Magufuli hayupo kipi kinawafanya CHADEMA kuliachia hewani suala la Wabunge 19 wa Viti Maalum?

Magufuli hayupo kipi kinawafanya CHADEMA kuliachia hewani suala la Wabunge 19 wa Viti Maalum?

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
16,950
Reaction score
13,527
Friends and Enemies, Greetings!

Hatuwezi endelea kuishi katika kivuli cha lawama kwa mwendazake hasa katika mambo ambayo yeye aliyafanya huku akiamini kwamba huenda alikuwa anaijenga Tanzania ya ndoto yake.

Binadam tumeumbwa kusahau, ila kama nchi tutakuwa tunafanya makosa sana kusahau japo kwa sekunde moja uvunjaji wa sheria uliofanyika katika suala la wabunge wa Chadema hawa covid 19 ambao kiukweli siyo tuh sakata hilo limevunja katiba, bali pia linafuja pesa zetu za jasho la kodi yetu.

Kuna kila dalili kwamba suala hilo lilipata baraka kutoka kwa mwendazake na Job Ndugai akatumika kama rubber stamp ya kuhitimisha suala hilo kibabe bila kujali katiba, wala sheria huku akijua kuwa ana backup ya Dola.

Swali kwa Mbowe na Chadema kwa ujumla, ni kipi kinawafanya waendelee kusugua miguu chini juu ya suala hili? Je, wana matumaini kuwa Job Ndugai atameza matapishi yake na kurud nyuma akatenda haki?

Pili, let's say walikuwa wanahofu ya mkono wa chuma wa mwendazake, mwendazake sasa keshaondoka, hofu yao ni nini kufanya mobilization kwa wanachama wake?

Mbowe na Chadema wako kwenye mission ya kuhamasisha katiba mpya; siyo jambo baya na ni kweli tunahitajio,Ila hili la Covid 19 mbona hatuliskii Tena?wameshalishana yamin tayar na hawa wabunge wao?

Tuanze na Kitila Mkumbo, Zitto kabwe, Halima Mdee, Patrobas Katambi, Peter lijualikali, Vicent Mashinji, Mwita Waitara, Joshua Nassari, Wibroad Slaa na wengine wengi, ni watu ambao kwa namna moja ama nyingine wamepita kwenye MIKONO ya Mbowe na Chadema.

Lakin ondoka ondoka yao kutoka chadema na kuchukuliwa na CCM kunaacha maswali mengi Sana kwetu sisi wananchi, nayo ni:

1. Either mbowe ni mjinga sana.

2. Mbowe ni mwerevu Sana ila anasalitiwa na hawa jamaa huku akihujumiwa na Dola.

3. Mbowe ni sehemu ya Dola,I mean he's party and parcel of a big project.

4. Au Mbowe anatengeneza mapinduz indirect way kwa kuwatumia hawa hawa jamaa zake,kwamba anatuma jeshi lake kuwajoin Ili baadae aje kuwadestroy, sielewi.

Ukimya wake na chama chake na kuonesha dalili ya kuchoka kutolea majibu suala lenye ukakasi kama hili la Covid 19 kwa vitendo kunatia shaka Sana kuhusu nia ya dhati ya wapinzan katika kuongoza nchi hii.

Je,wanastahili kuchukuliwa seriously au CCM bado haijapata mbadala wake katika kuongoza Taifa hili.
 
Ni kweli kama chadema wako serious sana na wanataka mabadiliko wanayo ya hubiri ni wakati wa kufanya maandamano nchi nzima kulazimisha wabunge hao watolewe.
Namimi nawauliza wanaogopa nini?
Na kama wamepata nafas ya kuzunguka nchi maeneo karibu yote,kuhamasisha katiba mpya, wataweza vip kuitetea hiyo katiba mpya,na Ili hali hii ya sasa inavunjwa na wako weak katika kuitetea isivunjwe?
 
