Elections 2015 Magufuli: Hatujaahidi kwenda mwezini, ahadi zetu zinatekelezeka

Akizungumza na watanzania kwanini wamchague yeye kuwa rais wao Dkt. Magufuli ameonekana mtu anayemaanisha kile anachokizungumza ameaahidi yafuatayo:-

Ninao uwezo, ujasiri na maarifa ya kubadilisha mfumo wa uongozi na utendaji ili uwatumikie zaidi wananchi na uwezeshe uwajibikaji wa viongozi ambao si waadilifu. Maagizo haya yapo kwenye ilani yetu ya 2015-2020 na nimejiandaa kuyasimamia kwa dhati kabisa.

Nitajenga utamaduni mpya wa viongozi kuwajibika kwa matokeo ya kazi tunazowapa. Nawahakikishia sitachelewa wala kusita kuwaweka pembeni viongozi na watendaji watakaokuwa wanatuchelewesha katika kutimiza ahadi zetu kwa wananchi.

Nitahakikisha tunakuwa na mpango kazi madhubuti wa kutekeleza ahadi zetu kwa kazi na wakati pamoja na kuwa tunawajulisha wananchi kila hatua ya utekelezaji.

Natambua ajira ni tatizo la kidunia lakini serikali yangu lazima ikabiliane nalo tena kwa ufasaha sana. Awamu yangu itakuwa ya viwanda. Ambapo serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi Tutajenga viwanda kwa usindikaji wa samaki mwambao wa bahari ya Hindi,Ziwa Victoria na Tanganyika; Tutajenga viwanda vya saruji; nyuzi,nguo na magunia; Nyama na bidhaa za ngozi; pembejeo za kilimo; kufufua viwanda vilivyokufa au kudorora na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika ujenzi wa viwanda.

Tumekuwa tukipambana sana kuona tunajitegemea kibajeti mfano mwaka 2005 bajeti yetu ilikuwa inategemea misaada kwa 34% na leo bajeti yetu 2015/2016 inategemea misaada kwa 8% tu.

Awamu yangu tutahakikisha tunajitegemea kamili. Natambua ili tujitegemee lazima tukusanye kodi kwa ufanisi; leo tunakusanya bilioni 900 kwa mwezi toka bilioni 175 kwa mwezi 2005 awamu yangu itakusanya zaidi.

Tutapunguza misamaha ya kodi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili fedha nyingi zaidi ziende kwenye miradi ya maendeleo.

Tutazipitia upya tozo za kodi ili ziwe kwenye kiwango ambacho watu wengi zaidi watalipa kodi na kwa hiari pamoja na kuitaka TRA kuweka utaratibu rafiki kwa walipakodi wenye malimbikizo. Ikiwa hivyo na serikali tukaisimamia vyema hakika Taifa hili litapaa kimaendeleo.

Uhakika zaidi wa mapato ndiyo unaotufanya tuseme watoto wetu watasoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne bure pamoja na kuimarisha miundombinu ya kitaaluma kama madarasa, madawati, vitabu, vyoo, na nyumba za walimu pamoja na kuwalipa vizuri ili wafundishe kwa ari zaidi.

Utawala wa Rais Kikwete umejenga vyuo vikuu vikubwa viwili UDOM na Nelson Mandela Arusha. Awamu yangu ilani inaelekeza serikali kujenga viwili pia mbavyo ni Chuo Kikuu Cha Kilimo na Sayansi Shirikishi cha Mwalimu J.K.Nyerere Butiama mkoani Mara na Chuo Kikuu Cha Sayansi za Madini mkoani Shinyanga.

Pamoja na kukamilisha ujenzi wa chuo kikuu cha Afyana Sayansi tumizi cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Tutakamilisha kwani elimu ya juu ina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya taifa letu.

Serikali yangu pia itaendelea kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kujenga hosteli za kutosha kwa wanafaunzi waliopo katika vyuo vya umma ili wasome kwa utulivu.

Natambua nchi yetu ya Tanzania ina utajiri mkubwa wa rasilimali. Lakini nchi kuwa tajiri kwa rasilimali sio sifa. Sifa ni kwa wananchi kuwa matajiri kutokana na rasilimali hizo kupitia mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali ili jitihada zao za kujiendeleza ziwanufaishe zaidi.

Ninawahakikishia nitaangalia upya utaratibu wa uvunaji rasilimali zetu ikibidi kupitia upya sheria zetu ili wananchi wanufaike zaidi. Pia nitahakikisha watanzania wanashiriki katika uvunaji na sio kuwa vibarua bali kama wamiliki na wawekezaji na kuona mikataba inalinufaisha taifa.

Kwa kutambua rasilimali asili hizi huisha na bei zake hubadilika kila wakati tutazitumia vizuri kwa maendeleo ya wananchi hususani kujenga rasilimali watu imara katika sekta muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi wa taifa letu kama Afya,Sayansi na Teknolojia, Gesi, mafuta, madini na Uchumi pamoja na Masuala ya ulinzi.

