Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Hivi kosa ni nini?
Kosa ni hilo LA umeme,watupishe na serikal yetu sikivu,huu sio muda wa kuumiza wananchi,nchi hii watu sijui wanasomea nini darasani gesi IPO wanambwelambwela na bei. na wewe Ewura subiri tuvute pumzi.GOOD ENOUGH MY PRESIDA
 

Mambo mengine ni juu sana ya uwezo wako kujadili. Kama Economics za Tanesco hauzijui, basi ujue kwamba mlizitengeneza makusudi mjinufaishe na miradi. CCM ilisaini IPTL ofisini Lumumba. Yanawatokea puani, mnaanza populist politics kuwalaghai wananchi mpo upande wao. Nonsense!
 
Mkuu, mimi nimeweka hilo baada ya kuona kuwa Magufuli amelenga kutafuta mtu pale CoET. Sasa nimeangalia kwa wale waliobaki nikaanza ECSE nikaja kule mining nikaenda Civil kisha nikamalizia na MECHE. Ukweli kwa Mwinuka sijui kaona nini. Pale walau Mgwatu sikuwa na shida na uteuzi wake. Sasa ukiangalia kote huko kiukweli aliyekuwa afadhali ni Kimambo ingawa kweli ule mradi ulikufa chini yake ila alikuwa na majukumu ya kuongoza CoET na kwa uzoefu kamuacha mbali sana Mwinuka. Naona hata Mwinuka huko aliko ameshangaa na najua mpaka sasa haamini kile kilichotokea. Nimejaribu kumcheki kwenye namba yake ya tigo hapatikani ila nitamtafuta tu nijue amepokeaje uteuzi huu!! Ila kwa CoET aliyebaki afadhali baada ya kuondoka kina Mgwatu ni Kimambo na anajua kuongoza sema ndo hivyo tena!! Mwinuka hana maamuzi kabisa na ni mtu wa ndiyo mzee... Ila bila kuficha Kimambo ni mpinzani mkubwa wa CCM. Mwinuka na Mgwatu ambao ndiyo walioonekana na Magufuli ni makada wa kutupwa wa CCM. Labda hicho ndicho kigezo kilichotumika!! Ngoja kwanza nimtafute tena Mwinuka!!
 
Kwa mwendo chuo cha UDSM ndo maana kinakufa na kupotea kitaaluma. Muda si mrefu kitakuja kuporomoka si kawaida maana PHD holders na wahadhiri ndo hao wanaondolewa,.. Hivi watapata muda wa kufundisha lini? Watapata wapi muda wa kufanya tafiti?
 
ktk gvt hii ukipewa power huna mamlaka ya kutumia power hiyo, mpaka umuulize bosi!
 
Toka alipoteuliea mramba kwa maoni yangu na kwa mara ya kwanza niliona tanesco wakifanya vizuri kwenye kutoa huduma kuliko wakurugenzi wote waliopita,,zile kelele za uooooo tulishazisahau ila si muda mrefuu zinarudiii
 
Nachelea kuendelea kujadiliana na wewe lakini ni wazi humfahamu Mwinuka kama unavyotaka kujiaminisha hapa. Hata huyo Kimambo humfahamu. Mi pro UKAWA( nisome mabandiko yangu yote). Nimefanya kazi ka karibu na wote Kimambo na Mwinuka. Hamna ukweli unaousema hapa. Tuishie hapa mkuu.
 
For the sake of public interest, Magu is still the best president.

gharama za umeme zinaumiza...
 
kitaalamu yaelekea kuna tatizo Tanesco. Yaelekea inakufa na tai shingoni aiingii akilini, wataalamu wa tanesco walikaa na kuona wanaendesha kwa hasara wakapeleka gharama zao Ewura nao wakakubali kwamba kutokana na mahesabu waliopelekewa bei ya umeme inahitajika kupanda. wakati yote yanafanyika ninaimani kwa asilimia kubwa kwamba waziri alikuwa na taarifa . Haiwezekani bei kupandishwa bila waziri husika kuwa na taarifa au imekuwa kama ile ya machinga wa mwanza? au waziri alitaka itangazwe ili apate kiki ya kuzuia?. NI MAWAZO TU!
 
Toka alipoteuliea mramba kwa maoni yangu na kwa mara ya kwanza niliona tanesco wakifanya vizuri kwenye kutoa huduma kuliko wakurugenzi wote waliopita,,zile kelele za uooooo tulishazisahau ila si muda mrefuu zinarudiii
Umeme na maji viliacha kukatika katika mara tu baada ya Magufuli kuwa rais
 
Acha awanyoshe maana hawasikii bado Ewura
 
Mkuu,ni kweli znanyesha?
ahahahahahha mtalima sana nyie.huyu si nasikia ni kati ya wale ambao mkulu analalamika kunawatu wanaficha pesa!!!!! ndo mana kuna ukata
 
Kosa ni hilo LA umeme,watupishe na serikal yetu sikivu,huu sio muda wa kuumiza wananchi,nchi hii watu sijui wanasomea nini darasani gesi IPO wanambwelambwela na bei. na wewe Ewura subiri tuvute pumzi.GOOD ENOUGH MY PRESIDA
Vingapi viko bei ya juu na wanyonge mnaojifanya kuwatetea wanakufa kwa kuvikosa na ni vya serikali?
 
Hii sirikali ya 🙄mwendokasi.🙁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…