Tena wote wanaoamini uzushi huu kuwa lugha ya Kiingezeza ni tatizo, hawaelewi kuwa kuna Kiingezeza cha kuandika na cha kuongea. Mtu aliyefanya thesis yake ya Ph.D kwa Kiingezeza, akai defend kwenye jopo la wasomi, na ikapita, hawezi kuwa hajui Kiingezeza, ila linapokuja suala la Kiingezeza cha kuongea sio hoja, mtu kushindwa kuongea lugha ya watu wengine kwa ufasaha sio issue wala kuongea Kiingezeza kwa intonation ya Kisukuma haina tatizo lolote, nimehudhuria UN GA Kipindi cha Mkapa na JK, maraisi wa nchi zao wanahutubia UN GA kwa lugha zao na hotuba zao zinafasiriwa na wakalimani kwa zile lugha 4 za UN, hivyo ningependa kumsikia Rais Magufuli akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa Lugha ya Kiswahili.
P.