Mkuu, mimi nimeweka hilo baada ya kuona kuwa Magufuli amelenga kutafuta mtu pale CoET. Sasa nimeangalia kwa wale waliobaki nikaanza ECSE nikaja kule mining nikaenda Civil kisha nikamalizia na MECHE. Ukweli kwa Mwinuka sijui kaona nini. Pale walau Mgwatu sikuwa na shida na uteuzi wake. Sasa ukiangalia kote huko kiukweli aliyekuwa afadhali ni Kimambo ingawa kweli ule mradi ulikufa chini yake ila alikuwa na majukumu ya kuongoza CoET na kwa uzoefu kamuacha mbali sana Mwinuka. Naona hata Mwinuka huko aliko ameshangaa na najua mpaka sasa haamini kile kilichotokea. Nimejaribu kumcheki kwenye namba yake ya tigo hapatikani ila nitamtafuta tu nijue amepokeaje uteuzi huu!! Ila kwa CoET aliyebaki afadhali baada ya kuondoka kina Mgwatu ni Kimambo na anajua kuongoza sema ndo hivyo tena!! Mwinuka hana maamuzi kabisa na ni mtu wa ndiyo mzee... Ila bila kuficha Kimambo ni mpinzani mkubwa wa CCM. Mwinuka na Mgwatu ambao ndiyo walioonekana na Magufuli ni makada wa kutupwa wa CCM. Labda hicho ndicho kigezo kilichotumika!! Ngoja kwanza nimtafute tena Mwinuka!!