Magufuli na Kenyatta walimaliza migogoro haya mengine yanatoka wapi?

Magufuli na Kenyatta walimaliza migogoro haya mengine yanatoka wapi?

hayaland

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
712
Reaction score
399
Nakumbuka marais hawa wawili waliwahi kuzungumza kwa simu hata kabla ya uchaguzi wa mwaka jana 2020 .Rais Magufuli alisema amezungungumza na Rais mwenzake wa Kenya mh Kenyatta na kuweka mambo sawa na kumwagiza waziri wa mambo ya nje wa Tanzania na wa Kenya kukutana mara moja Ili kusawazisha maelekezo waliopewa na maboss wao.Watanzania tuliamini kila kitu kimekaa sawa pamoja na tofauti zilizokuwepo kipindi cha nyuma tukaamini mambo yamekaa sawa sawa.

Tumesikia kuwa Kenya imepiga marufuku mahindi kutoka Tanzania kuingia nchini mwao kwa sababu mahindi hayo kutoka Tanzania yana sumu/ fungus inayojulikana kama Aflatoxins ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu na inaua. Na serikali imeagiza makamishna wa kaunti zinazozunguka mipaka ya Tanzania na Uganda na KBS kutekeleza agizo hilo.

Nimemsikia Naibu waziri wa kilimo Mh Bashe kuwa hawajapa taarifa za maandishi kuja serikali ya Tanzania juu ya swala hilo.Nipende kusema serikali ya Tanzania haiwezi kuletewa taarifa maana waliozuiwa ni mamlaka za ndani nchini Kenya.Hivyo ni ngumu serikali ya Tanzania kusubilia maandishi kutoka serikali ya Kenya.

Lakini mwisho wa haya ni lini?.Mungu ibariki Tanzania na majirani zake.
 
Hakuna mgogoro wowite bwashee!

Wakenya huja wao wenyewe kununua mahindi Tanzania hivyo hapo Namanga wanazuiana wao wenyewe!
 
Unaongelea mgogoro binafsi wa Magufuli na Kenyatta?au mgogoro wa Taasisi ya Kenya na Magufuli?

IMG_4245.jpg
 
Kwanza neno wowite bwashee manake ni nini?
Kwa hiyo wafanyabiashara ndyo wanaolinda mpaka hivyo wanajizuia wenyewe?
Hakuna mgogoro wowite bwashee!

Wakenya huja wao wenyewe kununua mahindi Tanzania hivyo hapo Namanga wanazuiana wao wenyewe!
 
Mtoa UZI acha kiherehere subiria tamko la serikali
 
Back
Top Bottom