ukurupukaji wake ndiyo umelitia Taifa hasara kibao zikiwemo za kusitisha hovyo mikataba ya makandarasi na matokea yake wakishinda kesi wanalipwa mabilioni, nyumba za Serikali , kivuko feki, na billion 251 zimeyeyuka wizara ya Ujenzi kwa njia za ufisadi.
 
Yaani nimekuja mbio niwaone hao waliotajwa lol....aibuu si bora akae kimya tuuu....
 
Hao mafisi hadi waliopo kwake wana nguvu kubwa kuliko yeye.Akibahatika atanywea tu maana hata polopesa alisema hana ubia na mtu lakini walimnyoosha na wanamnyoosha tu!😀😀

Awataje waliofirisi TTCL , ATC , msshirika ya umma , walionunua mabehewa feki na wizi bandarini na Escrow.
 
Kabla ya kuwataja yeye mwenyewe ajitizame kwanza yupo safii?
 
Duuu, hii kweli sanaa! Kama magazeti ya udaku. Habari ndefu but no facts
 
mimi nashangaa hawa wasomi wanaoimba Lowassa ni fisadi..
lakini hawatuelezi ameiba kwenye account gani na ni kiasi gani na kwa ushahidi upi ?
Kama ni richmond basi mtueleze kamati ya bunge ilikula shilingi ngapi,Waziri Karamagi alikula shilingi ngapi na Waziri mkuu wa kipindi hicho kama nae kuna hela alikula ?
nashangaa wanamsahau huyu fisadi alieisababishia Wizara ya ujenzi pekee hasara ya trilioni 1.3 !
 
Huyu mzee wa kukurupuka tu hata hajielewi. Anadhani suala la kudhibiti ufisadi ni sawasawa na kupiga push up jukwaani!
Na ikitokea bahati mbaya akashinda urais huyu mzee atakuwa kwenye wakati mgumu sana, kwani kwa upande mmoja amewaaminisha wananchi kwamba ana uwezo wa kufanya mambo mengi sana, na kwa upande mwingine atakumbana na ile hali halisi ya mfumo, sasa hapo ndio itabidi lazima akubaliane na jambo mojawapo kati ya hayo mawili. Akubali kudhibitiwa yeye na mafisadi ama akimbie urais ili wananchi wamwelewe kwamba kweli alikuwa na nia ya dhati kutumikia wananchi.
lLakini bahati nzuri ni kwamba urais atausikia kupitia tbccm.
 
Back
Top Bottom