Tetesi: Magufuli na awamu iliyoua Biashara: Ngurdoto, Impala, Naura, Tours, Warithi waapa kuirudisha: Awamu 5 ilifilisi

Naona ni muendelezo wa kupiga hela tu
Kuna wakubwa wameingiza zile $ zilizofichwa
Wapo mafala ila sio wote, tunajua vitu viliuzwa ili kulipa madeni na mishahara eti leo wamerudi
Aliekuwa nyuma ya baishara hizi alifariki kwa hiyo mtoto kachimbua almasi kama ya yule jamaa eti
 
Ukweli ni kwamba, Wafanyabiashara wengi TZ janja janja za ukwepaji Kodi na deals chakaram ndio sehem ya Maisha yao.


Kwa aina ya Magufuli, Ilikua ni ngumu kwao kusavaivu.

Hivo Swala hapa sio Magufuli, Wala sio Utalii.!!.


Swala ni Ile Timu ,ndo ipo kazin ,kuirudisha kilichopotea baada ya Mirija Yao kuzibwa.
 
Hizi akili za kimasikini. Unataka serikali ihodhi pesa zote sekta binafsi isiwe na pesa? Serikali inatakiwa iachie pesa zizunguke mtaani. Sasa under magufuli, kandarasi za ujenzi- tba na Suma jkt. Mikutano a semina za kiserikali- aicc/madrasa ya shule. Kwa sera hizo eventually pesa yote inakuwa imehodhiwa na serikali, na mtaani kutakuwa hakuna pesa. Pia wivu wa kike muachage. Unaona wivu Mrema kutajirika, bila kufikiria aliajiri watu wangapi kwenye biashara zake.
 
Hili ndilo janga linaloia taifa.
Hii nchi ni maskini sana.
Hawa matajiri hawana huruma na MTU ni wabaya kuliko mashetani .
Kwa Sasa gharama za matibabu ni kubwa sana.
Gharama za maisha zipo juu. Serikali inashindwa kutoa huduma Kwa sababu wajanja wengi wameamua kuhujumu nchi Kwa kusingizio cha PPP.
Hakuna Kiongozi Mzalendo anayekubali fedha za umma zichezewe. KAZI ya serikali ni kufanya malipo Halali na kusimamia miradi yake Kwa thamani halisi.
Yaani watu wafanye kikao kimoja cha kujadili maendeleo ya watu Halafu watumie fedha nyingi kama nusu ya bajeti ya wizara kulipa Chakula na ukumbi na Malazi kwenye Hoteli ya Mwizi na jambazi mmoja eti ametoa ajira . MTU huyo huyo anawalipa wafanyakazi wake vimishahara vidogo ambavyo halipi Hata Kadi Wala NSSF Wala Bima ya Afya. Hizo ni ajira au ni upimbi.
Nchi yenye Wananchi wanaomiliki Ardhi na nyumba Zao binafsi Kwa zaidí ya 70% Kama Tanzania inahitaji Kiongozi Mzalendo Ili Wananchi wasije wakajikuta wanageuka kuwa watumwa wakati wanamiliki ardhi yenye rutuba na rasilimali nyingi.
Lazima serikali ilinde fedha za umma na kutoa huduma Bora Ili biashara zibaki Kwa Wananchi wenyewe . Waziri anayetaka kwenda Ngurudoto kunywa Bia moja sh. Elfu 10 na juisi glasi Sh. 8000 ,Chumba Sh. Lakini 5 na mchepuko wake aende Kwa pesa za mshahara anaolipwa na serikali na posho zake na si vinginevyo.
Lakini haya mambo ya kulipa ukumbi mamilioni Kwa Kodi za Wananchi Kwa kumfeva MTU mmoja na familia yake Wakati kuna Maukumbi ya Bure ya serikali ni ufisadi.

Tutampambania Makonda aendelee kuwanyoosha wale wezi wanaotaka kulifanya taifa hili kuwa ni Chuo cha kujifunza ufisadi.
Bahati NZURI Paulo Makonda alikiri Mbele ya Kaburi la Mzalendo MAGUFULI kuwa hatamsaliti na atakwenda Katika nyendo na njia alizomwachia .
Wakati Unaokuja utakua ni mgumu zaidí Kwa wezi na Mafisadi.
Ni Bora waachane na kujifariji Kwa mgongo Wa Awamu hii ya msimu.
Nguvu ya Wananchi Iko nyuma ya Wazalendo wale wanaouchukia ufisadi
 
Hotel hii ina ubia na msoga gang,na hizi kelele za magufuli kaharibu,ni ule upuuzi tu wa msoga gang.
Mkuu,

Haijalishi, ni dhahiri taarifa tuliyomezeshwa inaonyesha kufilisika kwa Biashara ya Ngurudoto kulisababishwa na mzozo wa kifamilia kuhusu mirathi na kutokuwepo kwa mikutano ya kiserika na mikutano ya kimataifa. ambayo ilikuwa sehemu kubwa ya mapato yao

Piki, hakuna ushahidi wa moja kwa moja au wowote ule unaoonyesha kuwa Hayat Rais alihusika na kufilisika kwa Hoteli hiyo.