Hatuwalaum,swali letu kwao ni kwamba wao kama chama wameshakata tamaa tayar juu ya suala Hilo?
Mkuu unataka wakawatoe kwa nguvu bungeni? Aliyeapa kuitii katiba ndugai anachekewa tu, hata mama Kama mwenyekiti wa ccm anapaswa kumweka kitu Moto ndugai kwa kuvunja katiba. Hatuwezi kuwa na chama tawala viongozi wake andamizi wanavunja katiba waziwaz
 
Tumeambiwa tusilaumu tu bila ya kutoa maoni yako ili mwafaka ufikiwe au the best way forward,mtoa hoja unalaumu tu bila kushauri nini kifanyike, mazingira ambayo oppositions wanaendesha shughuli zao ni magumu mno hasa kutokana na KATIBA kuifanya ccm chama dola.President Samia ameonyesha kuwa wote sisi ni watanzania kwa kuruhusu vyama vya upinzani vianze shughuli zake,time will tell
 
Not exactly,je tuwaulize njia waliyotumia haijaleta positive outcomes,wamekata tamaa??kodi yetu inatumiwa vibaya kwa mgongo wa chama Chao sasa
Mkuu jukumu lao walishatenda, kilichofuata Ni kwa ndugai kuchkua hatua.huo Ni ukweli, hata ccm wakifukuza mbunge leo, spika hakuna haha ya chenga
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Unataka wafanyeje tena bwashee? Wapige bomu bungeni au?

Not exactly, je tuwaulize njia waliyotumia haijaleta positive outcomes, wamekata tamaa? Kodi yetu inatumiwa vibaya kwa mgongo wa chama Chao sasa
 
Tumeambiwa tusilaumu tu bila ya kutoa maoni yako ili mwafaka ufikiwe au the best way forward,mtoa hoja unalaumu tu bila kushauri nini kifanyike,mazingira ambayo oppositions wanaendesha shughuli zao ni magumu mno hasa kutokana na KATIBA kuifanya ccm chama dola.President Samia ameonyesha kuwa wote sisi ni watanzania kwa kuruhusu vyama vya upinzani vianze shughuli zake,time will tell

Wamepewa room ya kuonana na wananchi wao na wanachama wao, waitumie sasa kuhamasisha suala Hilo, kupaza sauti Ili utekelezaji ufanyike.

Wanakaa vip kimya?wanatuaminisha kuwa wameyamaliza kimya kimya na ruzuku wanachukua pia
 
Hao Covid-19 wanakula hela za watanzania si za Mh. Mbowe - kama watanzania mnamuona mtu mmoja anavunja katiba na anatamba bungeni kwamba hakuna cha kumfanya sasa mnataka Mbowe afanye nini zaidi ya anachowafanyia?

Masuala ya kudai mfumo mzuri wa utawala wa sheria ni wa kila mtanzania mwenye pumzi - si kazi ya Mbowe peke yake.

Kwa hao Covid-19 CDM imeshatimiza wajibu wake wa kuwatimua katika chama, na kama wanaendelea kula hela zenu watanzania hilo si tatizo la CHADEMA - tafuteni mchawi mhangaike naye na kama mnaona ni powa waacheni watusue.
 
Hao Covid-19 wanakula hela za watanzania si za Mh. Mbowe - kama watanzania mnamuona mtu mmoja anavunja katiba na anatamba bungeni kwamba hakuna cha kumfanya sasa mnataka Mbowe afanye nini zaidi ya anachowafanyia?

Masuala ya kudai mfumo mzuri wa utawala wa sheria ni wa kila mtanzania mwenye pumzi - si kazi ya Mbowe peke yake.

Kwa hao Covid-19 CDM imeshatimiza wajibu wake wa kuwatimua katika chama, na kama wanaendelea kula hela zenu watanzania hilo si tatizo la CHADEMA - tafuteni mchawi mhangaike naye na kama mnaona ni powa waacheni watusue.

Mkuu,lakin bado wanajitambulisha kama ni wabunge wa chadema bado hapo bungeni,inatuacha njia panda wananchi
 
Back
Top Bottom