Magufuli hapendelei kabisa Michezo na Burudani

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Mgombea urais wa CCM John Magufuli hana historia yoyote katika maisha yake hususani toka awe mwanasiasa ya kujihusisha na mambo ya sanaa, burudani na michezo.
Hakuna kumbukumbu zozote kzinazomuonyesha John Magufuli akishiriki matukio muhimu ya sanaa na burudani hususani mchezo wa soka, Muziki nk.
Hana tofauti kubwa sana Benjamin Mkapa ambaye kipindi cha uongozi wake suala la michezo halikuwa kipaumbele chake kabisa, na hata Mkapa mara kadhaa alipohojiwa kuhusu nini anachofahamu na kilichokuwa kinaendelea katika mchezo wa soka nchini alisema hajui chochote zaidi ya kusikia mizozo na migogoro tu. Pamoja na yote hayo bado Mkapa aliacha kumbukumbu kubwa katika michezo kwa kuwezesha kujengwa kwa uwanja mpya wa kisasa wa Taifa.

Hali hii ya Magufuli ni tofauti kabisa na Mtangulizi wake, Jakaya Kikwete ambaye alikuwa ni kinara katika kujihusisha na mambo ya burudani na michezo kabla ya kuteuliwa na CCM Kugombea urais na hata baada ya kushinda urais, jambo ambalo Mzee Ally Hassan Mwinyi pia alikuwa akilifanya.

Hili la Magufuli limejidhihirisha wazi hivi karibuni baada ya Magufuli kuwasili mjini Zanzibar na kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu ushabiki wake katika mchezo wa soka na hapo alijibu kuwa hana timu yoyote anayoishabikia zaidi labda ataishabikia Timu ya Taifa ya Tanzania.
Yote kwa yote Magufuli siku ya jana alialikwa na TFF kwenda uwanja wa taifa kufungua mashindano ya Kombe la Kagame, lakini pasipo kutegemea Magufuli hakudhuria katika ufunguzi huo tena bila kutoa taarifa kwa TFF waliomualika na badala yake aliendelea na ratiba ya shughuri zake za kisiasa mkoani Mwanza.

Huenda huu ukawa mwanzo mgumu kwa sekta ya michezo na tasnia ya sanaa nchini ambayo ilishaanza kuzoea na kubweteka kuwa wao ni watu muhimu na wa thamani sana kwa kuwa rais anayeondoka madarakani Jakaya Kikwete alikuwa karibu nao sana lakini mategemeo kwa mtu anayetaka kuchukua nafasi ya Kikwete hana muda kabisa na michezo na burudani.
 
Mkaribishen betting uone n okwi wa betting
 
Acheni hizo. Kwani hiyo ni primary qualification? Besides, michezo sio kipaumbele
 
Unaofuata ni utawala wa kunyoosha vilivyo pinda pia sio utawala wa kikwete zingatia hayo
 

jibu jepes sana,usiumize kichwa,angalia chimbuko lao
 
Ndio vizuri aliyekuwa anapenda michezo ni mwizi. Alikuwa anafuga majambazi sugu Ikulu ili kupotezea.
 
Uwanja wa Taifa uko ndani ya barabara! Inabidi uvunjwe bila fidia! Raid ajaye anafuata sheria! TANESCO la UBUNGO alishasema lazima livunjwe kama si Leo ni kesho! Hiyo kesho itafika siku ameapishwa! Vituo vya mafuta morogoro road vingi vipo ndani ya eneo la barabara vikae mkao wa maumivu! Je nani atauzuia mkono wa Tingatinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…