Pepesa kote,IMF, WB, BOT, ADB, utaona hakuna sehemu inasema au kudai kuwa Uchumi wa Tanzania chini ya serikali ya Magufuli uliteremka pamoja nakuwa Uviko 19 ulisambaratisha chumi nyingi Duniani. Itoshe, sera zake zilizoonekana zingweza kuleta athari hasi,zilileta athari chanya. Hiyo ni kusema Uchumi wetu ulikuwa imara na hivyo any notion kwamba uchumi wa Tanzani ulikuwa mbovu na kusababisha kufilisika kwa Ngurudoto, is unfounded.

Tatu, huyu mleta mada sasa ameamua kutia mzozo na migogoro ya Familia ya Auaye Mrema kwenye siasa za majitaka, hiyo siyo sawa kabisa.

Hata hivyo, sio sahihi kusema kwamba serikali ya awamu ya tano ilifilisi Ngurudoto. Ni upotoshaji kwani hakuna ushahidi wa kuunga mkono dai lake kwenye bandiko kuu.
 
Magufuli alikuwa hatari sana kwa ustawi wa nchi na watu wa Kaskazini.
 
Hujui wewe
 
Thibitisha nisicho kijua, zaidi ya hapo ulishosema sio muhimu.

Kanywe uji upunguze hasira kwanza.
Nakunywa uji lishe ninvyoandika hapa na huwa sili maandazi na chapati..

Magufuli ameua biashara nyingi za watu hasa Arusha na Moshi kupitia kibaraka wake Sabaya na wengine. Kulikuwa hata na mpango wa kujenga East African road kuunganisha nairobi, Arusha, Mombasa na Moshi alipoingia Magufuli yote yalipigwa stop. Huyu mtu acha aende huko!
 
Kwani jpm yeye alikuwa anonea wivu kila mtu mwenye mafanikio? Basi yule jamaa Bora lilivyodead tu
 
mtu mwenye akili ataona hapa shida sio magufuli, yani hawa jamaa walitaka kujumilikisha wao hiyo mikutano na walipwe pesa nyingi huku serikali ikiwa inapoteza tu pesa hovyo
Pesa za mikutano ya Jumuiya zinatoka katika bajeti ya Jumuiya ya Africa Mashariki.
 
Kwani jpm yeye alikuwa anonea wivu kila mtu mwenye mafanikio? Basi yule jamaa Bora lilivyodead tu
Hamjui tu watu walivyokua wanapigwa pesa kizembe, mikutano ya watumishi hata kutoka wilaya Moja tu wao wanaamua kwenda kufanyia kwenye mahoteli ya kifahari huku wakiandikiana posho za kufuru

Kwa akili hizi za kutowabana watu serikalini maendeleo hatutayaona mpaka kiama, pesa ni zetu wananchi ila zikifika serikalini hakuna wa kuhoji, tunawaacha watumie wanavyotaka
 
Ukweli ni kwamba, Wafanyabiashara wengi TZ janja janja za ukwepaji Kodi na deals chakaram ndio sehem ya Maisha yao.
Hii inawezekanaje mkuu, km wahusika wanafuatilia vizuri? Nafikiri km ni lawama basi ziwe pande zote!
Lakini, je na zile zilizolipwa tunatumia vizuri?! SIAGI vipi?! 😄
 
Kumbe Magufuli ndio alisababisha wanafamilia wakaanza kugombea mali za hotel mpaka kugawana funiture……?

Hahaha hivi..toka amekufa huyo Magufuli sasa ni miaka mingapi?
 
Kumbe Magufuli ndio alisababisha wanafamilia wakaanza kugombea mali za hotel mpaka kugawana funiture……?

Hahaha hivi..toka amekufa huyo Magufuli sasa ni miaka mingapi?
Hao jamaa wapuuzi sana! Utafikiri ni matajiri sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…