Leo 1.1.2017 Prof. Muhongo amehojiwa na Radio One na kueleza sababu za kusitisha mpango wa EWURA wa kupandisha bei ya Umeme kwa 8.5% kama ifuatavyo: -
1. Kwenye mikutano ya 'public hearing' nchini kote wadau walipinga myongeza ya bei;
2. hadi jana 31.12.2017 EWURA, kinyume na matakwa ya sheria, haikuwa imepeleka ripoti ya uamuzi wake kwa waziri mwenye dhamana, kujadiliwa na kupitishwa/kuthibitishwa kabla ya kutangazwa kwa pendekezo la bei mpya;
3. Ufumbuzi wa matatizo ya kifedha (madeni) wa TANESCO hauwezi utatuliwa kwa kupandisha bei ya Umeme. TANESCO inatakiwa kuwa na mkakati wa ku-improve efficiency kwenye management yake badala ya kuongeza bei ya Umeme; na
4. Wakuu wa TANESCO hawawpaswi kulipana bonus kila mwisho wa mwaka kiasi cha kufikia Tzs. 60m/- kwa mtu mmoja wakati shirika linashindwa kujiendesha isipokuwa kwa kupandisha bei ya Umeme. Hii inamaanisha kuwa wananchi wakamuliwe ili ipatikane pesa ya mabosi wa TANESCO kulipana bonus! Prof. Muhongo amesema ameagiza hata hiyo bonus isilipwe au irudishwe kwa waliokwisha kulipwa.