Magufuli na Serikali yako hamaki yenu inampandisha chati Lissu

Lisu amehamaki kivipi mkuu?

Magufuli kapiga marufuku habari za Lisu kwenye vyombo vya habari lakini ndio kwanza wananchi wanazidi kumuelewa Lisu yaani ni sawa na kizima Moto wa petrol kwa maji.

Magufuli kasimama juu ya sheria kuakikisha kila kitu anakipiga kabali kuakikisha upinzani haupumia lakini cheki sasa upepo umemgeuka yeye ndio ananyimwa pumzi na upinzani.


#NI YEYE
 
Wamekosa weledi na ni aibu kwa shirika kubwa kama hilo kutozwa faini..huwezi kuruhusu hewani habari ya kutuhumu bila kupata mrejesho kwa mtuhumiwa..

Hiyo katika uandishi inaitwa story balancing. Hapo wamesaidiwa kuongezewa skills za uandishi.
Na wewe uwe na akili, sio kila unaloambiwa unaamini. Magufuli na wafuasi wake hawawezi kuipiga faini BBC, anachoweza ni kuvifokea na kuvitisha akina Radio free pekee.
 
Hapana.. sio kweli.. vyombo vya habari vinamuandika ila sio kwa namna mnayotaka nyie chadema kwamba aaandikwe kila siku yeye tu. Kwa lipi sasa au hilo la kusema corona ipo, amesema akipita atajiongezea muda?

Kuhusu televisheni au redio inakuwa ngumu sana kumpa airtime kwa sababu hajui kuongea ila anaropoka. Mwisho wa siku kinabaki chombo cha habari yake.

Kuhusu vituo vya
 
Kama hamjahamaki kwanini mnaviminya vyombo vya habari na kuzuia Uhuru wa vyombo vya habari .. Ile fine mliyowapiga BBC ya kazi gani kama kweli hammuogopi Lissu !?

Au mkuu umeamua kujitekenya na kucheka mwenyewe!?
 
Kama hamjahamaki kwanini mnaviminya vyombo vya habari na kuzuia Uhuru wa vyombo vya habari .. Ile fine mliyowapiga BBC ya kazi gani kama kweli hammuogopi lissu !?

Au mkuu umeamua kujitekenya na kucheka mwenyewe!?
Kama vipi vyombo vya habari..au ulitaka aandikwe Tundu Lisu kila siku? Kwa lipi sasa alilofanya kwa nchi hii.. akitaka aandikwe kila siku yeye aende Kenya.
 
Serikali haijazuia habari za lissu ila vyombo vya habari imeona anaongea pumba zaidi..kama ak8jirekrbusha wakati wa kampeni watampa airtime.
Kumbe ili upate airtime BBC, Star TV. ITV, clouds tv ni kwa hisani ya serikali? Duh nimejuwa Leo hi kitu.
 
Hivi bado tunatafuta wale 'wasiojulikana' waliommiminia Lissu risasi?
Jeshi halina macho hili. IGP anadai hata Lisu bado jeshi lake linamtafuta na halijampata kwa ajili ya mahojiano kuhusu tukio la kushambuliwa kwake.
 
Nina imani CCM bado ina watu wachache wakini, wajaribu kushauri hili jambo....wasije wakakimbilia option nyepesi kwao ya kumkata jina hiyo inaweza kuwa ni mbaya zaidi.
 
Kumbe ili upate airtime Bbc star tv. Itv couds tv ni kwa hisani ya serikali? Duh nimejuwa Leo hi kitu.
Sasa kuna kituo ambacho kinaruhusu matusi?? Muwe mnajitafakari au anzisheni TV yenu mbona mna pesa nyingi tu. Muwe mnatukana
 
Ahahaha kweli aisee kama wamefanya mengi yenye tija hofu ya nini
 
Ngoja nimsaidie kujibu: BBC wamepigwa fain kwa kurusha matangazo ya mahojiano yao na Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia CHADEMA Ndugu Tundu Antipas Lisu.

Kwa ujibuji huu ndo maana o-level nilipata one
Hongera mkuu kwa kupàta one
 
Mwaka huu vitu vyenye ncha kali lazima viwaingie CCM ...
Wameingiziwa na mkuu wao lakini sasa ni zamu ya malofa kufanya yao ...

Mpaka kieleweke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…