Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane


Nimeisikiliza clip kitambo.

Ninapoandika kila neno lina uzito. Soma kila neno nililoandika kwa kituo.

Kama kuna kiingereza kimekupa shida omba msaada.

Ukiniuliza kama nimeisikiliza clip unanipa shaka kama umenisoma kwa kituo na kunielewa.
 



Magufuli nafikiri matokeo tu ya nchi ilivyo
sababu hata huo 'uchapakazi' wake kwa kuangalia tu barabara zilivyojengwa sijawahi kuelewa
why amekuwa branded 'mchapakazi'.... kuhusu priorities ....nafikiri kuna mengi sana ya kujadili kiasi kwamba
watu wengi wanaona kama ni 'kutwanga maji ndani ya kinu'...na ndo maana chochote kinachojitokeza kinadakwa tu hivyo hivyo hata kama sio big issue kulinganisha na mengine
 

On point the boss! Kwangu mimi elimu bora ni priority kwa nchi yetu. Kuna tafiti kadhaa nimezisikia kwamba oooh watoto level ya primary hawajui kiingereza n.k. n.k. kumbe mpaka Phd hili ni tatizo pia. Sasa kumjadili mtu ambaye ana Phd sentensi moja iliyonyooka ya kiingereza inampa shida na ameomba kutuongoza kwa miaka mitano ijayo bado ni sahihi kabisa kwani elimu ni kipaumbele.
 
Angekuwa mwanadada watu wangesema ni zile degree za chu.pi sasa huyu tusemeje? Hilo ndio linawatatiza wengi. Na likifahamika pengine litasaidia vijana wengine
 
Unajua kiongozi Mkuu kabisa wa nchi anatakiwa awe mfano kwa anaowaongoza. sasa huyu magufuli kama vitu vidovidogo vinamshinda ataheshimiwa na anaowaongoza? Hafahamu mambo ya kimataifa, hafahamu lugha, sasa huyu mtu alteuliwa kwa sifa gani? barabara km alivyosema Boss hapo juu ni mbovu zinabomoka baada ya nmwaka mmoja na zimetumia mabilioni ya shilingi. Eti mchapakazi, kivipi.? kwa huiyo tunachagua tu rais kwa sababu ni mchapakazi? Mbona wachapakazi wapo wengi tu? nao wanafaa kutuongoza? Magufuli hana hata sifa moja ya kuwa rais. Ni aibu tupu!
 
Kuna kila ushahidi mgombea urais ww ccm alikurupushwa kuchukua fomu bila kujiandaa,rais kwa dunia ya sasa ni lazima ujue habari za kimataifa kwa kujifunza ata kujisomea au kuangalia habari za kimataifa lakin kwa Magufuli hajui lolote kuhusu habari za kimataifa.

Kuhusu English najua kuna kuna watu mtasema mbona rais wa china,korea etc wanaongea lugha yao mkumbuke nchi hizo kuanzia chekechea hadi chuo wanajifunza kwa lugha zao na wanajitegemea sana.

Kwa hali ilivyo kwetu ya kutembeza bakuli Washington Dc inabidi rais awe anajua lugha maana kunakuwa na mikutano mingi ya kimataifa.

Wasuwasi wangu ile hotuba kama ya Idd Amin kwa Malkia wa Uingereza inaweza kujirudia tena.

Magufuli ni Dr mjue wa kusomea,angetakiwa kabla ya kugombea aende ata kwa rasi simba ampige msasa English course.
 
Lugha za kikabila anazojua hazina tija katika utandawazi wa dunia ya sasa kwa kiongozi wa kitaifa.
 

Magufuli yuko pale tu hii ni miaka mingine ya kikwete coz angesema anagombea tena ingekuwa issue. magufuli hajajiandaa hata kidogo anafikiri nchi ni baraaabara tu.Wakati ukusanyaji wa mapato ya ndani ndo nchi imara. Hapo anategemea kuomba kama Kikwete. Kuna bango moja limeandikwa magufuli king'amuzi kikwete remote nlifurai kweli wananchi wa sasa tunaona mbali. Wewe unategemea kuwa kiongozi mkubwa wa nchi unasema mkumchagua huyu mbunge wa ccm ntawaongezea kilometa kumi kipande cha lami ni akili iko kichwani au synovial fluid:wacko:
 

Tabby, I salute you for your great posts in this thread! We are speaking the same language.
 

Tabby, I salute you for your great posts in this thread! We are speaking the same language.
Ni kweli Tabby ametusaidia sana kufafanua ni kwa nini tunamshangaa Magufuli kutijua lugha aluyotumia kusomea elimu yake. Na ni ukweli kwamba tatizo la Magufuli si lugha tu bali ni kwamba hana upeo mpana wa uelewa. Na kuna uwezekano mkubwa hata anayoyaongea kakaririshwa tu na wala hajui anasema nini na wala ahadi anazotoa haelewi ataxitekelezaje! Kwa ufupi Magufuli hakujiandaa kushika hii nafasi. Ndio maana kikwete anatamani sana ashinde ili aendelee kuongoza nchi kwa mgongo wa Magufuli!
 
Kwa ualimu wa kemia na hisabati huhitaji sana kuwa mahiri wa lugha. Zaidi huwa ni vitendo. Cha msingi kama utaweza kumwelewa alokusidia kuongea its okey. Mbona wachina warusi wajerumani wajapani wanaongea broken na wako juu kimaendeleo
 
Kwa ualimu wa kemia na hisabati huhitaji sana kuwa mahiri wa lugha. Zaidi huwa ni vitendo. Cha msingi kama utaweza kumwelewa alokusidia kuongea its okey. Mbona wachina warusi wajerumani wajapani wanaongea broken na wako juu kimaendeleo

Mkuu soma post za juu utaelewa kwann watu wanalalamika
 
Nina hakika sio kuzungumza tu bali hata kusoma prepared text magufuli hawezi. Sidhani kama anaweza kupronounce maneno ya kiingereza walau yakafanana na kiingereza. Kwa hiyo wakuu kuna pia hii ishu ya kujiuliza, je Magufuli anaweza kusoma (prepared speech) kiingereza akaeleweka?
 
Magufuli..ana uelewa mdogo sana wa mambo..yeye anajua idadi ya km..na dagaa tu.. sijui atakua rais wa km na dagaa?
 
Kwa ualimu wa kemia na hisabati huhitaji sana kuwa mahiri wa lugha. Zaidi huwa ni vitendo. Cha msingi kama utaweza kumwelewa alokusidia kuongea its okey. Mbona wachina warusi wajerumani wajapani wanaongea broken na wako juu kimaendeleo

Naweza kuamini coz mimi ni mwalimu wa Chemistry A level,,kiukweli English hua inanipa tabu asee na wanafunz wangu wanajua lakini natumia mbinu ambazo zinawafanya wanaelewa kuliko hata walimu wanaojua English. Cjajua kwa upande wa Rais,ila itampa shida
 
Wengi mnaombeza Magufuli hata kiswahili kinapiga chenga...watanzania wako tayari kumchagua Magufuli asiejua kiingereza kuliko kuchagua fisadi papa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…