Mimi ni miongoni mwa watu wanaoumizwa sana na hali ya kukosekana kwa dawa na vifaa tiba hospitalini pamoja na huduma za kiafya kupatikana mbali na makazi ya wananchi.

Nawahakikishia najua tunaweza kuboresha hali hii kwa kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba pamoja na kujenga vituo vya afya, hospital za wilaya na hospital za mikoa na za rufaa za kanda.

Najua mtauliza nitawezaje, ndugu zangu naomba mniamini nchi yetu ni tajiri nitabana mianya kwa kufunga makufuli yangu ili pesa ziende kuwahudumia watanzania wanyonge.

Nimetumika serikalini kwa miaka 20 bila kupewa onyo, kusimamishwa wala kufukuzwa nawahakikishia sitakuwa na mzaha wala uvumilivu na watendaji wazembe ,wabadhirifu na wanaoendekeza urasimu.

Nawahakikishia nitajenga utamaduni mpya wa uwajibikaji. Kutakuwa hakuna kubebana wala kujuana. Nitaimarisha mfumo mzima wa utumishi wa umma ili kuiwezesha serikali kuwatumikia vizuri zaidi wananchi.

Usafiri wa anga ni muhimu kwa uchumi wa nchi yetu hususani katika kukuza biashara na utalii. Kwa kuzingatia umuhimu wake nawahakikishia nitafufua na kuliboresha shirika letu la ndege kwa kununua ndege mpya na kuuboresha mfumo wake wa utendaji ili uwe wa kibiashara zaidi ili lijiendeshe kwa faida.

Hili linawezekana maana Tanzania ni tajiri ndugu zangu niaminini. Pia, tutazifufua na kuboresha usafiri wetu wa reli ikiwa ni pamoja na kujenga reli mpya ya kisasa kwa ajili ya usafiri wa treni ya umeme. Inawezekana naomba mniamini ndugu zangu nchi hii ni tajiri.

Nawaahidi utumishi uliotukuka, uadilifu na uchapakazi.

Mtarajie serikali itakayokuwa inafanya maamuzi sahihi, kwa wakati sahihi na utekelezaji sahihi lakini kwa haraka.

Mtarajie uongozi wa kidemokrasia lakini uwepo wa nidhamu serikalini na jamii nzima. Nitaruhusu demokrasia inayojali na kuthamini maendeleo na ustawi katika maisha ya wananchi wetu zaidi.

Nitasimamia utawala wa sheria hakuna mtu atakayekuwa juu ya sheria na hakutakuwa na mzaha wala majadilano katika kufuata na kutii sheria za Nchi.

Nitapenda kuona serikali inachapa kazi na wananchi wanachapa kazi tu basi!

Nitalinda umoja, amani na usalama wa Nchi yetu kwa nguvu zote.

Nitatumia maarifa yangu, uwezo wangu na vipaji vyangu vyote na kumtanguliza Mungu wakati wote kutetea maslahi ya Tanzania katika dunia ya leo kwa kuyaenzi mema yaliyofanywa na watangulizi wangu.

Nitahakikisha serikali yangu wakati wote inasimamia uadilifu ili kuendelea kuijengea heshima nchi yetu kimataifa.

Nitaimarisha uhusiano na Nchi zingine lakini nitatumia muda wangu mwingi ndani ya nchi ili kuharakisha maendeleo ya watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maguf

Magufuli ni tapeli mkubwa ( a gingatic conman) ambalo halina hata ujuzi wa kupaka rangi maneno. Ni mropokaji na mweny upeo mdogo sana wa diplomasia. Miguvu ndo kinga anapoishiwa pumzi na kuwekwa "mtu kati!" Hakuna cha viwanda (labda vya kuweka maiti mitoni),mikopo shida,kodi lukuki,midege hasara tupu,maisha magumu kila kona,biashara zinashuka na deni linafura .
 
Alihaidi atawashughulikia wapinzani kila MTU yu shahid nadhani ndio vipaumbele vyake kwanza ili uchumi ukue.
 
Huyu bwana ilitakiwa aishie kwenye mabarabara ndio level ya mwisho kule ndo nguvu inatakiwa.
 
Maguf

Magufuli ni tapeli mkubwa ( a gingatic conman) ambalo halina hata ujuzi wa kupaka rangi maneno. Ni mropokaji na mweny upeo mdogo sana wa diplomasia. Miguvu ndo kinga anapoishiwa pumzi na kuwekwa "mtu kati!" Hakuna cha viwanda (labda vya kuweka maiti mitoni),mikopo shida,kodi lukuki,midege hasara tupu,maisha magumu kila kona,biashara zinashuka na deni linafura .

Wewe Jinga kweli. Soma ahadi na angalia utekelezaji. Zingatia ya nyuma na angalia muda Wake na historia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom