Elections 2010 Magufuli atoa rushwa kuisaidia CCM Igunga

Elections 2010 Magufuli atoa rushwa kuisaidia CCM Igunga

mi nafikiri wanaigunga wangemwuliza huyo waziri wa magamba alikuwa wapi miaka yote?kwanini hakujenga hilo daraja?
 
hivi tunatimiza miaka 50 ya uhuru na hilo daraja halikujengwa na serikali iliyokuwa madarakani ni hiyo hiyo ya ccm mi sioni kipya hapo nyie wananchi wa igunga amkeni kuna ahadi kibao tangu 2005 hazijatekelezwa, hiyo ni danganya toto kazi kwenu
 
Yuko wapi ritz aka mwita25 aka rejao, kishongo aka philanderer atetee matumbo?

Hivi mkuu umeshagundua siku akikosekana mmoja wanakosekana wote eh? Ina maana ni one man, million IDs...
 
leo taarifa ya habari ya itv imemuonyesha waziri magufuli akitoa ahadi kibao za ujenzi wa madaraja na makalvati huko igunga akiwa pamoja na naibu waziri wa maji ambaye naye katoa ahadi zake ,
hivi jamani hawa watu wameenda kama makada wa magamba au mawaziri wa serikali? Na kama wameenda kama makda wa ccm je hii si rushwa ya mchana kweupe?

hata ungekuwa wewe chama chako ungekipigia debe tu..ccm ni kama mama mama yako hata akiwa kichaa huwezi kumkata na kufanya hivyo ni laana maishani
 
anadhani kwa kuitwa igunga ataingizwa kwenye mtandao wa jk akidhani anasafisha nyota yake baadae aje apendekezwe kugombea urais kupitia magamba anajidanganya tu,anadanganya wana igunga kwa kuahidi barabara za lami ni mwongo huyo mkataeni.
 
Nitawalaani sana wapiga kura wa Igunda wakikubali kudanganyika tena na tena. Je ina maana tangu waanze kuwachagua viongozi kutoka ccm hawajawahi kuahidiwa kujengewa barabara, madaraja na kupatiwa maji? Kama walikuwa wakipewa ahadi hizo ni kwa nini mpaka leo hazijatekelezwa? Katika uchaguzi huu walitakiwa kuwa wanasikia ahadi mpya maana za miaka hiyo zinatakiwa ziwe zimeshafanyiwa kazi.
 
Ile sheria ya gharama za uchaguzi walishaigalagaza siku nyingi, walipoona imemshinda ****** siku hizi wameiacha kabisa, inasubiri kufutwa tu
 
Ile sheria ya gharama za uchaguzi walishaigalagaza siku nyingi, walipoona imemshinda ****** siku hizi wameiacha kabisa, inasubiri kufutwa tu

Takukuru mnasemaje rushwa za aina hii, bajeti na mipango ya maendeleo hupitishwa na bunge la jamhuri ya muungano hii ya magufuli imepitishwa na nani kama si rushwa ni nini basi? Dk hosea kazi kwako
 
Serikali na nchi kwa sasa hatuna dira ya tunakotaka kwenda na wamekalia uchaguzi na uongo mwingi Igunga. Hatuna hata low hanging targets zitusogeze kwenye maendeleo na tumebakia kuwekeza kushinda uchaguzi Igunga wakati wanafunzi wa vyuo wanakosa mikopo na mengine mengi yamekwama. Tatizo lipo vichwani mweti watanzania na inatibidi tubadilishe mitizamo yetu na fikra
 
Basi hakuna jinsi! kilichobaki ni wewe kuendelea na maombi ili Mungu amtangulize mbunge wako mbele ya haki ili upate hizo barabara nzuri,maji safi na pia upate msaada wa chakula mapema ili nduguzo kule Matombo wasife mapema,CCM wametoa na CHADEMA WAMETWAA Ashukuriwe Rostam
 
Leo taarifa ya habari ya ITV imemuonyesha waziri Magufuli akitoa ahadi kibao za ujenzi wa madaraja na makalvati huko igunga akiwa pamoja na naibu waziri wa maji ambaye naye katoa ahadi zake ,
Hivi jamani hawa watu wameenda kama makada wa magamba au mawaziri wa serikali? na kama wameenda kama makda wa CCM je hii si rushwa ya Mchana kweupe?

Sasa hutaki madaraja na makaravati na maji wapewe watu wa Igunga? Hongera Magufuli kwa kutoa ahadi hizo kikubwa tu zitimizwe kwa wakati! Mbona mgombea wa Magwanda anasema nikiwa mbunge wa Igunga wasipo jenga daraja tuta andamana jimbo lote! Magufuli endelea na kampeni kwa nguvu zote Igunga!
 
Nitawalaani sana wapiga kura wa Igunda wakikubali kudanganyika tena na tena. Je ina maana tangu waanze kuwachagua viongozi kutoka ccm hawajawahi kuahidiwa kujengewa barabara, madaraja na kupatiwa maji? Kama walikuwa wakipewa ahadi hizo ni kwa nini mpaka leo hazijatekelezwa? Katika uchaguzi huu walitakiwa kuwa wanasikia ahadi mpya maana za miaka hiyo zinatakiwa ziwe zimeshafanyiwa kazi.

Imeandikwa atakaye mlaani mwenzake basi yeye ata laaniwa mara mia zaidi! Usifanye hivyo dada magwanda uta laaniwa na magwanda yako,sawa dada mweupe!
 
Na nyie waandishi wa habari mtalaaniwa pia dada MwaJ mmechukua hela kote Chadema,CUF na CCM mnakua double standard sana waandishi wa bongo! Acheni njaa zenu bana!
 
Magufuli nae mbona najivunjia heshima? Hivi kwanza atuambie yuko likizo au? Maana hata gari alilokwenda nalo ni la serikali< dereva analipwa posho, mafuta n.k! Pia kula lile jibaba la kulala bungeni TYSON limepiga kambi Igunga! Sijui ofisi kamwachia nani! Yeye pia anatumia nyenzo za serikali! Tunaomba walipa kodi mtuambie!
 
Kwann wasingejenga kabla ya kampen? Wajinga ndo wamedanganywa na kukubali rushwa!
 
Nampenda Magufuli naipenda CCM! Magufuli for 2015! Igunga msimwangushe Magufuli! Kwanza mna bahati kubwa sana Rais wenu wa 2015-2025 amekuja kuwambieni ukweli wa mambo! Hakika atatimiza hizo ahadi za barabara na Madaraja namfahamu vizuri John Pombe Magufuli! Igunga for CCM!
 
Imeandikwa atakaye mlaani mwenzake basi yeye ata laaniwa mara mia zaidi! Usifanye hivyo dada magwanda uta laaniwa na magwanda yako,sawa dada mweupe!

Potelea mbali na iwe hivyo! Magamba yanakera na ahadi zao hewa kila uchaguzi.
 
Back
Top Bottom