Magufuli nakuunga mkono lakini kuwa makini kwenye kipindi chako cha pili

Magufuli nakuunga mkono lakini kuwa makini kwenye kipindi chako cha pili

James Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
1,205
Reaction score
1,509
Wana jamiiforum leo nimeona nitoe tathmini yangu ya Rais Magufuli na kipindi chake cha kwanza cha uongozi. Najua wengine mtachukizwa na haya ninayoyaandika lakini nimeona ni muhimu kutoa maoni yangu.

Mpaka sasa kwa watu waliosoma maoni yangu watagundua kwamba nilikuwa nikimsifia Rais wetu pale anapofanya mazuri lakini pia nikichukizwa na mambo mengine yaliyotokea kwenye serikali yake.

Baadhi ya mambo yaliyonichukiza ni kutomuadhibu Paul Makonda kwa kujichukulia sheria mkononi pale alipovamia studio za Clouds, kushambuliwa kwa Tundu Lissu bila kupatikana wahalifu, kubadilisha sheria za takwimu n.k. Nilituma maoni yangu kuonyesha kuchukizwa na mambo yote haya.

Pamoja na hayo lakini pia yabidi ni kutendee haki kwa mazuri uliyoyafanya kama kudhibiti ubadhirifu, ufisadi, ukusanyaji wa mapato ya serikali, kujenga vituo vya afya, kupiga vita uzembe n.k.

Binafsi naamini kwamba hakuna mtu duniani mwenye kuwa na uzoefu wa mambo yote ya urais, mambo mengine unajifunza ukiwa madarakani. Kwahiyo muheshimiwa rais natumaini kwamba ulijifunza mengi kwenye kipindi chako cha kwanza.

Nasikia huwa una tabia ya kupitia mitandaoni. Kwa hiyo, kama utasoma ujumbe huu nakutakia uchaguzi mwema na kama ukishinda utufanyie mengi kwenye kipindi chako cha pili.
 
Nimezingatia hii sentence [emoji1542][emoji1542][emoji1542][emoji1542]na utufanyie mengi kwenye kipindi chako cha pili.

Hapana sikuwa na maana kama lazima atashinda bro. Nitarekebisha sentensi yangu. Shukran
 
...... Pamoja na hayo lakini pia yabidi ni kutendee haki kwa mazuri uliyoyafanya kama kudhibiti ubadhirifu, ufisadi, ukusanyaji wa mapato ya serikali, kujenga vituo vya afya, kupiga vita uzembe n.k...........
Hakuna ubadhirifu wala ufisadi wowote uliodhibitiwa.

Kilichofanyanyika ni kudhibii wapiga kelele ili walaji wale kimya kimya.

Yuko wapi CAG kama watu ni wasafi.

Watu wote wanaoangalia mapato wamedhibitiwa.

Opposition parties
CAG
PAC
Media.
Sasa kusema ubdhirifu umepungua, umetumia vigezo gani au propaganda za Jiwe.

Hata hivyo vituo vya Afya ni propaganda tu.

Tangu mwaka 2015 hakuna ajira mpya za Afya za kueleweka kwahiyo wmejenga majengo ya kutunzia popo ( kama yapo )

Kumwamini Magu unatakiwa kuwa na mtindio wa ubongo.
 
Kwani tayari uchaguzi umeshafanyika?

"The NEC chairman ninampa mshahara na gari na marupurupu , halafu ashindwe kunitangaza kuwa nimeshinda ??!!".

Hiyo ni kauli iliyopata kusemwa HADHARANI; zamani ilipatwa kusemwa na kiongozi mmoja wa nchi moja ya Africa magharibi.
 
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15] Magharibi[emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Huyu Rais ni Muongo mno mno mno....siku atakayopigwa chini utaona watu wataonyesha sura zao halisi na ole wao tarehe 25 wamkate mgombea wa wananchi ndo watatujua nyambafu.
Hakuna ubadhirifu wala ufisadi wowote uliodhibitiwa.

Kilichofanyanyika ni kudhibii wapiga kelele ili walaji wale kimya kimya.

Yuko wapi CAG kama watu ni wasafi.

Watu wote wanaoangalia mapato wamedhibitiwa.

Opposition parties
CAG
PAC
Media.
Sasa kusema ubdhirifu umepungua, umetumia vigezo gani au propaganda za Jiwe.

Hata hivyo vituo vya Afya ni propaganda tu.

Tangu mwaka 2015 hakuna ajira mpya za Afya za kueleweka kwahiyo wmejenga majengo ya kutunzia popo ( kama yapo )

Kumwamini Magu unatakiwa kuwa na mtindio wa ubongo.
 
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15] Magharibi[emoji2827][emoji2827][emoji2827]

Yes, It was firstly spoken by a former president of one of West Africa countries during general election in the country in the wake of a question from one west media on how he saw the trend of the election at that time, (I don't remember the president and the country).

The same talk you hear in Tz (from mkuu wa kaya) is just a copy-paste of what was said before by the president of the west Africa who aspired at one time for second term in the office.
 
Huyu kama kashindwa kujirekebisha awamu ya kwanza sasa awamu ta pili tumpe akafanye nini? Huu ndyo muda sasa wa kumtumbua kama alivyotumbua wenzake.
 
Yes, It was firstly spoken by a former president of one of West Africa countries during general election in the country in the wake of a question from one west media on how he saw the trend of the election at that time, (I don't remember the president and the country).

The same talk you hear in Tz (from mkuu wa kaya) is just a copy-paste of what was said before by the president of the west Africa who aspired at one time for second term in the office.
giphy.gif
 
Huyo rais aliye tamka huo upupu bado tunaye duniani?
 
Awe makini kipindi gani cha pili??? Kuanzia November 2020 atakuwa Chato anaugulia maumivu ya kupigwa vibaya na Lissu kwenye sanduku la kura!!
 
Ajawahi pambana na ufisadi bali ametumia fimbo ya ufisadi kuwashughulikia wapinzani wake,si muwazi juu ya matumizi ya kodi zetu,anakopa huku anatudanganya hela za ndani,anatuburuza na ngombe zake,si kwamba ameleta uadilifu makazini bali woga na vitisho na kuwafanya watu wawe masikini ili wamuabudu sababu ya ugumu wa maisha watumishi wanamugopa sababu ya njaa na sio wanamuheshimu.Hakuna chuo kinachofunja uraisi bali kukubali kushaurika ni chuo tosha na sio one man show ziko to total failure.
Akirudi kipindi cha pili ni mwanume
 
Back
Top Bottom